Lissu: Kumkamata Harbinder Sethi na James Rugemalira ni sawa lakini haitoshi

KUMKAMATA HARBINDER SINGH NA JAMES RUGEMALILA NI SAWA LAKINI HAITOSHI!!!!

Na Tundu Lissu

Harbinder Singh Seth na James Rugemalila walikuwa ni sehemu muhimu ya mtandao uliokwapua shilingi bilioni 306 zilizokuwa Benki Kuu.

Ni sawa, kwa hiyo, wakifunguliwa mashtaka ya jinai ya uhujumu uchumi.

Hata hivyo, tusije kusahau kwamba walikuwa ni sehemu tu ya mtandao wa ufisadi. Vipande vingine vya chain hiyo viko wapi???

Ili bilioni 306 zitoke Benki Kuu ilikuwa lazima Gavana wa BoT Prof. Benno Ndullu na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Paymaster General, Dr. Servacius Likwelile watoe ridhaa yao.

Gavana Ndullu bado yuko ofisini kama Gavana. Dr. Likwelile ametumbuliwa ili kumpisha mpwa wa Bwana Mkubwa kuwa Katibu Mkuu na Paymaster General.

Ili bilioni 306 zitoke BoT ilikuwa lazima Waziri wa Fedha Saada Mkuya ajue na aridhie. Vinginevyo alikuwa ni Waziri wa Fedha wa aina gani asiyejua jambo kubwa kama hilo ndani ya Wizara yake.

Saada Mkuya sio Waziri wa Fedha tena lakini bado ni mbunge na yuko huru hadi sasa.

Ili bilioni 306 za umma zitoke ilikuwa lazima Rais Jakaya Kikwete afahamu na atoe ridhaa yake.

In fact, ripoti ya Kamati ya PAC ilionyesha ushahidi kwamba Prosper Mbena, wakati huo Msaidizi wa Rais Kikwete na sasa mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, aliandika dokezo kwa Gavana Ndullu kwamba Rais ameridhia mabilioni hayo yatoke.

Prosper Mbena sasa ni mheshimiwa mbunge na Kikwete ni mzee ambaye tumeambiwa tusimzungumzie bungeni wala magazetini, tumwache apumzike.

Nje ya hawa niliowataja, wapo wale waliopokea mgawo wa mapato ya udhalimu wa mabilioni hayo.

Wapo waliothibitika kuchukua tuhela twa mboga kama Prof. Anna Tibaijuka na Andrew Chenge (bilioni 1.6 kila mmoja); majaji wa Escrow, watumishi wa serikali na hata wa Ikulu ya Kikwete kama Shabani Gurumo, mapadre na maaskofu, n.k.

Wote hawa ni wahalifu kwa mujibu wa sheria za jinai za nchi hii. Karibu wote bado wako huru na wengine, kama Chenge, wamepanda vyeo na kuwa Mwenyekiti wa Bunge.

Pia kuna taasisi inayoitwa Simba Trust ambayo PAC ilisema inamiliki 50% ya IPTL. Serikali ya Kikwete ilikataa katakata kusema hawa Simba Trust ni akina nani.

Mpaka sasa serikali ya Rais Magufuli haijasema Simba Trust ni akina nani ili tuweze kujua nusu ya mgawo wa Tegeta Escrow ulichukuliwa na nani.

Kwa sababu zote hizi, nadhani ni mapema sana kuanza kumshangilia Magufuli kwa ajili ya Harbinder Singh Seth na James Rugemalila kushtakiwa mahakamani leo.

Badala ya kushangilia, tunapaswa kumuuliza Rais Magufuli kwa nini amekamata wafanya biashara waliochotewa mabilioni ya Tegeta Escrow lakini ameacha mawaziri na maafisa wa serikali walioruhusu uchotwaji wa fedha hizo, au wote waliopata mgawo wa fedha hizo.

Tunapaswa tumhoji kwa nini anaelekea kukwepa watu fulani fulani lakini wengine anawakaba koo? ??

Tumwambie kwamba katika sheria za haki za binadamu za kimataifa, mahakama za kimataifa zimesema kwamba, kama ambavyo marais hawana kinga kwa makosa dhidi ya ubinadamu au uhalifu wa kivita, marais pia hawana kinga dhidi ya mashtaka kwa uhalifu wa kiuchumi dhidi ya nchi zao.

Magufuli hastahili kupewa hata benefit of the doubt.

Kumbukeni ya Kikwete na mashtaka ya hujuma ya uchumi dhidi ya Prof. Mahalu na akina Mramba na Daniel Yona.

Kikwete huyo huyo ndiye baadae alimteua Prof. Mahalu kwenye Bunge la Katiba.

Na Magufuli ndiye aliyemrudisha Prof. Muhongo wizarani baada ya Bunge kumlazimisha Kikwete kumfukuza kazi kutokana na kashfa ya Tegeta Escrow.

We'd not allow ourselves to be taken in and/or fooled by these gimmicks again.

Usiku mwema.
Excellent
 
upumzikage tu huko huko lissu,ukirudi huku wanakumalizia,,kwanza unarudi kutafuta nn tena?..ubunge hawakupi tena,uraisi hauwezi tena kugombea maana sheria imebadilishwa na hata ukigombea haupati kwa chaguzi zetu hizi,,ss si bora ukaombe kazi huko hata ya kuwa mhudumu wa mahakama
 
Tundu Lissu is a genius. Great thinker. Watu wawili hawawezi hujumu uchumi kwa kiasi hichi bila msaada wa maafisa kutoka Serikalini. Wote waliohusika wakamatwe na kufunguliwa mashtaka - uchunguzi wa kina ulishafanyika.
 
Mimi kwa upande wangu ningewashauri wahusika wasadie upelelezi ukamilike mapema kuliko wao pekee kuendelea kusota rumande huku washirika wengine wakila bata mtaani
 
Kuna watu walimbeza Lissu leo yakwapi?? Mlishangilia weee ila pesa zimeliwa na hakuna aliyekutwa na hatia more so kina chenge na Muhongo wapo mtaani wanadunda tu bila hta maigizo ya kupelekwa mahakamani. Then kuna mtu anasema eti tuna mahakama ya mafisadi??

Kiufupi ukurasa wa ESCROW umefungwa rasmi leo baada ya waliotolewa kafara kuachiwa. Na waliohusika wapo serikalini wametulia tu wanakula mzigo waliogawana pale Stanbic bank.
 
Back
Top Bottom