Lissu: Nimepata taarifa kwamba kuna mkakati unaandaliwa wa kunivua Ubunge

Madimba jr

JF-Expert Member
Aug 12, 2017
1,577
3,143
BAADA YA RISASI KUSHINDWA, SASA WANATAKA KUNIVUA UBUNGE!!!!

Nimepata taarifa, kutoka kwa watu wawili tofauti, kwamba kuna mkakati unaandaliwa wa kunivua Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki. Mkakati huo unaihusisha Ikulu ya Rais John Magufuli na uongozi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Spika Job Ndugai.

Hoja inayojengwa na wakubwa hawa ni kwamba mimi ni mtoro wa Bunge. Yaani sijamwandikia Katibu wa Bunge taarifa yoyote ya maandishi kuhusu kuumwa kwangu wala matibabu yangu, n.k. Kwa maneno mengine, sijahudhuria vikao vya Bunge tangu tarehe 7 September, 2017, hadi sasa bila sababu au taarifa yoyote rasmi.

Sina sababu yoyote ya kutilia shaka taarifa hizi. Walionipatia ni watu wenye dhamana kubwa Bungeni na kwenye Serikali ya Magufuli.

Sijashangazwa na kuwepo kwa mkakati huu. Visasi na chuki ndiyo umekuwa utamaduni wa kawaida ya Serikali ya Magufuli. Kilichonishangaza ni hoja zinazojengwa kuhalalisha uovu huu.

Ni taarifa gani ya maandishi watu hawa wanahitaji wakati nilishambuliwa nikiwa kwenye vikao vya Bunge Dodoma.

Nilipelekwa Nairobi nikiwa sijitambui kutokea Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma, baada ya kikao kilichomshirikisha Katibu wa Bunge wakati huo, Dr. Thomas Kashilila, Spika Ndugai na Naibu Spika Tulia Ackson.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Katibu Mkuu wake Dr. Ulisubisya Mpoki walikuwepo kwenye kikao hicho. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Mh. Mwigulu Nchemba, alikuwepo; na nilisindikizwa mpaka Nairobi Hospital na daktari kutoka Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma.

Wakati wote ambao nimekuwa kwenye matibabu uongozi wa Bunge umewasiliana kwa maandishi na mwakilishi wa familia yangu kuhusu matibabu yangu. Wametoa matamko mengi hadharani kuhusu kushambuliwa kwangu na kuhusu matibabu yangu.

Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan amekuja kuniona nikiwa hospitalini Nairobi; Balozi wa Tanzania Ubelgiji, Joseph Sokoine, amekuja kuniona hospitalini Leuven mara mbili.

Ni Spika Ndugai na uongozi wote wa Bunge, akiwemo Katibu wa Bunge, Steven Kagaigai, na maafisa wakae, ndio hawajawahi kukanyaga hospitalini kuja kumwangalia mgonjwa wao, aliyeumizwa vibaya akiwa Bungeni.

Katika mojawapo ya barua alizowahi kuiandikia familia yangu, Katibu wa Bunge Kagaigai aliahidi kwamba timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ingekuja kunitembelea Nairobi au Leuven. Mwaka mzima umepita na sijawaona.

Ni wazi, kwa hiyo, kwamba uongozi wa Bunge haujawahi kujihangaisha na mimi na matibabu yangu kwa namna yoyote ile, zaidi ya kuninyima haki zangu za matibabu kinyume na Sheria ya Uendeshaji wa Bunge.

Katika mazingira haya, ni kitu gani ambacho hawakifahamu kuhusu kushambuliwa na kuumizwa kwangu, na kuhusu matibabu yangu, ambako kunahitaji waandikiwe barua rasmi???

Na waandikiwe barua gani zaidi ya barua nne au tano ambazo wamekwishaandikiwa na kaka yangu, wakili Alute Mughwai na ambazo wameshazijibu???

Ninachoona ni hiki: walitaka nife kwa risasi. Imeshindikana. Wakataka nife kwa kukosa matibabu na huduma nyingine kama mgonjwa. Ikashindikana. Sasa wanataka kunifuta Ubunge kwa mabavu. Itashindikana vile vile.

Badala ya kuona aibu na kukaa kimya, wanataka kuzima moto kwa kuumwagia petroli. Hautazimika, utawaka zaidi. Na, kwa kufanya hivyo, watajianika hadharani ili dunia nzima ishuhudie uovu wao!!!
 
Nimekuwa nikifuatilia siasa za vyama vya upinzani hapa nchini kwa zaidi ya miaka 19 sasa, Nimekuwa muhanga wa kupigwa mabomu ya machozi kwenye siasa za Arusha. Mwisho wa siku nimeona kwamba kuwa mpinzani Tanzania kushika madaraka litabaki kuwa ndoto labda miaka 100 ijayo. Binafsi Sababu ninazoziona mpaka sasa kwamba haiwezekana ni:-

Sisimu kuwa chama dola - Kuna tofauti kati ya chama tawala na chama dola, chama tawala ni kile chama kinchoongoza serikali kwa muda flani baada ya kuchaguliwa na wananchi. Chama dola ni kile chama kinachoongoza serikali na kimeshapenyeza mizizi kwenye vyombo vya dola (vyombo vya ulinzi) kwamba chama na dola ni kitu kimoja hii tunashuhudia Tanzania kwamba wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ambao ni wenyeviti wa kamati za ulinzi kwenye maeneo yao ni makada wa chama tawala. Kwa mazingira hayo upinzani hauwezi kuchipua vizuri, hautendewi hali, unyanyasaji na kupata kila aina ya shuruba mifano iko waziwazi.

Elimu ya Uraia - Watanzania asilimia kubwa bado wamelala kisiasa, wengi hawafahamu umuhimu wa siasa kwenye maendeleo, kutokutambua haki zao kisiasa, hapo ndipo wenzetu Kenya wametuacha kwa mbali.

Kwa ufupi kwa siasa za Tz ni vyema wanasiasa kuwa upande wa chama tawala (sisimu) kuliko upinzani. sisimu hakuna unyanyasaji, kupigwa mabomu ya machozi, kufungwa rumande, kula kuku kwa mrija na ni rahisi kupiga hatua za kiuongozi UBUNGE- UNAIBU/WAZIRI - RAIS. kuliko kuwa upinzani ambapo ndoto hiyo haitakaa itimie kwa kizazi hiki labda vilembwe wetu. (Nguvu wanazotumia Zitto na Tindu Lissu i wish wangekuwa sisimu wapate nafasi kubwa za kiongozi).
 
Mnaopanga mipango mibaya kwa ajili ya Tundu Lissu hamuwezi kufanikiwa mnashindwa kujifunza mlipotaka kumuua mlindwa bado mnahangaika kumvua ubunge ??? Mnashindwa kuelewa kwamba mipango ya shetani haijawahi kufanikiwa

Kiuhalisia, hukutakiwa kuwa mbunge mpaka sasa,umekidhi vigezo vyote vya kuvuliwa ubunge. Shukuru Mungu unafanyiwa favor.
Huko alipo mbowe na lowasa watakiwa wamefurahia hii taarifa by the way kama ni ya kweli.
 
Nimekuwa nikifuatilia siasa za vyama vya upinzani hapa nchini kwa zaidi ya miaka 19 sasa, Nimekuwa muhanga wa kupigwa mabomu ya machozi kwenye siasa za Arusha. Mwisho wa siku nimeona kwamba kuwa mpinzani Tanzania kushika madaraka litabaki kuwa ndoto labda miaka 100 ijayo. Binafsi Sababu ninazoziona mpaka sasa kwamba haiwezekana ni:-

Sisimu kuwa chama dola - Kuna tofauti kati ya chama tawala na chama dola, chama tawala ni kile chama kinchoongoza serikali kwa muda flani baada ya kuchaguliwa na wananchi. Chama dola ni kile chama kinachoongoza serikali na kimeshapenyeza mizizi kwenye vyombo vya dola (vyombo vya ulinzi) kwamba chama na dola ni kitu kimoja hii tunashuhudia Tanzania kwamba wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ambao ni wenyeviti wa kamati za ulinzi kwenye maeneo yao ni makada wa chama tawala. Kwa mazingira hayo upinzani hauwezi kuchipua vizuri, hautendewi hali, unyanyasaji na kupata kila aina ya shuruba mifano iko waziwazi.

Elimu ya Uraia - Watanzania asilimia kubwa bado wamelala kisiasa, wengi hawafahamu umuhimu wa siasa kwenye maendeleo, kutokutambua haki zao kisiasa, hapo ndipo wenzetu Kenya wametuacha kwa mbali.

Kwa ufupi kwa siasa za Tz ni vyema wanasiasa kuwa upande wa chama tawala (sisimu) kuliko upinzani. sisimu hakuna unyanyasaji, kupigwa mabomu ya machozi, kufungwa rumande, kula kuku kwa mrija na ni rahisi kupiga hatua za kiuongozi UBUNGE- UNAIBU/WAZIRI - RAIS. kuliko kuwa upinzani ambapo ndoto hiyo haitakaa itimie kwa kizazi hiki labda vilembwe wetu. (Nguvu wanazotumia Zitto na Tindu Lissu i wish wangekuwa sisimu wapate nafasi kubwa za kiongozi).
hujawahi kuwa mpinzani na huwezi kua mpinzani....njaa itakuua
 
Nitashangaa watakaohangaika na ubunge wa Lissu hali kuwa muda wake umeshaisha. Sasa hivi hakuna tena Chaguzi ndogo yanini wahangaike na nafasi ambayo tayari ime expire. Labda kama ni mbinu ya kumnyima mafao.
 
Tundu Lissu level yako si ya ubunge tena,uko kwenye level ya Urais sasa hivi,kwanini unajiangaisha na vitu vidogo vidogo,sisi tunasubiri 2020
hii hapana kwa kweli Lissu kwa urais bado sana,hawez kufikia level ya Lowassa hata kidogo,anahitaji kujijenga zaidi
 
Back
Top Bottom