Lissu: Kumkamata Harbinder Sethi na James Rugemalira ni sawa lakini haitoshi

Matamshi ya Lissu huwa yana ukakasi sana. Hivi aliyemuambia inatosha nani? Unajua mtu mzima unapo bwata bwata hovyo haipendezi.Binafsi ningependa JPM apewee nafasi.Vineno vineno vya namna hii visivyo na tija vinam- demoralize.Let us give him time,it's too early.
 
Embu kuwa serious mkuu yye kasema ana kinga ya kukamatwa ila sio kinga ya kuhojiwa??? Sasa dhambi kwa mkuu wa nchi kuhojiwa kwamba ilikuwaje ikulu ikaidhinisha pesa za kifisadi ambazo hata katibu wake bwana gurumo alikuwa mnufaika??? Mbona mkapa alienda kuhojiwa kuhusu balozi mahalu??? Acheni utoto nyie kikwete sio malaila afterall IPTL iliingia nchini yye akiwa waziri wa kawaida tu ssa hyo kinga ni mpaka kwa uwaziri wake?? Kwani inakataza asihojiwe na kueleza mafisadi wote wakwapi wakamatwe???

Acheni kulindana ili haki itendeke
sentensi yako ya mwisho imefanya utetezi wako usiwe na maana,namlinda nani..kikwete!?,umekataa nini umekubali nini?
 
Mchana kuna mtu nilikuwa nadiscuss nae,akaniambia "Lisu hata hili la kukamatwa hawa atalipinga atasema wengine wako wapi"...huyu Lisu mimi ananishangaza sana kiukweli.kila kitu anakipinga,,,hivi kama kulikuwa na wezi 10 halafu ukakamata wawili bado tu sio hatua hiyo?? Wamekamatwa wale vinara wenyewe wanyonyaji,lakini yeye anataka wakamatwe hadi wale waliochotewa pesa,je waliochotewa wana kosa gani??
Mkuu umesoma alichosema Lisu na ukakielewa? Wapi amepinga alichofanya JPM? Au ameshauri tu nini kifanyike zaidi ya hapo!! Tatizo mnakimbilia kucomment bila kusoma uzi kwanza.
 
Kwani unaharaka gani kazi moja ndio imeanza na wengine watafuata... tuliza kipago hicho...
 
You have the option to either put your brain to work or continue to outsource the thinking function to Lissu at your own risk! Unless and until you allow the power of reason to run the show, please do yourself a favor by steering clear of high-stake debates. Otherwise, you'll keep making arguments that lack substance and are fraught with internal inconsistencies.
Your newfound hero isn't only a lawmaker but also a practicing attorney. Why hasn't he filed a lawsuit against anyone he accuses of having committed economic crimes? Why hasn't he introduced a private bill in the legislature to amend the most deficient laws? ...Just as though legality were equal to morality!

That Lissu has admirers like you ain't surprising at all. ... Remember, even the most dangerous fundamentalists to ever have lived, such as Hitler and Bin Laden, had and continue to have admirers!
It will be too late when you will realise that, it was not a matter of necessity for you to utter this nonsense.

Lisu isn't an attorney from prosecutor's office to be eligible to file a case against the accused persons, or even if he can, but not before he gets consent from the same authority, for which he would have got nothing.

So long as Hitler or Bin laden, had admirers, according to your assertion, there is nothing wrong for Lisu to enjoy this privilege, albeit he comes from different historical background as the former and you will agree with me that what he is fighting for is not the same cause the two fought for.

Lastly, I advise you not to politicize everything that comes across your eyes, as that, can terribly interfere with your reasoning potential as it seems to have been the case in your "poorly conceived article", as you have flatly failed to substantiate Tundu Lisu's hypocrisy, vis a vis, the subject matter.
 
It's sad that you're politicizing this, yet you think you ain't but others are!

I wish I were a 5th grade teacher to help you understand the meaning of the word "hypocrisy". I'd only suggest that you study Lissu's pre-2015 speeches and written positions about Lowasa, Sumaye, and the likes; hopefully, you'll come to your senses when you analyze his post-2015 association, speeches and written positions.

