OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,148
- 103,551
Mgombea urais Tundu Lissu ameendelea kusisitiza na kumtaka Rais Magufuli awaachie mara moja mashekhe wa Uamsho na mahabusu wengine waliofungwa kwa hila.
Tundu Lissu ameahidi ndani ya siku 100 za kwanza atakapo ingia madarakani ataawachia mashekhe wa Uamsho kwani kesi yao haina msingi wowote.
Lissu amewauliza waislam wa nchi hii kwa nini hawapazi sauti kuhusu unyama wanaofanyiwa waislam wenzao? Hapo hapo akawaomba watumie kura yao vizuri katika uchaguzi huu ili ndugu zao waweze kuachiwa huru.
Tundu Lissu ameshangaa iweje mashekhe hao wasipelekwe mahakamani kama kweli wana kesi ya kujibu ili mahakama iweze kuamua kama wamevunja sheria ama lah.