Uchaguzi 2020 Lissu: Nikichaguliwa, ndani ya siku 100 za kwanza masheikh wa Uamsho wataachiwa huru

Lissu hapa anatuonyesha, UNAFIKI wa hali ya juu sana. Anakubaliana na wengi tuonao hawa Mashekhe wamedhulumiwa na hawana hatia yoyote. Lakini anasema akipewa ridha na akawa Raisi atachukua muda wa siku 100 au miezi 3, kuwapa UHURU WAO HAO MASHEKHE, kwa nini muda wote huo, na unaamini kuwa hawana hatia, kama anataka kuhakikisha kesi yao, jee hatoweza kuwapa dhamana kwanza na ndani ya wiki mbili ama wakapandishwa kizimbani kwa tuhuma zozote ama kuachiwa huru.

Inawezekana miaka 7 uchunguzi haujakamilika na Lissu pia anahitaji siku 100???????? HUU NI UNAFIKI EXPRESS, AKATAFUTE HOJA NYENGINE, TUNAJUA HAWA MASHEKHE KINA JAMBO HADI VATICAN ITOE RUHUSA HAWATOKI.
aisee kiukweli binadamu tunatofautiana uwezo wa kuelewa. Hivi mtu unaelewa nini mtu akisema ndani ya siku mia? Akiapishwa leo kesho akawaachia au wakapewa dhamana haitakuwa ndani ya siku mia? Halafu kwa akili yako unadhani Lissu ataeleza mchakato woooote akiwa kasimama jukwaani? zile zinakuwa dondooo tu
 
"Nikishinda... na kule Bara nna uhakika atashinda Lissu... atanrudishia watu wangu" Maalim Seif. Hao Masheikh hakuna mtu ndani ya sisiemu anawazungumzia!
Wana kesi mahakamani, Sasa CCM inahusika hapo? Kama chadema wanahusika wakawatoe miaka yote huyo Lissu mwanasheria kakaa kimya Sasa anatafuta kura anajitoa ufahamu eti Hadi awe rais, kwani rais Magufuli ndo kawaweka mahabusu?
Yeye lissu ni mwanasheria aende akafungue kesi awatoe.
 
View attachment 1602807

Mgombea urais Tundu Lissu ameendelea kusisitiza na kumtaka Rais Magufuli awaachie mara moja mashekhe wa Uamsho na mahabusu wengine waliofungwa kwa hila.

Tundu Lissu ameahidi ndani ya siku 100 za kwanza atakapo ingia madarakani ataawachia mashekhe wa Uamsho kwani kesi yao haina msingi wowote.

Lissu amewauliza waislam wa nchi hii kwa nini hawapazi sauti kuhusu unyama wanaofanyiwa waislam wenzao? Hapo hapo akawaomba watumie kura yao vizuri katika uchaguzi huu ili ndugu zao waweze kuachiwa huru.

Tundu Lissu ameshangaa iweje mashekhe hao wasipelekwe mahakamani kama kweli wana kesi ya kujibu ili mahakama iweze kuamua kama wamevunja sheria ama lah.
Lissu anadhani anagombea uenyekiti wa kamati ya sendoff; kuomba kura jambo moja, unaweza kuhadaa watu kwa kila ahadi, ila ukishatangazwa na kuapishwa kuwa rais utakutana na utaratibu wa namna ya kuongoza nchi, na sio kila jambo utalipayuka jukwaani. Kuna mambo utayakuta na kuyaacha hivyohivyo.
 
Kura yako ni sawa na kuweka sukari ziwa victoria ukitegemea utakunywa chai Lissu hawezi kushinda hata viti maalum
 
Lissu amewauliza waislam wa nchi hii kwa nini hawapazi sauti kuhusu unyama wanaofanyiwa waislam wenzao? Hapo hapo akawaomba watumie kura yao vizuri katika uchaguzi huu ili ndugu zao waweze kuachiwa huru.

Tundu Lissu ameshangaa iweje mashekhe hao wasipelekwe mahakamani kama kweli wana kesi ya kujibu ili mahakama iweze kuamua kama wamevunja sheria ama lah.
Hapa kateleza.

Ni matumaini yangu kwamba atajirekebisha makosa kama haya.

Hao Mashekh ni waTanzania.

Ni ndugu wa waTanzania wote na sio wa waislam pekee. Ni wajibu wa waTanzania wote kupaaza sauti kila mTanzania wa aina yoyote anapoonewa.

Akianza kuweka watu katika makundi, hata yeye hatakuwa tofauti na huyo anayetafuta kumng'oa kwenye kiti.

Uonevu kwa mTanzania yeyote ni lazima ukataliwe na umma wa waTanzania bila kujali dini, kabila au jinsia zao.
 
Mimi muumini wa sheria na kisheria walitakiwa wafunguliwe mashtaka hukumu itolewe ila kuwafunga watu miaka bila kesi hilo tatizo kubwa lakini nataka niende mbali kidogo tusitumie hii issue kisiasa zaidi kupatia kura ila iwe ni kwa wote ambao kwa sababu moja au nyingine wako ndani au mahabusu bila kuhukumiwa kinyume sheria wafanyiwe haki. Hapa angesema siku 100 za mwanzo nitahakikisha mahakama inasimama kama huru na sheria za kesi zinafuatwa maana sheria ziko na makosa yote kuwa na dhamana na sheria za dhamana ziko haki itendeke kwa wote.
Anayewashikilia hao Mashehe ni Serikali/executive na siyo Mahakama.
Serikali kupitia DPP inaweza kuifuta kesi hiyo muda wowote.
 
Ni kweli lakini wote tunajuwa DPP ni nani na anafanya kazi za nani, akipewa kimemo anafanya tu sio DPP wa wenzetu huko hata Rais anaweza kushitakiwa huku wote ni walewale tu.
 
Mgombea wetu anatetea magaidi? Maana wanatuhumiwa kufanya ugaidi Zanznibar, mwaka huu chama chetu kimechemka sana.
Nadhani huyo ni mgombea wenu kifamilia unafurahia utawala usiojali sheria tafakari kama ndio Baba,baba mdogo wako yuko huko jela bila kesi yoyote huo unaoita ugaidi nenda kaprove mahakamani.
 
Kwani suala lipo wapi? Halipo mahakamani.
 
View attachment 1602807

Mgombea urais Tundu Lissu ameendelea kusisitiza na kumtaka Rais Magufuli awaachie mara moja mashekhe wa Uamsho na mahabusu wengine waliofungwa kwa hila.

Tundu Lissu ameahidi ndani ya siku 100 za kwanza atakapo ingia madarakani ataawachia mashekhe wa Uamsho kwani kesi yao haina msingi wowote.

Lissu amewauliza waislam wa nchi hii kwa nini hawapazi sauti kuhusu unyama wanaofanyiwa waislam wenzao? Hapo hapo akawaomba watumie kura yao vizuri katika uchaguzi huu ili ndugu zao waweze kuachiwa huru.

Tundu Lissu ameshangaa iweje mashekhe hao wasipelekwe mahakamani kama kweli wana kesi ya kujibu ili mahakama iweze kuamua kama wamevunja sheria ama lah.
Mkashitaki kwenye Jumiya Za Kinataifaa tuwekewe Vijwazo... Maana Tukiwaambia Hakuna Cha Jumuiya za Kimataifaa Wala Nini KUNA JAMUHULI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SHERIA ZAKE...
 
View attachment 1602807

Mgombea urais Tundu Lissu ameendelea kusisitiza na kumtaka Rais Magufuli awaachie mara moja mashekhe wa Uamsho na mahabusu wengine waliofungwa kwa hila.

Tundu Lissu ameahidi ndani ya siku 100 za kwanza atakapo ingia madarakani ataawachia mashekhe wa Uamsho kwani kesi yao haina msingi wowote.

Lissu amewauliza waislam wa nchi hii kwa nini hawapazi sauti kuhusu unyama wanaofanyiwa waislam wenzao? Hapo hapo akawaomba watumie kura yao vizuri katika uchaguzi huu ili ndugu zao waweze kuachiwa huru.

Tundu Lissu ameshangaa iweje mashekhe hao wasipelekwe mahakamani kama kweli wana kesi ya kujibu ili mahakama iweze kuamua kama wamevunja sheria ama lah.
Kwanini siku mia moja? Si utamke tu mara baada ya kuapishwa? Au unajua kuna 'formalities' za kufuatwa na hapa unawafurahisha wasiojua?
 
Kauli hii moja kwa moja inaonyesha nia iliyojificha ya Lissu ya kuhakikisha Tanzania inaingia kwenye mgogoro na vurugu ili wale wanaodhaniwa kumtuma watimize azma yao ya kuitokomeza Tanzania kama alivyowahi kuahidi Lissu mwenyewe. Katika suala hili, Lissu alitakiwa kutumia lugha unganishi kwa watanzania badala ya lugha farakanishi aliyoitumia. Kutaja kuwa watanzania wa dini fulani ndiyo wahusike kufuatilia suala la namna hii inaonyesha wazi Lissu ana nia ovu dhidi ya Watanzania. Kwa hili lazima Lissu aadhibiwe kwa kunyimwa kura katika ifikapo tarehe 28/10/2020.
Hapana.

Lissu katumia mfano wa kesi kubwa.

Hao Watanzania wa dini fulani, ni Watanzania pia. Dinibyao haiwaondolei uTanzania wao.

Tena kasema na wengine, wala hajaishia kwa hao.

Ukiona dini hapo, wewe ndiye mdini.

Serikali ya CCM imejamba. Imewafunga watu miaka mingi bila kuwashitaki.

Lissu katema mate, kasema huu ushuzi unanuka tusiukubali.

Sasa wewe badala ya kumlaumu aliyejamba, unamlaumu aliyetema mate na kusema huu ushuzi unanuka tusiukubali?
 
View attachment 1602807

Mgombea urais Tundu Lissu ameendelea kusisitiza na kumtaka Rais Magufuli awaachie mara moja mashekhe wa Uamsho na mahabusu wengine waliofungwa kwa hila.

Tundu Lissu ameahidi ndani ya siku 100 za kwanza atakapo ingia madarakani ataawachia mashekhe wa Uamsho kwani kesi yao haina msingi wowote.

Lissu amewauliza waislam wa nchi hii kwa nini hawapazi sauti kuhusu unyama wanaofanyiwa waislam wenzao? Hapo hapo akawaomba watumie kura yao vizuri katika uchaguzi huu ili ndugu zao waweze kuachiwa huru.

Tundu Lissu ameshangaa iweje mashekhe hao wasipelekwe mahakamani kama kweli wana kesi ya kujibu ili mahakama iweze kuamua kama wamevunja sheria ama lah.
🤣😂🤣😂 Ukitakaa kuamini Wafuasi Wa CHEDEMA WENGI NI WAHUNI ni Leo Sugu kapita Sokoni Anaiimbiwa Rais, Rais, Rais🤣😂🤣 Nimecheka sana Sijui CHADEMA URAIS WANAUCHUKULIAJE ... Hiki chama Kinahitajii Neema ya Mungu kuwepo mpka 2025 maana Kinaongozwa Na Wahuni wapiga deal. Ila Safarii hii kimekutana Na CHUMA mwisho wake umefikaaa

HATUWEZI KUKABIDHI NCHI KWA WAHUN💪🏽
 
"Nikishinda... na kule Bara nna uhakika atashinda Lissu... atanrudishia watu wangu" Maalim Seif. Hao Masheikh hakuna mtu ndani ya sisiemu anawazungumzia!
Masheikh waliwaunganisha wazanzibar kupitia dini..hapakua na ccm wala cuf..walikuwa wanasepa na kijiji..mwishowe watu wangebinuliwa na masheikh kushika hatamu..ndomana wale hawasemi chochote..ni mwiba kooni
 
Back
Top Bottom