Lissu is a political contrarian that shouldn't waste the precious time of anyone who's willing and able to think for himself or herself. For those of you who have outsourced your thinking function to Lissu, feel free to preserve the status quo!
 
Hapa ndio utashangaa maajabu ya maandishi, tumemsoma wote but mwishoni mwa siku utasikia wengine tuliosoma nao maandishi haya haya wanakuja na kusema, "Lissu anatetea wezi na mafisadi" Dunia ina maajabu hi.
 
hata hamjui mnataka nini
wangekamatwa wengine mngesema wamekamtwa dagaa mapapa yanapeta
sasa wamekamatwa mapapa mnahamisha magoli
 
Matamshi ya Lissu huwa yana ukakasi sana. Hivi aliyemuambia inatosha nani? Unajua mtu mzima unapo bwata bwata hovyo haipendezi.Binafsi ningependa JPM apewee nafasi.Vineno vineno vya namna hii visivyo na tija vinam- demoralize.Let us give him time,it's too early.
Jitahidi kuwa na fikra pana juu ya hiki kinachotokea kuliko kuweka ushabiki wa vyama na chuki kwa mtu hata kama anachozungumza au kuandika kina maana kubwa. Ebu jiulize inakuwaje unawakamata watu waliopokea fedha za wizi na kuwaacha watu walio ruhusu kwa taratibu zote za kiofisi na kutoa fedha hizo? je ni nani aliandika Barua na DOKEZO la kuomba fedha hizo je ni nani alipitisha na kuruhusu fedha hizo zitoke? elewa kuwa katika sakata hili UWT, IKULU na BOT hawachomoki kama kweli kuna nia ya dhati kulishughulikia suala hili la IPTL la sivyo itakuwa IGIZO lisilokwisha kama ISINDINGO THE NEED.
 
KUMKAMATA HARBINDER SINGH NA JAMES RUGEMALILA NI SAWA LAKINI HAITOSHI!!!!

Na Tundu Lissu

Harbinder Singh Seth na James Rugemalila walikuwa ni sehemu muhimu ya mtandao uliokwapua shilingi bilioni 306 zilizokuwa Benki Kuu.

Ni sawa, kwa hiyo, wakifunguliwa mashtaka ya jinai ya uhujumu uchumi.

Hata hivyo, tusije kusahau kwamba walikuwa ni sehemu tu ya mtandao wa ufisadi. Vipande vingine vya chain hiyo viko wapi???

Ili bilioni 306 zitoke Benki Kuu ilikuwa lazima Gavana wa BoT Prof. Benno Ndullu na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Paymaster General, Dr. Servacius Likwelile watoe ridhaa yao.

Gavana Ndullu bado yuko ofisini kama Gavana. Dr. Likwelile ametumbuliwa ili kumpisha mpwa wa Bwana Mkubwa kuwa Katibu Mkuu na Paymaster General.

Ili bilioni 306 zitoke BoT ilikuwa lazima Waziri wa Fedha Saada Mkuya ajue na aridhie. Vinginevyo alikuwa ni Waziri wa Fedha wa aina gani asiyejua jambo kubwa kama hilo ndani ya Wizara yake.

Saada Mkuya sio Waziri wa Fedha tena lakini bado ni mbunge na yuko huru hadi sasa.

Ili bilioni 306 za umma zitoke ilikuwa lazima Rais Jakaya Kikwete afahamu na atoe ridhaa yake.

In fact, ripoti ya Kamati ya PAC ilionyesha ushahidi kwamba Prosper Mbena, wakati huo Msaidizi wa Rais Kikwete na sasa mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, aliandika dokezo kwa Gavana Ndullu kwamba Rais ameridhia mabilioni hayo yatoke.

Prosper Mbena sasa ni mheshimiwa mbunge na Kikwete ni mzee ambaye tumeambiwa tusimzungumzie bungeni wala magazetini, tumwache apumzike.

Nje ya hawa niliowataja, wapo wale waliopokea mgawo wa mapato ya udhalimu wa mabilioni hayo.

