jackline1
JF-Expert Member
- Oct 11, 2012
- 2,142
- 2,688
Hii avatar yako na wewe ni verified user haiwezi kweli kukuletea matatizo kwa wenye dunia?? Yaani Muingereza au Mmarekani anaweza kukunyima Visa-anyway I was just thinking aloudKitendo cha Lissu mara tu baada ya kusomwa kwa ripoti ya Prof: Mruma na Ossoro kwamba Acacia hawatalipa deni wanalohisiwa kudaiwa na badala yao wao ndiyo watatushitaki mahakamani, ndicho kinawachochea Acacia kuwa wajeuri kwa madai wanayopelekewa?
Inakuwaje tuliambiwa "wamekubali kulipa" lakini sasa kila leo wanatoa matamko kuonesha kwamba hawadaiwi na hawajui madai ya sasa yanatokana na nini? Jee Lissu ndiye anayewapa kiburi ama wana hoja za msingi kupinga wanachotakiwa kutulipa?
Inawezekanaje Lissu wakati ule alipingana na Maprofesa wawili ambao walitoa ripoti zao kwa Rais, na leo tena ionekane kwamba na Acacia nao hawaziamini ripoti za Maprofesa wale. Jee zile ripoti zimeandikwa nini na kwa nini Lissu alizipinga jee aliziiona ama aliona tu zile taaarifa fupi (Summary) za ripoti zenyewe?
Ni kwa nini mwenendo na matendo pamoja na misimamo ya Acacia ifanane na ya Lissu kwenye hili jambo. Au Lissu na Acacia ndiyo wako kwenye upande wa ukweli dhidi ya uzushi wa kisomi? Kwa nini Serikali haijibu hoja za Lissu badala yake inaishia kumwita mtetezi wa wezi?
Lissu alisema tutashitakiwa, na sasa Acacia nao wanaonekana kuelekea kwenye njia ya kutushitaki. Jee Lissu angesikilizwa wakati ule kama taifa tungepata faida gani ama tungepata hasara gani tofauti na hali ilivyo hivi sasa?
Mpaka hapa tulipofikia Lissu alikuwa sahihi ama waliokuwa wanampinga ndiyo walikuwa sahihi? Tangu sakata hili lianze tumepata nini na tumepoteza nini na uko mbele ya safari tutapata nini na tutapoteza nini?