Uchaguzi 2020 Lissu: Nikichaguliwa, ndani ya siku 100 za kwanza masheikh wa Uamsho wataachiwa huru

DPP kaambiwa na mahakama ama akamilishe uchunguzi ndani ya mwezi mmoja, ama aahirishe mashtaka na watuhumiwa waachiwe mpaka DPP atakapokuwa tayari.

Hiyo ilikuwa September 14 2019.

Mahakama imesemanhivyo September 14 2019.

Hata mahakama inaona hoja anayoisema Tundu Lissu.

Kwa sababu sasa hivi watuhumiwa wanapigwa danadana huku wako ndani miaka nenda rudi kwa style ya "uchunguzi unaendelea".


Ndicho kitu ninachosema kuwa hilo ni la Mahakama na SIYO la Executive kama anavyodai huyo ndugu mwingine. Tuiache Mahakama ifanye ya kwake hayo ya Lissu yatakuwa "ni kuingilia mhimiri mwingine".
 
"Nikishinda... na kule Bara nna uhakika atashinda Lissu... atanrudishia watu wangu" Maalim Seif. Hao Masheikh hakuna mtu ndani ya sisiemu anawazungumzia!
Wanawapambania magaidi wenzao
 
Lowasa aliiahidi hivyo hivyo ktk uchaguzi wa mwaka 2015 Lisu naye tena mwaka huu 2020...kuna jambo la kutafakari
Condition ni nini MKuu??? Unajua Suala wanalozungumziwa linahitaji Level fulani ya Mamalaka; Ndio maanakuna COndition kwamba "Nikiingia madarakani" Sasa Je ameingia? Refer ishu ya Babu Seya, Lowasa alisema, lakini mwisho wa siku aliyetekeleza ni aliye na mamlaka.
 
View attachment 1602807

Mgombea urais Tundu Lissu ameendelea kusisitiza na kumtaka Rais Magufuli awaachie mara moja mashekhe wa Uamsho na mahabusu wengine waliofungwa kwa hila.

Tundu Lissu ameahidi ndani ya siku 100 za kwanza atakapo ingia madarakani ataawachia mashekhe wa Uamsho kwani kesi yao haina msingi wowote.

Lissu amewauliza waislam wa nchi hii kwa nini hawapazi sauti kuhusu unyama wanaofanyiwa waislam wenzao? Hapo hapo akawaomba watumie kura yao vizuri katika uchaguzi huu ili ndugu zao waweze kuachiwa huru.

Tundu Lissu ameshangaa iweje mashekhe hao wasipelekwe mahakamani kama kweli wana kesi ya kujibu ili mahakama iweze kuamua kama wamevunja sheria ama lah.
Siku 100 za nn inatakiwa siku unaapishwa na watu waachiwe mara moja
 
Nilipinga mahakama kuingiliwa wakati Lowasa anaahidi kumuachia Seya na wanae.

Nikapinga kuingiliwa mahakama Magufuli alivyowaachia Seya na wanae.

Ninapinga kuingiliwa kwa mahakama Tundu anavyoahidi kuingilia maamuzi ya mahakama.
Hayo maamuzi ya mahakama aliyoahidi Lissu kuyaingilia ni yapi hayo?...ilihali hao masheikh hata bado hawajahukumiwa?
 
Hayo maamuzi ya mahakama aliyoahidi Lissu kuyaingilia ni yapi hayo?...ilihali hao masheikh hata bado hawajahukumiwa?
Sasa si aache mahakama iendelee kuwashikilia mpaka itakavyoonekana hawana haja ya kushikiliwa?
 
Kwa nini kila uchaguzi wanasiasa wanatumia Mashek wa uamsho kama kete ya kutaka kura? kama hao mashee wana haki kwa nini hawapewi lkn ktk kila kipindi cha uchaguzi utasikiaa wagombea wana watumia kama kete....halafu uchaguzi ukiisha hakuna atakaye wazungumzia!! Lowasa aliiahidi hivyo hivyo ktk uchaguzi wa mwaka 2015 Lisu naye tena mwaka huu 2020...kuna jambo la kutafakari
Sasa Lowassa aliunda serikali?? Angewatoa vipi katika mazingira alokuwa nayo? Yataje aliyoahidi mgombea wenu na kushindwa kuyatekelwza ndipo watu tutakuelewa maana yeye kaunda serikali na kila taasis hadi mahakama zilikuwa chini yake!
Nakusihi wewe na nduguzo tarehe 28.10.2020, Ungana nami kumpigia kura Lissu uyashuhudie hayo aloyahidi!
 
