Lissu: Naishi kwenye makazi ya balozi(Ujerumani) kwa sababu maisha yangu hayako salama, nitarejea Ubelgiji

Nchi imekuwa ya hovyo kabisa hii!!
Ondoka utuachie nchi hovyo wewe uende huko kuzuri. Mtu halazimishwi kuishi mahali, ndiyo maana kuna international immigration. tutafutane nikuelekeze namna ya kupata legal immigration kwenda popote unapotaka, hata ukitaka Burundi au DRC utakwenda! Hata kwa Kagame napo inwezakana. Kama unatamani Juba, njia ipo.
 
Hao walompigia sim kama sio watu wake aweke mawasliano hapa. Hakuna anayetaka kumuua aache kujitisha

Ila kama anapenda kuishi ubalozini vile
Mwanzoni mliongea hup upumbavu lakini mwishowe ukaenda Dodoma na Bashite na akina cyprian Musiba mkaenda kumpiga risasi na sasa katoa tahadhari lazima watu wawe makini na yeye binafsi ajihami
 
Ondoka utuachie nchi hovyo wewe uende huko kuzuri. Mtu halazimishwi kuishi mahali, ndiyo maana kuna international immigration. tutafutane nikuelekeze namna ya kupata legal immigration kwenda popote unapotaka, hata ukitaka Burundi au DRC utakwenda! Hata kwa Kagame napo inwezakana. Kama unatamani Juba, njia ipo.
Wewe ni mnufaika wa bajeti kubwa ya blackmail uonevu unyanyasaji uovu mateso kwa wapinzani
 
Sawa, hata kama serikali ya sasa hivi haitoi uhuru huo uliosema, je ni busara kwenda kusemea nchi za nje kuhusu mapungufu ya nchi yako??

Unategemea hao wazungu watamsaidia Lissu kutatua hayo mapungufu ya serikali ya Tanzania bila malipo yoyote??
Mkoloni kaburu mweusi hatou uhuru wa kuongea ukiwa Tanzania lakini wapinzani wakaongee popote Duniani
 
Alikuwa na Tiketi ya kurudi tayari kwahiyo hakuna jipya hapo ni kick kwa Pikipiki
Huu upumbavu ndiyo umeikosesha CCM kura mpaka NECCCM Tumeccm wakurugenziccm na Polisiccm wakaamua kuubaka kuunajisi kuulawiti uchaguzi mkuu kwa njia haramu za kishetani maana hakuna Mtanzania mwenye Akili timamu anaweza kuipa kura yake CCM kutokana na kusheheni watu wapumbavu kama wewe
 
Mpumbavu huamini kila kitu,watu mnalipuka kwa habari za kupikwa. Hivi serikali ya Magufuli ilivyo busy hivi inaweza kujihangaisha na huyo Mbeligiji kweli?.Chadema kuna genge la maharamia kwelikweli ndio hao wanao mtaishia Mbeligiji. Genge lilelile lililomtoa chacha wangwe bado linarandaranda Ufipa kuona nani anataka kumchallenge mwenyekiti mpendwa.
Busy ipi hiyo? Kuwabambikia kesi wapinzani ni kuwa busy? Uharamia unao wewe shetani unayepanga kumuua Lisu akafu kwa ufala wako unataka akae kimya kwa vigezo vyako vya kishamba na kipumbavu,
 
Lengo la Lissu lilikuwa ni kuanzisha vurugu nchini ili mataifa ya nje (mabeberu) waingilie kati na kumwondoa JPM kwa nguvu ili wamweke yeye. Ccm na serikali walilijua hilo mapema sana ndo maana wakati wa kampeni walimwacha afanye anavyotaka bila kuchukua hatua yoyote (Polepole alisema hawatamshitaki ng'oo)

Sasa plan imebuma, watanzania wamemshitukia, kwa anatafuta njia ya 'nitoke vipi'!
Aende zake huko Belgium, tena haraka tu!
CCM ndiyo yenye lengo la kuanzisha vurugu kwa kuubaka kuunajisi kuulawiti uchaguzi mkuu kwa njia haramu za kishetani, hakuna kilichobuma kwa Lisu kwa maandamano yalikuwa tarehe 2 lakini nyinyi wapumbavu tarehe 1 mkawakamata viongozi wa ACT na chadema siku moja kabla
 
Hivi wewe una uhakika gani huyo Lisu anayoyasema ni ya ukweli au ni firigisu ili kuleta mkangany’iko kwenye jamii yetu??
Mara ya kwanza aliposema anataka kushambuliwa mlikuja na maneno ya kibwege kama haya matokeo yake akina cyprian Musiba wakatekeleza shambulio
 
Jamani ukistaajabu ya Musa utayashangaa ya Lisu, jamaa si kwamba anadigree ya sheria tu hata ya masta ya uongo anayo. Kwa sasa Lisu ni kama galasa yaani hana madhara yoyote yeye labda baada ya uchaguzi kuisha atulie afanye shughuli zake hakuna mtu mwenye shida naye labda aanze kuzingua. Chadema havi sasa tunavyo ongea ni kama chama cha UMD au NRA yaani hakina madhara tena kwa CCM sasa iweje atafutwa kuuliwa.
Enzi za Lisu na Chadema ndiyo baibai itabaki historia kuwa tulikuwa na chadema kama tunavyosema tulikuwa na NCCR Mageuzi au CUF wako wapi leo. Lisu anatafuta umashuhuri wakati hana leo huo umamashuhuri, yeye anatakiwa kurudi Ufipa na kujenga chama na ajue kuwa kujia hii ni nchi ya amani na utulivu kama ataamua kuukana uraia wa Ubeligiji arudi home kuendelea na maisha ya mchangani kama wengine naye aju
Tanzania hakuna Amani bali kuna uvumilivu tu, Tanzania ni kisiwa cha uvumilivu tu hakuna Amani, mara ya kwanza alitoa tahadhari kama hizo wapenda ushetani mkaja na maneno ya kipumbavu kama haya matokeo yake cyprian Musiba na wenzake wakamshambulia kwa risasi, sasa kaja na tuhuma kama za awali mnakuja na maneno yale yale ya kubeza kienyeji kipumbavu wakati kuna Hatari mbele, acheni ushetani wenu huko Belgium bila wewe kumpiga risasi angefikaje?
 
Lisu katoa tahadhari ile ile kama aliyoitoa awali kabla ya shambulio la kwanza kule Dodoma, Wenye Akili timamu watamwelewa vizuri lakini wenye ushetani mwingi watakuja na maneno ya kipumbavu zaidi na kutomuogopa mungu
 
Tundu Lissu akihojiwa na redio Ujerumani DW anasema amepata simu za kutishiwa amani na ameamua kujificha kwenye makazi ya Balozi wa Ujerumani

Anasema maisha yake yako hatarini na anajipanga kuondoka na kurudi Ubeligiji

Tundu ni mwanasheria na very treak man tujihadhari naye sana

=========

LISSU: Niko katika makazi ya balozi wa Ujerumani, Dar es Salaam tangu siku ya Jumatatu.

MWANDISHI: Kulikoni?
LISSU: Naishi kwenye makazi ya balozi kwa sababu maisha yangu hayako salama tangu siku ya Jumamosi iliyopita, napata ujumbe wa kunitishia maisha kwa hiyo niliondoka nyumbani kwangu siku ya Jumapili na siku ya Jumatatu nikaenda ubalozini, nikafatwa na askari polisi wa Tanzania wakiwa kwenye magari mawili, nikakamatwa nikapelekwa kituo cha polisi Central na isingekuwa uwepo wa maafisa wa kibalozi wa Ujerumani siku hiyo pengine nisingerudi nyumbani kwangu.

MWANDISHI(LILIAN MTONO): Unasema kwamba ulianza kupata vitisho siku ya Jumamosi kabla hujahamia kwenye makazi ya balozi, ni vitisho vya aina gani ulivipata na nani hasa alikuwa anakutisha?
LISSU: Siku ya Jumamosi nilipigiwa simu na mtu ambae hakujitambulisha akaniambia kwamba, mheshimiwa maagizo tuliyopewa ni kumalizana na wewe, once and for all na baadae kidogo nikaletewa simu nyingine na mtu mwingine aliniambia hivyo hivyo kwamba mheshimiwa oda ya kukumaliza imetolewa kwa hiyo kama unaweza kujiokoa jiokoe.

MWANDISHI: Kwa hiyo hawa waliokupa taarifa ni wale waliotumwa ama labda ni wasamaria wema?
TUNDU LISSU: Nafikiri kwa jinsi walivyojitambulisha ni wako katika hilo kundi la watu waliotumwa lakini hawakubaliani na mambo haya.

MWANDISHI: Utakuwa hapo hadi lini?
TUNDU LISSU: Nitakuwa hapa mpaka hapo usalama wangu utakapohakikishwa, sipendi kukaa hapa, mimi ni mtu mwenye shughuli nyingi kwa hiyo nataka niondoke hapa haraka iwezekanavyo na bahati mbaya siwezi nikajua itakuwa lini kwa sababu wale wanaopaswa kuhakikisha usalama wangu wanaonekana kama hawataki kujicommit kwamba kama nikitoka nje nitakuwa salama.

MWANDISHI: Kwanini unasema hivyo?
LISSU: Kwa sababu tangu nimekuwa hapa kumekuwa na jitihada za mabalozi wa nchi mbalimbali kuiambia serikali ya Tanzania kwamba haya mambo yanatokea sio masuala sahihi na mpaka sasahivi hizo jitihada hazijafanikiwa bado.

MWANDISHI: Utakapofanikiwa kuondoka, utabakia nchini au utarudi Ubelgiji?
LISSU: Nitaondoka kurudi Ubelgiji kwasababu hali ya usalama sasa hivi sio nzuri hata kidogo, hivi vitisho ni vitu ambavyo lazima nivichukulie kwa uzito mkubwa na wa kipekee.

MWANDISHI: Bado unajiona utasimama tena kwenye kinyang'anyiro kijacho cha Urais na utaendelea na harakati zako za kisiasa?
LISSU: Tuombe Mungu atupe uzima tujue miaka inayokuja itatuweka vipi lakini nachoweza kusema waziwazi ni kwamba harakati ni maisha yangu.
Lisu anakimbia kivuli chake, dhamiri yake ndio inamsuta kwa maneno na matendo yake juu ya nchi yake.
 
Wenye 'Maono' yetu 'makubwa' tena 'yaliyobarikiwa' kabisa 'tulionya' hapa hapa JF kuwa TL asirejee 'Mkatudharau' na 'Kutupuuza' acha yamtokee.

Yes, kwa sababu anayemtafuta sio ccm wala serikali

He is out there for other reasons
 
Nchi imekuwa ya hovyo kabisa hii!!
Ninyi ndiyo mmemkosesha ndugu Lissu kuaminika mbali na mwendenendo wake juu nia yake isiyo eleweka kuhusu kuendelea kuwepo kwa nchi yetu Tanzania.Maana amewahi kunukuliwa akisema jambo la ovyo na la kushangaza juu ya kuendelea kuwepo nchi ya Tanzania hapa Duniani
 
Alipigwa risasi na mpka leo hakuna aliyekamatwa lissu ana haki ya kuogopa kila kitisho juu ya maisha yake yeyote anayekebehi hili ndo nyie mshazoea kumwaga damu...
 
Hivi mtu mwenye njia ya kukudhuru anakuambia kabisa jiandae nakuja kukumaliza/kukudhuru kama unaweza jiokoe

Acheni usanii

Sehemu ya genge ambao hawakukubaliana na hicho kitendo ndoa walitoa taarifa kama wasamalia wema tu
 
Ili iwe fundushisho kwa wavurugaji wote wa nyakati za sasa na zijao, moja: wahakikishe nchini hachomoki, mbili: anashitakiwa na kutiwa hatiani, na tatu: hukumu atakayopata iwe ni ya kifungo cha jela tena cha muda mrefu miaka 30.
Ungezijua sheria za kimataifa ,MTU akishakimbilia ubalozi wowote tayari yuko chini ya taifa lingine.
 
Back
Top Bottom