Lissu: Mwenyekiti wa Parole alipaswa awe Jaji au aliwahi kuwa jaji

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
MWENYEKITI wa Parole, Augustino Mrema amemshukia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), kuwa anafanya makosa makubwa kutetea watuhumiwa wa dawa za kulevya.

Akizunguma na MTANZANIA kwa simu jana, Mrema alisema anamshangaa Lissu kuwatetea watu wanaojihusisha na dawa za kulevya na kumshauri atumie elimu yake ya sheria kuwatetea waathirika na wanaotaja wahusika wa dawa za kulevya akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mbali na Lissu, Mrema aliigeukia mahakama itambue kuwa pamoja na kutafsiri sheria, jukumu la kuzuia dawa za kulevya lipo mikononi mwao.

“Nashangazwa na hawa wanaotuhumiwa kukataa kwenda kupimwa na kuonyesha juhudi za kuzuia zoezi hilo, wakubali kwenda kupimwa kwani ndio itakuwa kusafishwa kwao kama majibu yatatoka kuwa hawatumii,” alisema Mrema.

Akizungumzia kauli hiyo, Lissu alisema Mrema anapaswa kujiuzulu cheo alichopewa cha Mwenyekiti wa Parole kwa sababu alipewa kinyume cha sheria.

Alisema sheria ipo wazi kwamba Mwenyekiti wa Parole awe jaji au alishawahi kuwa jaji na si mwanasiasa kama Mrema.

“Ninapoona Mrema anapiga kelele, anatetea chakula chake na si vinginevyo, kisheria Mwenyekiti wa Palore anapaswa kuwa jaji au alishawahi kuwa jaji,”alisema Lissu.

Aidha kuhusu kuwatetea watuhumiwa, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, alisema sheria ipo wazi kwamba Wanachofanya mawakili kwa sasa ni kuwatetea watuhumiwa wote hata wanaotuhumiwa na dawa za kulevya, kwani sheria inamtaka wakili kutetea yeyote bila ubaguzi.


Chanzo: Muungwana

Kwa mujibu wa sheria namba 25 ya 1994 iliyotiwa sahihi na Rais tarehe 17 Januari 1995, sehemu ya pili ukurasa 236 kifungu cha 2(a) kinataja uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa.

"The National Parole Board shall consist of the Chairman who shall be a person vested with knowledge and xperience in legal matters or in administration of criminal justice, and who shall be appointed by the President".

Tafsiri:

Bodi ya Kitaifa ya Parole itajumuisha na Mwenyekiti ambaye atakuwa mtu mwenye ujuzi na uzoefu wa masuala ya kisheria au usimamiaji wa masuala ya jinai na atateuliwa na Rais.

Kifungu cha 3(a) kinazungumzia teuzi za Wenyeviti wa Bodi za Mikoa:

The Regional Parole Board shall consist of the Chairman who shall be appointed by the Minister and who is vested with knowledge and experience in legal matters or in administration or criminal justice.

Tafsiri:

Bodi ya Parole ya Mkoa itajumuisha na Mwenyekiti ambaye atateuliwa na Waziri na ambaye atakuwa mtu mwenye ujuzi na uzoefu wa masuala ya kisheria au usimamiaji wa masuala ya jinai.
 
Mrema njaa itamuua..Angejikalia zake kimya tu otherwise mkate aliopewa atanyang'anywa aanze kulialia. Rais kamuonea huruma kumpa hiko cheo baada yakukosa ubunge halafu analeta za kuleta hapa. Kila mtuhumiwa ana haki ya kutetewa na mwanasheria,Lisu kumtetea wema kuna shida gani? Muacheni mtu afanye kazi yake. Tatizo uoga unawasumbua sababu ya record nzuri ya Lisu kusinda kesi
 
duuuh kumbe mrema yupo kimakosa pale ila awamu hii mtukuuuuuuuuuuuf hakosei kwaiyo kapatia kabisa
pia mbinu mnayotumia chadema ya kuwatetea watu ili wajiunge na chama chenu ni nzuri aisee iyo nizaid ya kampen na mikutano ya wazi
hahahaaaaaa zaid ya kuita press conference .....Mungu namwomba anipe tu uzima jaman 2020 tutajionea mapya walah
 
Lisu......ukiwa Mbeya hilo jina linamaanisha NYASI. Hata ndani kwako kama hujasiliba na kufanya usafi...Lisu zinaota tu!!!
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom