LISSU NA LEMA WALIKIMBIA KWANINI HAWATAKI MBOWE AACHIWE

taboa

JF-Expert Member
Feb 9, 2021
399
711
Ukweli ni kwamba kwa jinsi Hali ya kisiasa na kikatiba ilivyo,nchi hii Rais anaweza fanya lolote na asitokee mtu wa kufanya fyokofyoko,ndo maana JPM alipora Uchaguzi,Ndo maana Jecha alifuta matokeo,Ndo maana Lissu alishambuliwa kikatili na mpaka leo Hakuna kinachojiri.
Lemma alikimbia kwa kuogopa kubambikiwa kesi ya UGAIDI,Lissu alikimbia mpka kwa Mabalozi kwa kuogopa kukaa ndani,Kwa Sasa Jambo liwe Mbowe kuachiwa hayo Mengine yataendelea akiwa nje.
Sasa ninapoona Lissu na Lema wanapinga Mbowe kuachiwa wakati wao wamekimbia na Mwenyekiti anateseka jela huku akishindwa kujumuika na familia yake na kuendelea na michakato yake wanakuwa hawatendi haki.
Mbowe mwenyewe anapambana kwa kutumia mawakili halafu mtu anataka azidi kuteseka jela ili iweje?kwa mfano akifungwa jela watafanya nini?Watulie mama atoe huo anauita msamaha then Mbowe akija aendelee na Madai ya KATIBA najua itakuwa ngumu kukamatwa tena.
NB:NGUVU ALIYONAYO RAIS NI KUBWA SANA HAKUNA MWENYE UWEZO WA KUPAMBANA NAYE MPAKA KATIBA ITAKAPOBADILIKA,INGAWA PIA ANATAKIWA KUMTANGULIZA MUNGU KATIKA UONGOZI
 
Mbowe ataachiwa na hilo sio ombi bali ni lazima. Yule dalali anayejifanya kuomba msamaha akakiombee chama chake, hatutaki msamaha kwa mtu ambaye hana kosa.
 
.

..Mbowe hakukamatwa na Lissu au Lema, bali alikamatwa na serikali.

..kwa msingi huo wenye uwezo na mamlaka ya kumtoa mahabusu ni serikali ambao walimkamata.
 
Back
Top Bottom