Lissu: Naishi kwenye makazi ya balozi(Ujerumani) kwa sababu maisha yangu hayako salama, nitarejea Ubelgiji

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,317
Tundu Lissu akihojiwa na redio Ujerumani DW anasema amepata simu za kutishiwa amani na ameamua kujificha kwenye makazi ya Balozi wa Ujerumani

Anasema maisha yake yako hatarini na anajipanga kuondoka na kurudi Ubeligiji

Tundu ni mwanasheria na very treak man tujihadhari naye sana

=========

LISSU: Niko katika makazi ya balozi wa Ujerumani, Dar es Salaam tangu siku ya Jumatatu.

MWANDISHI: Kulikoni?
LISSU: Naishi kwenye makazi ya balozi kwa sababu maisha yangu hayako salama tangu siku ya Jumamosi iliyopita, napata ujumbe wa kunitishia maisha kwa hiyo niliondoka nyumbani kwangu siku ya Jumapili na siku ya Jumatatu nikaenda ubalozini, nikafatwa na askari polisi wa Tanzania wakiwa kwenye magari mawili, nikakamatwa nikapelekwa kituo cha polisi Central na isingekuwa uwepo wa maafisa wa kibalozi wa Ujerumani siku hiyo pengine nisingerudi nyumbani kwangu.

MWANDISHI(LILIAN MTONO): Unasema kwamba ulianza kupata vitisho siku ya Jumamosi kabla hujahamia kwenye makazi ya balozi, ni vitisho vya aina gani ulivipata na nani hasa alikuwa anakutisha?
LISSU: Siku ya Jumamosi nilipigiwa simu na mtu ambae hakujitambulisha akaniambia kwamba, mheshimiwa maagizo tuliyopewa ni kumalizana na wewe, once and for all na baadae kidogo nikaletewa simu nyingine na mtu mwingine aliniambia hivyo hivyo kwamba mheshimiwa oda ya kukumaliza imetolewa kwa hiyo kama unaweza kujiokoa jiokoe.

MWANDISHI: Kwa hiyo hawa waliokupa taarifa ni wale waliotumwa ama labda ni wasamaria wema?
TUNDU LISSU: Nafikiri kwa jinsi walivyojitambulisha ni wako katika hilo kundi la watu waliotumwa lakini hawakubaliani na mambo haya.

MWANDISHI: Utakuwa hapo hadi lini?
TUNDU LISSU: Nitakuwa hapa mpaka hapo usalama wangu utakapohakikishwa, sipendi kukaa hapa, mimi ni mtu mwenye shughuli nyingi kwa hiyo nataka niondoke hapa haraka iwezekanavyo na bahati mbaya siwezi nikajua itakuwa lini kwa sababu wale wanaopaswa kuhakikisha usalama wangu wanaonekana kama hawataki kujicommit kwamba kama nikitoka nje nitakuwa salama.

MWANDISHI: Kwanini unasema hivyo?
LISSU: Kwa sababu tangu nimekuwa hapa kumekuwa na jitihada za mabalozi wa nchi mbalimbali kuiambia serikali ya Tanzania kwamba haya mambo yanatokea sio masuala sahihi na mpaka sasahivi hizo jitihada hazijafanikiwa bado.

MWANDISHI: Utakapofanikiwa kuondoka, utabakia nchini au utarudi Ubelgiji?
LISSU: Nitaondoka kurudi Ubelgiji kwasababu hali ya usalama sasa hivi sio nzuri hata kidogo, hivi vitisho ni vitu ambavyo lazima nivichukulie kwa uzito mkubwa na wa kipekee.

MWANDISHI: Bado unajiona utasimama tena kwenye kinyang'anyiro kijacho cha Urais na utaendelea na harakati zako za kisiasa?
LISSU: Tuombe Mungu atupe uzima tujue miaka inayokuja itatuweka vipi lakini nachoweza kusema waziwazi ni kwamba harakati ni maisha yangu.
 
Njama, hila na ulaghai wa Lissu umeshajulikana. Yaani kipindi chote cha kampeni hakukuwa na tishio, iweje baada ya Uchaguzi awe anatishiwa?

Asichofahamu ni kudhani alikuwa anapendwa na watanzania kumbe wananchi walikuwa wanaenda kwenye kampeni zake kumfurahisha maana alikuwa anataka Kura za huruma.

Uzuri ni kuwa hata hao Wazungu anawalilia sasa hivi wameshamfahamu kwamba ana matatizo ya kisakolojia.
 
Lisu na chadema yake ndo wa hovyo kabisa. Hakuna matisho yoyote, ila anajitahidi kuichafua nchi. Hakuna MTU mwenye time na Lisu sasa hivi, ajipange na kusubiri 2025. Hizo mbinu zimefeli kabla ya utekelezaji!!!!
Hivi mwaka ule wa 2017, wakati Tundu Lissu alipotoa taarifa za aina hii hii za vitisho, je Jeshi la Polisi lilichukua hatua gani?

Je mmeshasahau kuwa siku chache baada ya kutoa taarifa hiyo ndipo akamiminiwa risasi mfululizo kwa nia ya kumuua?

