Lissu: Naishi kwenye makazi ya balozi(Ujerumani) kwa sababu maisha yangu hayako salama, nitarejea Ubelgiji

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,995
2,000
Unakumbuka baada ya alitekua mjumbe wa Tume ya Katiba Mpya Dr. Sengondo Mvungi kuua kinyama na watu walioitwa majambazi zoezi zima lilivurugika na wajumbe wote waliokua wamebaki hai walijawa na hofu mpaka Leo ndio wamejisalimisha na kuungana na wapinga katiba mpya.
Wajumbe waliokua wametumia mbilioni ya fedha za watanzania leo wanasema kwa wazi kabisa kuwa hawako tayari kuona katiba mpya inapatikana Tanzania mana itakwamisha maendeleo.

Jiulize kitu gani kimewatia hofu wajumbe waliobaki hai? Je, huoni kuwa mauaji ya kinyama ya Dr. Sengondo ndiyo yaliyowatia hofu ? Huoni kuwa waliofanya njama za kijambazi kumuua Dr.Sengondo bado wapo na ndio waliojenga mazingira ya kuwatia hofu akina Kabudi ,Polepole, na Wengineo ?

Ni MTU mwenye Roho ya kimungu Pekee asiyeogopa kifo lakini wengine wote wanaogopa kifo!!

Shetani kwa muda Mrefu ameutawala ulimwengu kwa sababu alikua ameshikilia funguo za Mauti . Mauti ndiyo tishio kwa watu.
Wakristo na waislam wanaamnini katika ufufuo siku ya kiyama. Imani hiyo ndiyo raraja kuu ya kuondoa hofu ya kifo mana wanaoua hawana mamlaka ya kuwapeleka marehemu popote baada ya kifo.
Yaani akisha muua binadam mwenzake kazi inakua imeishia hapo hana la kufanya tena kwenye nafsi ya marehemu.

Mpaka sasa jambo baya kabisa kumtendea binadamu ni kuua mana kila mmoja anatamani kuishi !!
Wanaoshabikia kuuawa kwa wengine bila hatia ni wale wanaofanya kazi za kumwakilisha shetani duniani japo kila siku tunasafiri kuelekea siku ya kufa. Kila mnapofurahiya siku kuongezeka lakini mfurahiye pia siku kupungua kwenye zile siku zilizopangwa na Mungu.
 
Aug 13, 2020
7
45
Kweli upinzani kwisha kabisa naona humu ndani karibia wote tunamponda Lisu tukipiga kura humu jamiforum bado magufuli anashinda urais
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,995
2,000
Ninaelewa baadhi ya mambo mengi uliyoandika hapo kwenye gazeti hilo la nipashe.
Ila kwa kifupi, Mungu ndio anapanga nani awe kiongozi, dua lako la kuku halitompata mwewe. Pili, kelele za chura hazimnyimitembo kunywa maji.
Mungu anapanga lakini ukumbuke kuwa Duniani kuna roho ya nuru na roho ya giza .
Hizi zote zina nguvu kama ilivyo kwa usiku na mchana. Yote ni masaa 12.

Aina ya utawala unaoishi kwa ufahari na maslahi makubwa na kila aina ya mamlaka mkubwa kwa kodi za watu wote lakini unabagua watu huwezi kuuita utawala wa Mungu.

Yesu hakukosea aliposema tuombe siku zote kuwa Ufalme wa Mungu uje?
Alijua kuna ufalme wa Giza au shetana ambao upo hivyo tuombe wa Mungu uje.

Suala sio Dua la kuku mana kwa Tanzania ukishabikia mauaji ujue sio muda mrefu yaterejea kwenye familia yako.
Unajua Msigwa na JPM ni MTU na mkwe wake!!
Unajuaje kama Mimi na wewe watoto wetu hawataoana au wajukuu zetu?
Ndio maana tunapinga taifa la watu wanaojengeana chuki za kuuana kwa sababu ya vyama visivyo na roho wala nafsi.
Kwani CCM ikifa kihalali au chadema watu si watabaki hai? Lakini mkianza kuwamaliza watu ili CCM ibaki itabaki na nani?
Hamuoni jinsi taifa lilivyopooza kwa ushindi wa 84%+ ?
Huoni ni bora mngeshinda kwa 51% ya hapali na furaha ingekua kubwa sana na kila mtu angempania mwenzake awamu ijayo na watu wangeishi kwa raha na upendo.?

Unategemea nini Siku Simba ishinde yanga kwa Goli kumi na mbili za kubebwa na refa wazi wazi ?
Huoni ni bora Ingeshinda Goli moja la halali na kwa haki kuliko kumi na mbili ya dhulma? Huwezi kukubali ukweli wa asili mpaka asili itakapokuhukumu mana Damu hua inalipwa kwa damu. Hakuna mbadala wa Damu ya MTU inapomwagwa ardhini. Ni kanuni ya asili.
 
Samwel Jr

JF-Expert Member
May 9, 2020
1,053
2,000
Huyo bhana haishiwi hoja za kijinga kwa Tanzania ipi? Wakat kote wamewajaza wenzao

Asilete ujinga wake ulaya
 
Chesi20

JF-Expert Member
Nov 1, 2020
291
250
Mungu anapanga lakini ukumbuke kuwa Duniani kuna roho ya nuru na roho ya giza .
Hizi zote zina nguvu kama ilivyo kwa usiku na mchana. Yote ni masaa 12.

Aina ya utawala unaoishi kwa ufahari na maslahi makubwa na kila aina ya mamlaka mkubwa kwa kodi za watu wote lakini unabagua watu huwezi kuuita utawala wa Mungu.

Yesu hakukosea aliposema tuombe siku zote kuwa Ufalme wa Mungu uje?
Alijua kuna ufalme wa Giza au shetana ambao upo hivyo tuombe wa Mungu uje.

Suala sio Dua la kuku mana kwa Tanzania ukishabikia mauaji ujue sio muda mrefu yaterejea kwenye familia yako.
Unajua Msigwa na JPM ni MTU na mkwe wake!!
Unajuaje kama Mimi na wewe watoto wetu hawataoana au wajukuu zetu?
Ndio maana tunapinga taifa la watu wanaojengeana chuki za kuuana kwa sababu ya vyama visivyo na roho wala nafsi.
Kwani CCM ikifa kihalali au chadema watu si watabaki hai? Lakini mkianza kuwamaliza watu ili CCM ibaki itabaki na nani?
Hamuoni jinsi taifa lilivyopooza kwa ushindi wa 84%+ ?
Huoni ni bora mngeshinda kwa 51% ya hapali na furaha ingekua kubwa sana na kila mtu angempania mwenzake awamu ijayo na watu wangeishi kwa raha na upendo.?

Unategemea nini Siku Simba ishinde yanga kwa Goli kumi na mbili za kubebwa na refa wazi wazi ?
Huoni ni bora Ingeshinda Goli moja la halali na kwa haki kuliko kumi na mbili ya dhulma? Huwezi kukubali ukweli wa asili mpaka asili itakapokuhukumu mana Damu hua inalipwa kwa damu. Hakuna mbadala wa Damu ya MTU inapomwagwa ardhini. Ni kanuni ya asili.
Wewe una hekima na busara.
Kuna baadhi ya mambo umeandika hapo juu ambayo ninakubaliana nayo 100%.
Yale nisiyokubaliana nayo kimsingi mm naona una haki ya kusema hapa kama mm nilivyotoa maoni yangu.
Barikiwa saaana mtu wa Mungu.
 
Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
10,152
2,000
Lisu katoa tahadhari ile ile kama aliyoitoa awali kabla ya shambulio la kwanza kule Dodoma, Wenye Akili timamu watamwelewa vizuri lakini wenye ushetani mwingi watakuja na maneno ya kipumbavu zaidi na kutomuogopa mungu
Mwanaume mzima unajipeleka mwenyewe! Unalishwa, unapewa chumba na mwenzio, unaacha mkeo na watoto aaargh!
Haya Mambo ya haki za binadamu anayotetea anapata huko?
 
mwaimu Jt

JF-Expert Member
May 7, 2017
809
500
Huu upumbavu ndiyo umeikosesha CCM kura mpaka NECCCM Tumeccm wakurugenziccm na Polisiccm wakaamua kuubaka kuunajisi kuulawiti uchaguzi mkuu kwa njia haramu za kishetani maana hakuna Mtanzania mwenye Akili timamu anaweza kuipa kura yake CCM kutokana na kusheheni watu wapumbavu kama wewe
UNAFIKIRI KWA MAKALIO, tofauti ya kura milioni kumi unasema umeibiwa? ila kwa sasa sishangai tena hii fashion sasa kila anaeshindwa anadai kaibiwa, lissu, trump, n.k.
 
JET SALLI

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
1,143
1,500
Hatia ni hatia tu huwezi kushinda UCHAGUZI kwa kishindo alafu ukabaki unamuogopa mtu ambae hata wabunge wawili hana nchi nzima na bunge zima.sasa hiyo ni akili au matope.tuache kutawaliwa na ujinga.kama wameshinda kwa HAKI basi wafungue mitandao ya kijamii.Dhamira humsumbua sana mwizi akijua amemwibia maskini.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom