Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,068
- 10,954
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amejitosa kuzungumzia sakata la barua ya malalamiko kuhusu uteuzi alioufanya wa viongozi watendaji wa juu na wajumbe wa kamati kuu akisema haina mashiko yoyote.Barua hiyo ni ya kada wake, Lembrus Mchome, aliyoiandika kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chadema na nakala kuituma Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa anapinga uteuzi wa viongozi hao uliofanywa na Lissu, Januari 22, 2025, akidai umekiuka katiba ya chama hicho.
Mchome, ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro, amesema uteuzi wa vigogo hao uliidhinishwa bila akidi ya kikao cha baraza kuu kutimia.
Leo Jumapili, Februari 23, 2025, Lissu amefanya mahojiano maalumu na Mwananchi nyumbani kwake, Tegeta jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine ameulizwa swali juu ya barua hiyo na tahadhari zinazotolewa wasije kuingia kwenye mgogoro kama ulivyoshuhudiwa kwa vyama vingine.
Lissu amesema anajua anachokifanya kada huyo ni kuwapotezea muda au hajui vizuri Katiba ya chama hicho kwani wana orodha yote ya wajumbe wa Baraza Kuu lililokutana Januari 22, 2025 katika ukumbi wa Mlimani City.
Pia soma
- Pre GE2025 - Team Mbowe wajidhatiti kumkwamisha LISSU, wapinga uteuzi wa Wajumbe watano wa kamati kuu aloufanya Lissu, waandika Barua kwa msajili wa Vyama
- Pre GE2025 - Barua ya malalamiko kuhusu Uteuzi wa viongozi watendaji na wajumbe wa kamati kuu CHADEMA imewafikia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
- Pre GE2025 - John Mnyika adai kuna hujuma za kuyumbisha harakati za 'No Reforms No Election' kufuatia pingamizi la uteuzi wa vigogo nane CHADEMA