Wapo waliothibitika kuchukua tuhela twa mboga kama Prof. Anna Tibaijuka na Andrew Chenge (bilioni 1.6 kila mmoja); majaji wa Escrow, watumishi wa serikali na hata wa Ikulu ya Kikwete kama Shabani Gurumo, mapadre na maaskofu, n.k.

Wote hawa ni wahalifu kwa mujibu wa sheria za jinai za nchi hii. Karibu wote bado wako huru na wengine, kama Chenge, wamepanda vyeo na kuwa Mwenyekiti wa Bunge.

Pia kuna taasisi inayoitwa Simba Trust ambayo PAC ilisema inamiliki 50% ya IPTL. Serikali ya Kikwete ilikataa katakata kusema hawa Simba Trust ni akina nani.

Mpaka sasa serikali ya Rais Magufuli haijasema Simba Trust ni akina nani ili tuweze kujua nusu ya mgawo wa Tegeta Escrow ulichukuliwa na nani.

Kwa sababu zote hizi, nadhani ni mapema sana kuanza kumshangilia Magufuli kwa ajili ya Harbinder Singh Seth na James Rugemalila kushtakiwa mahakamani leo.

Badala ya kushangilia, tunapaswa kumuuliza Rais Magufuli kwa nini amekamata wafanya biashara waliochotewa mabilioni ya Tegeta Escrow lakini ameacha mawaziri na maafisa wa serikali walioruhusu uchotwaji wa fedha hizo, au wote waliopata mgawo wa fedha hizo.

Tunapaswa tumhoji kwa nini anaelekea kukwepa watu fulani fulani lakini wengine anawakaba koo? ??

Tumwambie kwamba katika sheria za haki za binadamu za kimataifa, mahakama za kimataifa zimesema kwamba, kama ambavyo marais hawana kinga kwa makosa dhidi ya ubinadamu au uhalifu wa kivita, marais pia hawana kinga dhidi ya mashtaka kwa uhalifu wa kiuchumi dhidi ya nchi zao.

Magufuli hastahili kupewa hata benefit of the doubt.

Kumbukeni ya Kikwete na mashtaka ya hujuma ya uchumi dhidi ya Prof. Mahalu na akina Mramba na Daniel Yona.

Kikwete huyo huyo ndiye baadae alimteua Prof. Mahalu kwenye Bunge la Katiba.

Na Magufuli ndiye aliyemrudisha Prof. Muhongo wizarani baada ya Bunge kumlazimisha Kikwete kumfukuza kazi kutokana na kashfa ya Tegeta Escrow.

We'd not allow ourselves to be taken in and/or fooled by these gimmicks again.

Usiku mwema.
IMG_20161103_093228.jpg
 
Jitahidi kuwa na fikra pana juu ya hiki kinachotokea kuliko kuweka ushabiki wa vyama na chuki kwa mtu hata kama anachozungumza au kuandika kina maana kubwa. Ebu jiulize inakuwaje unawakamata watu waliopokea fedha za wizi na kuwaacha watu walio ruhusu kwa taratibu zote za kiofisi na kutoa fedha hizo? je ni nani aliandika Barua na DOKEZO la kuomba fedha hizo je ni nani alipitisha na kuruhusu fedha hizo zitoke? elewa kuwa katika sakata hili UWT, IKULU na BOT hawachomoki kama kweli kuna nia ya dhati kulishughulikia suala hili la IPTL la sivyo itakuwa IGIZO lisilokwisha kama ISINDINGO THE NEED.
Ndio maana nimesema tumpe nafasi,after all he has been in office for just a while! Mimi na wewe nadhani hatujui his plan of operations na sio lazima his timing of what he does,ioane na unavyofikiria wewe.

Finally mkuu, there are no political agendas here,it's just reasonable to think that way.
 
Upande uleeee jamaaaa lisu keshawapoteza tayari tulikuwa kwenye makinikia sasa amewapeleka kwa rugemarila na seth duh hadi raha
 
Back
Top Bottom