Lissu lipotezee bunge la Tulia komaa na kazi ya uwakili

Stabilaiza

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
1,843
1,143
Nchi yetu iko katika hali ngumu katika awamu hii ikiwemo watawala kuonea wananchi bila hata aibu. Uonevu wa watawala hawa umekomaa kiasi kwamba hawaoni tabu kuvunja sheria ili kutimiza malengo yao ya binafsi. Sasa hivi kuna wimbi la wananchi kufungwa na kuswekwa rumande kwa uonevu. Kuna watu wako ndani kwa kunyimwa dhamana kwa kutuhumiwa na makosa ambayo yanasitahili kupata ndamana.

Bunge nalo kwa sasa limechuja mno. Wananchi hatuoni live wawakilishi wetu wakiwa kazini huko mjengoni. Kibaya zaidi kuna-monitor imewekwa hapo mjengoni wakati remote yake inawashwa na kuzimiwa maeneo ya magogoni. Hivyo kazi ya bunge imekuwa ni kufanya matakwa ya mwenye kushikilia remote. Bunge si sehemu tena ya kusimamia maslahi ya wananchi bali watawala. Hivyo, machango wa mh. Lissu katika kutengeneza sheria, kusimamia na kuiwajibisha serikali unakwamishwa na monitor iliyopachikwa mjengoni.

Wito wangu kwa Lissu ni kulipotezea bunge katika awamu hii na kujikita kuwatetea wananchi wanaoonewa bila sababu na watawala wenye matakwa binafsi. Juhudi za Mh. Lissu katika kutetea utawala wa sheria na kuzuia kukandamizwa kwa wananchi zinaonekana. Lakini Lissu atatoa mchango mkubwa zaidi katika utawala huu akifanya zaidi kazi ya uwakili ili kuwaokoa wanaoonewa na kuozea magerezani. Katika kazi hii ya uwakili, Lissu aunde timu- yaani timu Lissu kwa ajili hiyo. Tundu Lissu aende bungeni pale tu panapokuwa na jambo nyeti linalohitaji ujuzi na ufahamu maalamu wa Lissu. Vinginevyo, Tundu Lissu jikite katika uwakili na kukaa na wananchi wa jimboni kwako kuliko kupoteza muda katika Bunge la Tulia huku wananchi wanaoonewa katika utawala huu wakizidi kuongezeka.
 
Kuzuia bunge laivu mitandao inapata pesa bajameni watu wananunua bundle kwa fujo ili wa download.. kufa kufaana.
 
Kuzuia bunge laivu mitandao inapata pesa bajameni watu wananunua bundle kwa fujo ili wa download.. kufa kufaana.
Wabunge ni wawakilishi wa wananchi, Hivyo bunge laivu kwenye Tv linaangaliwa na wananchi wengi kuliko wale wenye kuwezo wa ku-download clip kwenye computer na simu.
 
Tundu anafaa kote
Ni sawa, lakini kwa sasa hatumiki vizuri bungeni sababu ya monitor iliyosimikwa mjengoni. Akijikita kwenye uwakili atakomboa watu wengi wanaoonewa. Pia kulipotezee bunge la sasa Lissu atapata muda wa kutoka kuzungumza na wananchi katika jimbo lao.
 
Back
Top Bottom