Lissu: Muungano wa Tanzania (Zanzibar na Tanganyika) ni propaganda za watawala Nyerere alitaka Serikali moja wakati Karume alitaka Tatu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Na, Wakili wa Mahakama Kuu Msomi, Tundu A. Lissu.

Nimefadhaishwa kidogo na baadhi ya michango ya humu ndani kuhusu masuala mbali mbali yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Inaelekea tuna tatizo kubwa sana la uelewa wa historia yetu ya kisiasa na kikatiba. Kinachofundishwa kwa watoto wetu mashuleni kama 'historia' au 'civics' ni propaganda za kisiasa, if not outright fabrications.

Matokeo yake ni kwamba wengi wetu hatujielewi hata hapa tulipo, na tumefikaje hapa tulipo.

Kwa sababu hiyo, nawaombeni radhi kwa kuwachosha na hiki nitakachoandika kuhusu 'Nchi yetu.'

Muungano wetu umeundwa kwa mfano wa Muungano wa Falme ya Britannia Kuu (ile inayoitwa kimakosa 'Uingereza'), kwa kifupi UK.

Sheria ya Mapatano ya Muungano Kati ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ya tarehe 22 Aprili, '64, ilikopiwa moja kwa moja kutoka kwenye Sheria ya Mapatano ya Muungano Kati ya Uingereza na Scotland ya 1703.

Hii ni kwa sababu mtunzi wa Sheria hiyo alikuwa Mwingereza Roland Brown, aliyekuwa Solicitor General wa Tanganyika mara baada ya Uhuru, na wakati wa Muungano. Brown alitumia mfano wa nchi yake mwenyewe katika kutengeneza Muungano wetu.

Muungano wa aina hii hauui nchi washirika wake. Ni Muungano katika baadhi ya mambo tu. UK inaundwa na nchi nne (Uingereza, Scotland, Wales na Ireland ya Kaskazini) ambazo zimeendelea kuwepo zikiwa na mamlaka kamili katika mambo fulani fulani.

Ndivyo ilivyo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Zanzibar ina mamlaka kamili katika mambo yote yasiyokuwa ya Muungano ya Zanzibar.

Kwa upande mwingine, Serikali ya Jamhuri ya Muungano ina mamlaka kamili katika mambo yote ya Muungano; na pia kwa mambo yote yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika.

Hapa ndipo lilipo tatizo la msingi la Muungano wetu, na chanzo kikuu cha ugomvi wetu na Wazanzibari. Na ndipo palipojaa propaganda za kisiasa.

Wanaosema Tanganyika 'ilipotea' kwa sababu ya Muungano hawako sahihi. Tanzania ndio Tanganyika. Kinachoitwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiuhalisia ni Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika iliyonyakua madaraka ya Zanzibar katika yale yanayoitwa 'Mambo ya Muungano.'

Siku Muungano huu unazaliwa, yaani tarehe 26 Aprili, '64, Mwalimu Nyerere alitunga sheria mbili kwa amri ya Rais (decree).

Sheria moja iliekeza kwamba watumishi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika, kuanzia siku hiyo watahesabika kuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Aidha, Mahakama Kuu ya Tanganyika itakuwa ndio Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano. Vile vile, kila mahali katika kila jambo na katika kila sheria za nchi panapotamkwa neno 'Tanganyika', patatamkwa maneno 'Jamhuri ya Muungano.'

Sheria ya pili ilielekeza kwamba Nembo za Taifa la Tanganyika, yaani 'Bibi na Bwana' na Bendera ya Taifa la Tanganyika, zitakuwa ndio Nembo za Taifa za Jamhuri ya Muungano.

Baadae kidogo Mwalimu Nyerere alitunga sheria nyingine iliyoigeuza Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika kuwa ndio Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuhusiana na mambo ya Muungano.

Kwa hiyo, tangu siku ya kwanza kabisa ya Muungano, Tanganyika ilivaa koti la Tanzania. Haijawahi kulivua tangu wakati huo.

Tatizo hili la Muungano lilitokana na uelewa tofauti wa aina ya Muungano wenyewe,kati ya waasisi wake, yaani Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume.

Kwa Mwalimu, Muungano huu ulikuwa njia ya muda tu ya kuelekea Serikali moja, i.e. Serikali ya Tanganyika iliyojifunika koti la 'Tanzania.'

Kwa Sheikh Karume, Muungano huu ulikuwa ni njia ya muda tu ya kuelekea Serikali tatu, yaani Serikali ya Muungano, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mwalimu Nyerere na 'sisi' Watanganyika tumekuwa na agenda ya kuimeza Zanzibar tangu mwanzoni kabisa.

Kuna ushahidi mkubwa wa nyaraka unaoonyesha kwamba Mwalimu Nyerere alimlazimisha Sheikh Karume kuwa na Muungano. Kumbuka Jeshi la Tanganyika lilipelekwa Zanzibar siku tatu tu baada ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mara baada ya Muungano, Mwalimu Nyerere na watu wake walianza kazi ya kuimeza Zanzibar, kwa kutumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Mifano ifuatayo inathibitisha kauli yangu.

Kwanza, muundo wa Serikali mbili, uliokuwa ni temporary arrangement tu kwa mujibu wa Mapatano ya Muungano, ukafanywa ndio muundo wa kudumu chini ya Katiba ya Mpito ya mwaka '65, na baadae Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka '77 iliyopo sasa.

Pili, kuanzia mwaka '64 hadi '77, Katiba yetu iliendelea kutumia jina la 'Tanganyika' katika vifungu vyake kadhaa.

'Tanzania Bara' ilizaliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka '77. Katiba hii iliua pia jina la 'Zanzibar' na badala yake ikazaliwa 'Tanzania Visiwani.'

Tatu, mabadiliko ya orodha ya Mambo ya Muungano. Hati ya Mapatano ya Muungano ya mwaka '64 ilikuwa na mambo 9 tu ya Muungano. Sasa orodha ya Mambo ya Muungano kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano ina mambo 22.

Mwaka '83, NEC ya CCM ilisema kwamba lengo la kuwa na orodha ya Mambo ya Muungano lilikuwa na kufafanua masuala yaliyoko chini ya mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo yatahamishiwa kwenye mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, i.e. Serikali ya Tanganyika.

Nne, kufuatia mgogoro mkubwa wa Muungano wa mwaka '83/'84, uliopelekea 'kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa'; na kungolewa madarakani kwa Rais wa Zanzibar, Alhaj Aboud Jumbe, mambo mawili yalitokea kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Moja, 'Tanzania Visiwani' iliuawa, na 'Tanzania Zanzibar' ikazaliwa. Hivyo, maneno 'Tanzania Zanzibar' yaliyopo kwenye Katiba ya sasa ni ya mwaka '84.

Mbili, maneno ya ibara ya 1 ya Katiba ya sasa kwamba 'Tanzania ni nchi moja...' yaliingizwa. Maneno haya hayakuwepo tangu mwanzo wa Muungano huu, yaliingizwa mwaka '84, miaka 20 baada ya Muungano kuzaliwa.

Wazanzibari hawajawahi kukubali kupoteza nchi yao. Mifano ya kuthibitisha kauli hii ni mingi sana. Nitataja baadhi tu.

Moja, Zanzibar haikuwahi kutunga sheria ya kuridhia Mapatano ya Muungano, kama ilivyokuwa inatakiwa na Hati ya Mapatano ya Muungano.

Mbili, mgogoro juu ya kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania mwaka '66/67. Karume na Wazanzibari walitaka kuwa na Benki Kuu yao wenyewe, ili wawe na uhuru katika masuala ya fedha na uchumi. Badala ya Benki Kuu, waliishia kupata Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), benki ya kibiashara.

Tatu, kwa sababu ya kuongezwa kinyemela kwa mambo ya Muungano, kuna ushahidi kwamba Sheikh Karume alikuwa na mpango wa kuvunja Muungano muda mfupi kabla ya kuuawa kwake Aprili 7, '72.

Nne, kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa mwaka '84, na kung'olewa madarakani kwa Aboud Jumbe.

Kwa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wake, Bashir Ebassuah Kwaw Swanzy, Jumbe alipanga kuitisha Mahakama Maalum ya Jamhuri ya Muungano ili kupata ufumbuzi wa 'Kero za Muungano.'

Mwalimu Nyerere, kwa kutumia majasusi wake alimuwahi, na baadae akamlazimisha kujiuzulu. Aidha, Mwanasheria Mkuu Kwaw Swanzy, raia wa Ghana, alifukuzwa nchini; na Waziri Kiongozi Ramadhani Haji Faki alifukuzwa kazi.

Vile vile, Wazanzibari wengi, akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ya wakati wa Muungano, Wolfgang Dourado, waliwekwa kizuizini.

