Lissu: Mwenyekiti wa Parole alipaswa awe Jaji au aliwahi kuwa jaji

Mrema anatuangusha wachaga dah!! Tulipasa kumwacha apumzike maana akili pia huchoka jameni. Pole mzee wetu Kiraracha oldboy
Ana waanhusha nini ?
Kwani yeye ni kiongozi wa wachaga au wa taifa?

Kwani alichokosea ni kipi haswa ,kwenda kupima kwa mkemia majibu ndio yatakayokufanya uwe msafi au mwenye makosa
 
Kabisa hiyo nafasi anatakiwa mtu mwenye elimu ya sheria na administration of justice sasa huyu babu hana sifa hizo, watangulizi wake wote walikuwa majaji
 
Ana waanhusha nini ?
Kwani yeye ni kiongozi wa wachaga au wa taifa?

Kwani alichokosea ni kipi haswa ,kwenda kupima kwa mkemia majibu ndio yatakayokufanya uwe msafi au mwenye makosa
Mkemia ni mtumishi wa serikali, vipi kama akiambiwa aandike kuwa unatumia? Utabishia wapi!?
 
Mrema anatetea ugali kwani asingeteuliwa kuwa mwenyekiti wa parole sukari ingeshammaliza
Ile nafasi ni kweli kutibiwa bure tu India ametoka India juzi juzi tu......ashukuru hivyo hivyo njaa mchezo....tena ikiwa kichwani!!!
 
MWENYEKITI wa Parole, Augustino Mrema amemshukia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chaydema), kuwa anafanya makosa makubwa kutetea watuhumiwa wa dawa za kulevya.

Akizunguma na MTANZANIA kwa simu jana, Mrema alisema anamshangaa Lissu kuwatetea watu wanaojihusisha na dawa za kulevya na kumshauri atumie elimu yake ya sheria kuwatetea waathirika na wanaotaja wahusika wa dawa za kulevya akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mbali na Lissu, Mrema aliigeukia mahakama itambue kuwa pamoja na kutafsiri sheria, jukumu la kuzuia dawa za kulevya lipo mikononi mwao.

“Nashangazwa na hawa wanaotuhumiwa kukataa kwenda kupimwa na kuonyesha juhudi za kuzuia zoezi hilo, wakubali kwenda kupimwa kwani ndio itakuwa kusafishwa kwao kama majibu yatatoka kuwa hawatumii,” alisema Mrema.

Akizungumzia kauli hiyo, Lissu alisema Mrema anapaswa kujiuzulu cheo alichopewa cha Mwenyekiti wa Parole kwa sababu alipewa kinyume cha sheria.

Alisema sheria ipo wazi kwamba Mwenyekiti wa Parole awe jaji au alishawahi kuwa jaji na si mwanasiasa kama Mrema.

“Ninapoona Mrema anapiga kelele, anatetea chakula chake na si vinginevyo, kisheria Mwenyekiti wa Palore anapaswa kuwa jaji au alishawahi kuwa jaji,”alisema Lissu.

Aidha kuhusu kuwatetea watuhumiwa, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, alisema sheria ipo wazi kwamba Wanachofanya mawakili kwa sasa ni kuwatetea watuhumiwa wote hata wanaotuhumiwa na dawa za kulevya, kwani sheria inamtaka wakili kutetea yeyote bila ubaguzi.


Chanzo: Muungwana
Tatizo linaanzia kwa mwenye nyumba kwa kuwa anateua tu bila kuzingatia matakwa ya kisheria katika nafasi za uteuzi na mifano ya mikoroganyo hii ipo wazi mojawapo ni ile nafasi ya kuteua wabunge kumi.
 
Mrema anatatizo la kupungukiwa sukari mwilini kwa hiyo Magufuli kamuwekea sukari mezani hili awe analambalamba.
 
Back
Top Bottom