Mnataka na safari hii afanye hivyo hivyo wakati wale wauaji wake hadi leo "wanafichwa" na watawala wa nchi hii?
 
Ili iwe fundushisho kwa wavurugaji wote wa nyakati za sasa na zijao, moja: wahakikishe nchini hachomoki, mbili: anashitakiwa na kutiwa hatiani, na tatu: hukumu atakayopata iwe ni ya kifungo cha jela tena cha muda mrefu miaka 30.
 
Maelezo yako na conclusion uliyofikia kama haviendani. Awali umeeleza wasiwasi aliokua nao TL kuhusu usalama wa maisha yake hadi akaamua kuomba hifadhi kwenye makazi ya Balozi wa Ujerumani.

Sasa jinsi ulivyomalizia ndio sijaelelewa. Ni kwamba tujihadhari naye kwasababu tu ya yeye kua mwanasheria tricky au ni kitu gani? Jamaa hana jeshi, hana polisi au hata mgambo.

Hana chombo chochote cha habari pengine ataeneza propaganda zake za "kuhatarisha amani" na usalama wa nchi, na hata angekua nacho kingefungiwa na Mamlaka za Udhibiti, Hiyo hatari yake mpaka sisi tulioshinda kwa tsunami na wananchi wanatupenda kwelikweli tuanze kumuogopa iko wapi?
 
Hana lolote huyo anajaribu kupata unafuu wa kurudi Ubelgiji tu anajua sasa Ubelgiji kuna lockdown hawezi kuingia kirahisi sasa anataka arudi kwao inajulikana ana uraia tayari wa Ubelgiji sasa anataka aonekane amekwenda Ubelgiji kama mkimbizi wakati alishapata uraia siku nyingi, awadanganye mbumbumbu wenzie wanasaccos.

Tunajua alikuja Tanzania kuanzisha vurugu lakini Watanzania wamemnyoosha hakuna cha kuingia barabarani kama alivyokuwa ametumwa na mabeberu wake akina Robert Amsterdam. Yeye arudi tu kwao Ubelgiji hakuna aliyenashida naye!
 
Hana lolote huyo anajaribu kupata unafuu wa kurudi Ubelgiji tu anajua sasa Ubelgiji kuna lockdown hawezi kuingia kirahisi sasa anataka arudi kwao inajulikana ana uraia tayari wa Ubelgiji sasa anataka aonekani amekwenda Ubelgiji kama mkimbizi wakati alishapata uraia siku nyingi awadanganye mbumbumbu wenzie wanasaccos. Tunajua alikuja TZ kuanzisha vurugu lakini watz wamemnyoosha hakuna cha kuingia barabarani kama alivyokuwa ametumwa na mabeberu wake akina Robert Amsterdam. Yeye arudi tu kwao Ubelgiji hakuna aliyenashida naye!
Washeni basi mitandao ya kijamii maisha yaendelee! Hizi propaganda mfu zimeshafeli!
 
Maelezo yako na conclusion uliyofikia kama haviendani. Awali umeeleza wasiwasi aliokua nao TL kuhusu usalama wa maisha yake hadi akaamua kuomba hifadhi kwenye makazi ya Balozi wa Ujerumani.

Sasa jinsi ulivyomalizia ndio sijaelelewa. Ni kwamba tujihadhari naye kwasababu tu ya yeye kua mwanasheria tricky au ni kitu gani? Jamaa hana jeshi, hana polisi au hata mgambo. Hana chombo chochote cha habari pengine ataeneza propaganda zake za "kuhatarisha amani" na usalama wa nchi, na hata angekua nacho kingefungiwa na MAMLAKA ZA UDHIBITI", Hiyo hatari yake mpaka sisi tulioshinda kwa tsunami na wananchi wanatupenda kwelikweli tuanze kumuogopa iko wapi?
Alikuwa ana maana kuwa tujihadhari naye asije akakuingiza mkenge ukaingia kwenye jinai wakati yeye ameshaingia mitini anakuachia msala. Inajulikana yeye tayari ana uraia wa Ubelgiji kwa hadhi ya ukimbizi sasa anataka kuhalalisha kiaina!

Ili dunia ijue sasa ndiyo amepata uraia wa ukimbizi huko Ubelgiji wakati siyo kweli tangu aliporudi hapa TZ alikuwa tayari ana uraia wa Ubelgiji alikuja kuhamasisha vurugu tu ndiyo maana alikuwa anavunja sheria za uchaguzi kila mara na kwa makusudi. Yeye aende tu atuachie nchi yetu.
 
Mlikuwa mnataka muwaingize watz kwenye machafuko watz wamewashitukia sasa mmeamua kujifanya wakimbizi wakati tayari mna uraia wa Ubelgiji. Cha kushangaza kwa ninj hakukimbilia ubalozi wa Ubelgiji?
Kama Watanzania wamepuuza, washeni mitandao ya kijamii tuendelee na maisha tuliyoyazoea!
Hizo porojo nyingine sina muda nazo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom