Lissu: Magufuli anatulisha matango pori, toka mwaka 1999 alikuwa anaunga mkono uuzwaji wa migodi, hicho kishika uchumba Accacia wako mahakamani

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Anaandika #Tundu_Lissu

21.02.2019

'Nateseka' na hili suala kwa sababu 'nimeteseka' nalo toka mwaka 1999, wakati Magufuli 'akiunga mkono' juhudi za Rais Mkapa za kuuza utajiri wetu kwa wageni. Huu ni mwaka wangu wa 20 'nateseka' nalo na nitaendelea kuteseka nalo as long as nina pumzi.

Mnadanganywa na tunadanganywa na Magufuli na watu wake. Alipokuja President John Thornton mwaka jana, tuliambiwa Barrick watalipa 'kishika uchumba' (á la Prof. Kabudi) cha dola 300m.

Hawakulipa. Kwa nini??? Kwa sababu Acacia Mining walikataa. Badala yake walitufungulia kesi ya kuvunja mikataba yao ICSID, wanakotudai mabilioni ya dola.

Sasa amekuja President Willem Jacobs. Naye amesema Barrick watalipa 'kifuta machozi' cha dola 300m, lakini mpaka kwanza 'independent board of directors' ya Acacia Mining wakubali. Hao hao waliokataa kulipa mwaka jana wanatakiwa wakubali kulipa sasa.

Halafu kwenye press release yao iliyotolewa jana hiyo hiyo, Barrick wanasema ahadi zao hizo kwa Magufuli ni 'forward looking statements' ambazo, kwa kifupi, sio makubaliano yoyote yenye nguvu za kisheria. Hawafungwi na chochote walichokisema kwenye makubaliano yao na Serikali ya Tanzania.

Ndio maana nimesema someni hiyo disclaimer vizuri. Wazungu hawa sio wajinga. Wanasema hizo 'forward looking statements' zao zinaweza kuathiriwa na kesi au mashauri yanayoendelea mahakamani. Maana yake ni nini??? Wakitushinda kwenye kesi waliyotufungulia ICSID hawatatulipa.

Wanasema hizo 'forward looking statements' zao zinaweza kuathiriwa na faida au hasara katika uwekezaji wao. Maana yake ni nini??? Wakipata hasara hawatatulipa.

Sheria ya sasa ya Madini inasema mkataba wowote unaohusu madini unatakiwa kuwasilishwa Bungeni. Kama hawatulishi matango pori watayawasilisha makubaliano haya bungeni. Wasipoyawasilisha ujue ni matango pori.
 
Kuna watu wanajua wanadanganywa ila hawana la kufanya zaidi ya kumsadia kudanganya

Jiwe yupo point of no return maana akirudi kuyafanyia kazi maneno ya Lissu basi itakua kakubali Lissu hakua mpotoshaji bali yeye
 
Mzee Meko anataka kuongeza muda wa kukaa madarakani ila kwa vile hana ABC za kucheza hii michezo angejiuzulu tuu maana kila siku iendayo kwa Mungu Mambo yanazidi kuwa Mambo.

Yaani Kama ningekutana naye ningemwambia hakuna mtu anayetoa hela yake aliyoitolea jasho aidha kwa wizi au kwa kutapeli. Kama ana mawazo hayo basi nimpe pole tena pole Sana hakuba mjinga kiasi hicho.

Acha achezewe tuuu maana hasikiagi la mtu mpaka abaki mwenyewe ndo atajua kwamba Hawa jamaa ni akili nyingine na sio hizo propaganda zake za kitoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salaam,
Nakutakia afya njema na nakuombe upone katika operesheni yako ya 23.

Masuala ya JPM Barrick, Accacia mwachie Mwenyewe, aliyeyaanzisha ndiye atakayeyamaliza, kama wewe unaendelea na ya kwako endelea!! Hujalazimishwa kulalamikia mambo yanayofanywa na mtu mwingine.

Yeye anafanya katika kile ambacho anaona sawa, kwa maana nyingine siyo lazima atumie ushauri wako katika kushughulikia mambo hayo. Umekuwa na tabia ya kuingilia namna Rais anavyofanya kazi zake sio sawa, mwache ashindwe au aweze mwenyewe, kama yeye amehakikishiwa watalipa basi subiri uone nini kitatokea, acha maneno maneno yako.
 
Ubarikiwe na upone haraka lissu hakika ww , zitto na wapambanaji wengine mnafanya jiwe na vuvuzela wake kabudi wasiwe na Amani na uwongo wao
nakwambia Lissu ni mgonjwa na akiongea utando mweupe waanzaa kutoka mashavuni kupitia mdomo huku akiomba msaada wa kusomesha wanaye
 
Back
Top Bottom