Jamani naomba yeyote aliye karibu na Mnyika afikishe ushauri huu:
Katika hiki kipindi cha wiki moja ilosalia nawasihi CHADEMA waandae bango la matangazo ya maandishi kama lile la NEC linaloonyesha idadi vituo na wapiga kura. Sasa hili la CHADEMA lionyeshe yale mambo yote atakayofanya Lissu ndani ya siku 100.

Bango hili pia kwa juu na chini liwe na picha ya LIssu iliyoko kwenye karatasi za kupigia kura. Bango liwe linarushwa kama tangazo maalum kupitia ITV .

FAIDA ZA TANGAZO HILI:
1.Itasaidia sana kuwakumbusha watu wa makundi mbali yaliyoumizwa na serikali ya CCM kwa miaka, maana ahadi hizo zinagusa karibu makundi yote ya wapiga kura.
2. Itasaidia pia kufikisha ujumbe kwa makundi ya walemavu mfano walemavu wa masikio ambao hawasikii sauti lakini wanweza kusoma maandishi.

3.Itasaidia kuifikisha picha ya mgombea wa CHADEMA maeneo mbalimbali ambako hakuweza kufika kutokana na sababu mbalimbali kama kukosa muda au kufanyiwa figisu kama zile za kunyimwa kivuko.

4.Itasaidia kuzifikisha sera za CHADEMA katika mtindoa wa summary ambayo ni short and clear!
 
Ndicho kitu ninachosema kuwa hilo ni la Mahakama na SIYO la Executive kama anavyodai huyo ndugu mwingine. Tuiache Mahakama ifanye ya kwake hayo ya Lissu yatakuwa "ni kuingilia mhimiri mwingine".
Mahakama yenyewe ilishamwambia DPP akamilishe uchunguzi au awaachie watuhumiwa ndani ya mwezi mmoja.

Hiyo ilikuwa September 14 2019.

Sijui kilichofuatia ni nini hapo.

Labda Mahakama imepata "amri kutoka juu". Kitu ambacho si sawa. Hapo itakuwa executive imeingilia judiciary.

Pia, katika kesi hizi ambazo DPP/ Jamhuri ndiye anashitaki, rais ana uwezo wa kumuagiza DPP kumaliza kesi. Kwani DPP ni sehemu ya executive. DPP anafanya kazi kwa maelekezo ya rais.Hata leo Magufuli akimwambia DPP amalize kesi, kwa sababu hii au ile, au bila sababu, basi rais atakuwa sawa.

Na DPP ana uwezo wa kumaliza kesi, kwa sababu hii, au ile, au bila kutoa sababu.

Sasa unachosema hapo ni kwamba mshitaki aiachie mahakama iamue kesi.
Wakati mahakama ilishamuambia mshitaki alete ushahidi kesi imalizwe, au kama hana ushahidi, watuhumiwa waachiwe. DPP akamilishe ushahidi kwanza.Akikamilisha arudi kuanza kesi upya. Inaonekana DPP hayuko tsyari. Anafunga watu miaka nenda miaka rudi wakati hana ushahidi wa kuendesha kesi.

Mahakamq iliona watuhumiwa kukaa lupango miaka sita bila kuhukumiwa kwa sababu "uchunguzi unaendelea", ni kama wameshahukumiwa kifungo cha miaka sita kabla kesi haijaanza.
 
Week moja kabla ya uchaguzi, maalim seif anatangaza chama chao ACT wanamsapoti Lissu kwenye nafasi ya urais, siku chache baadae mgombea wake wa urais membe anasema bado yupo kwenye competition, guys hamkuwa serious, hamkujiandaa, hamkuwa mnajua nini mnataka jipangeni 2025, bado hamjachelewa
 
16 JUNI 2021

MASHEIKH WA UAMSHO WALIOACHILIWA WATOA SHUKRANI


Siku chache baada ya maSheikh wa UAMSHO kuachiliwa wametoa asante kwa wote waliowapigania haki yao ya kusikilizwa kesi yao au kuachiliwa ikiwa Jamhuri imeshindwa kuleta ushahidi kwa miaka 8 .
 
watarudishwa kama wataendelea kuhatarisha muungano,
kiapo cha rais>>>>-nitaulinda muungano kwa gharama yoyote ile :cool:
 
54 Reactions
Reply
Back
Top Bottom