Tano, Katiba ya sasa ya Zanzibar ni 'Katiba ya Uhuru ya Zanzibar.' Maneno 'Zanzibar ni Nchi'; kutakuwa na 'Mzanzibari'; Rais wa Zanzibar ni 'Mkuu wa Nchi ya Zanzibar'; Rais wa Zanzibar ni 'Kamanda Mkuu wa vikosi Maalum vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar', n.k., ambayo yametapakaa katika Katiba hiyo ni uthibitisho kwamba Wazanzibari wanataka uhuru wao.

Sita, mjadala wa Katiba Mpya wa mwaka '11-'15 na mapendekezo ya Tume ya Warioba ni uthibitisho mwingine tosha kwamba Wazanzibari wanataka uhuru wao.

Sisi Watanganyika, kwa sababu ndio 'wafaidikaji' wakubwa wa Muungano huu, mara nyingi tumeshindwa kuelewa kilio hiki cha Wazanzibari na kukiunga mkono.

Kama ilivyo kawaida ya watu wanaotawala watu wa mataifa mengine, kumekuwa na fikra potofu kwamba, actually, tunawasaidia Wazanzibari, badala ya kuwakandamiza kisiasa na kuwanyonya kiuchumi.

Tunajiona 'tumepoteza' Tanganyika yetu, wakati ukweli ni kwamba tumeinyakua Zanzibar na tunaikalia kinyume na matakwa ya Wazanzibari walio wengi.

Kama sehemu ya mabadiliko makubwa ya kisiasa na kiuchumi yanayohitajika Tanzania, suala la Muungano na Utaifa wa Zanzibar ni la umuhimu wa kipekee.

Ili kulitatua kwa njia ya maridhiano, sisi Watanganyika tunao wajibu mkubwa. Wajibu wetu wa kwanza ni kuifahamu historia yetu halisi, ili kuuelewa Muungano huu na kero zake na kuzitafutia dawa muafaka.

Tundu AM Lissu, MB.
Tienen, Belgium.
27 Aprili, 2019.
 
Niiwahi sema humu kuwa,wengi tumesoma historia kama hadithi tu, ila Lissu mbali na kuisoma,pia anaitumia historia kama kioo cha maisha yake.

Hakika sikukosea.

Na historia ni moja ya vitu vinavyomfanya Lissu kuwa na maono kwani katika hii dunia, mambo mengi yanajirudia tu na kwamba hakuna jipya(Binafsi huwa naamini kujua Historia ni chanzo cha maono).

 
Sielewi kwanini Lissu akiandika nasoma hadi nukta.... sijui..
BTW Swala la Muungano ni very complicated...

Ni kweli wanaitaka nchi yao .. lakini jamii ipi kubwa itaingia matatani endapo Zanzibar utakuwa nchi huru?
Kwanini tu risk amani yetu kama tunaweza kuilinda?
Some facts are classified.... Nadhani bora tunganganie na ikiwezekana tui absorb completely iwe nchi moja tu....
Zanzibar iwe Kama Lindi Au Tanga... administrative support costs za kuiendesha zimekuwa kubwa mno kuliko uwezo wetu kama nchi.....
Imagine hela yote inayoenda kwenye mifuko ya wanasiasa uchwara Zanzibar ingeelekezwa kwenye Afya au Elim. ..

Nilishangaa kidogo katiba ya Warioba kutaka Serikali tatu, yes ni maoni lakini hapa kuna issue kubwa za usalama na maslahi yetu kama nchi...
3 governments for what. .. nchi yenye less than 2M people tuwaundie na bunge Lao kabisa tena na Serikali kamili... hel no.. it was a mistake and hope it will never repeat again .....

Zanzibar imefanana sana kimtizamo na Somalia, Eritrea na Djibouti. .....
Kuipa mamlaka kamili kutaitesa sana Tanganyika kama ilivo kwa Mexico na USA.....
See Drug lords wengi wa natoka Zanzibar. .. imagine iwe nchi huru....
Ingawaje CCM wanainjoy hiyo opportunity , with all the due respect Mr. LISSU.. NO, I'm not for Free Zanzibar whatsoever.
Hata USA sio Majimbo yote yanapenda kuongozwa kutoka Washington DC. .
 
Kamanda kama kawaida yake!

Nondo zimeenda shule!
kuhusu hoja kuwa Mwl alitaka serikali 1 na Karume alitaka serikali 3
The role of pen,,nmekuelewa sana TL
kuhusu hoja kuwa Mwl alitaka serikali 1 na Karume alitaka serikali 3 Lisu amejuaje maana yeye anaongea kama vile yeye Lisu alishiriki kwenye hayo mazunguzo hayo
 
Back
Top Bottom