Lissu ni mzalendo wa kweli katika nchi hii, ila ni msaliti wa kweli kwa tawala zisizo heshimu misingi ya utawala wa sheria

gemmanuel265

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
8,503
2,000
Historia ya Tundu Lissu katika kupigania misingi ya utawala bora yenye kuheshimu haki za binadamu ni kubwa sana katika nchi hii

Lissu ameanza kupigania maslahi ya nchi hii toka miaka ya 1990+ wakati huo watawala waliopo sasa wakiwa upande wa wanyonyaji wakitunga sheria mbovu za kunyonya taifa kwa maslahi yao binafasi

Lissu wakati anaanza kupigania maslahi ya taifa hili miaka hiyo ya 1990+ wakati huo watawala wakiungana na wanyonyaji wa rasilimali za taifa hili kutunga sheria kandamizi dhidi ya wananchi walimuita majina yote mabaya ili kuhalalisha dhuluma yao dhidi ya wananchi

Lissu aliitwa mpinga maendeleo, anataka kufukuza wawekezaji, ni adui wa taifa n.k, leo hii wale wale walioshiriki kutunga sheria adui kwa maslahi ya wananchi wakati huo wakiwa mawaziri waandamizi ndio wanapiga kelele kuwa tuliibiwa sana sana! Kweli wapo binadamu waliokosa sura za aibu kama mawe!

Lissu hajawahi kuwa kinyume na maslahi ya taifa hili toka kuzaliwa kwake, majina ya ajabu ajabu anayoitwa na watawala ni kwa sababu ni adui wa maslahi binafsi ya watawala na si vinginevyo

Watawala kwa sababu hawana hata chembe za uzalendo dhidi ya taifa hili ndio maana wanajaribu kutumia nguvu kubwa za dola kuaminisha wananchi kuwa Lissu ni adui wa nchi

Lissu ni adui wa viongozi mungu mtu wenye kupenda kuyasikia yale yawafurahishayo peke yake, wenye kupenda kuabudiwa, kupewa sifa za utukufu na mapambio

Leo hii tunasikia kila aina ya maneno kuwa Lissu ni msaliti wa taifa, lakini hawatoi hoja kuhalalisha madai yao hayo zaidi wanaishia kutoa vitisho tu huku hoja za kwanini aitwe msaliti zikikosa majibu yenye msingi wa madai yao

Watanzania lazima tutofautishe maslahi ya nchi na maslahi ya viongozi tuliowapa dhamana ya kutawala nchi, Magufuli, Majaliwa, Mama Samia, Ndugai n.k hawa siyo nchi ni watu tu waliopewa dhamana ya kutawala kwa muda fulani na wataondoka na watakuja wengine, lakini nchi ipo na itaendelea kuwepo milele

Lissu hawezi kamwe kumsifia na kumpigia mapambio mtu anayemtuhumu kuendesha zoezi la mauaji dhidi yake

Lissu hajawahi kuwa adui wa nchi wala hajawahi kutuhumu nchi kuhusika na shambulio dhidi yake.Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,096

Puuumba kabisaa. Yaani wewe Mwakibinga wa kufanya mdahalo na Tundu Lisu kwa level gani uliyonayo? Umechanganyikiwa wewe tupishe
 
Kitaturu

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
6,077
2,000
Puuumba kabisaa. Yaani wewe Mwakibinga wa kufanya mdahalo na Tundu Lisu kwa level gani uliyonayo? Umechanganyikiwa wewe tupishe
Kuna kila dalili kuwa, umekosea njia....!

Mwakibinga anaingiaje tena hapo?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom