chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,383
- 24,939
Akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho na Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Mhe.
Tundu Lissu amesema timu ya wanasheria wa chama hicho wameanza taratibu za kukata rufaa, kwa kuandaa notisi ya rufaa na maombi ya dhamana ya dharura wakati uamuzi juu ya rufaa yake ukisubiriwa ili Mhe.
Lijualikali aweze kupata dhamana huku wakiendelea na kesi hiyo.
Aidha, Mhe. Lissu amesema, hukumu hiyo kwa Mhe. Peter Lijualikali haina athari zozote kwa hadhi yake kama mbunge wa jimbo la Kilombero kwani Katiba imeeleza wazi juu ya makosa yanayoondoa sifa za kuwa mbunge na kwamba adhabu ya kifungo alichopewa haijazidi miezi 6 na kosa alilohukumiwa siyo kosa la kugushi, ubadhirifu ama makosa mengine yanayoambatana na utovu wa uaminifu.
Chanzo : EATV