Lissu: Kumkamata Harbinder Sethi na James Rugemalira ni sawa lakini haitoshi

BAKOI

JF-Expert Member
Jan 31, 2016
1,059
2,000
KUMKAMATA HARBINDER SINGH NA JAMES RUGEMALILA NI SAWA LAKINI HAITOSHI!!!!

Na Tundu Lissu

Harbinder Singh Seth na James Rugemalila walikuwa ni sehemu muhimu ya mtandao uliokwapua shilingi bilioni 306 zilizokuwa Benki Kuu.

Ni sawa, kwa hiyo, wakifunguliwa mashtaka ya jinai ya uhujumu uchumi.

Hata hivyo, tusije kusahau kwamba walikuwa ni sehemu tu ya mtandao wa ufisadi. Vipande vingine vya chain hiyo viko wapi???

Ili bilioni 306 zitoke Benki Kuu ilikuwa lazima Gavana wa BoT Prof. Benno Ndullu na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Paymaster General, Dr. Servacius Likwelile watoe ridhaa yao.

Gavana Ndullu bado yuko ofisini kama Gavana. Dr. Likwelile ametumbuliwa ili kumpisha mpwa wa Bwana Mkubwa kuwa Katibu Mkuu na Paymaster General.

Ili bilioni 306 zitoke BoT ilikuwa lazima Waziri wa Fedha Saada Mkuya ajue na aridhie. Vinginevyo alikuwa ni Waziri wa Fedha wa aina gani asiyejua jambo kubwa kama hilo ndani ya Wizara yake.

Saada Mkuya sio Waziri wa Fedha tena lakini bado ni mbunge na yuko huru hadi sasa.

Ili bilioni 306 za umma zitoke ilikuwa lazima Rais Jakaya Kikwete afahamu na atoe ridhaa yake.

In fact, ripoti ya Kamati ya PAC ilionyesha ushahidi kwamba Prosper Mbena, wakati huo Msaidizi wa Rais Kikwete na sasa mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, aliandika dokezo kwa Gavana Ndullu kwamba Rais ameridhia mabilioni hayo yatoke.

Prosper Mbena sasa ni mheshimiwa mbunge na Kikwete ni mzee ambaye tumeambiwa tusimzungumzie bungeni wala magazetini, tumwache apumzike.

Nje ya hawa niliowataja, wapo wale waliopokea mgawo wa mapato ya udhalimu wa mabilioni hayo.

Wapo waliothibitika kuchukua tuhela twa mboga kama Prof. Anna Tibaijuka na Andrew Chenge (bilioni 1.6 kila mmoja); majaji wa Escrow, watumishi wa serikali na hata wa Ikulu ya Kikwete kama Shabani Gurumo, mapadre na maaskofu, n.k.

Wote hawa ni wahalifu kwa mujibu wa sheria za jinai za nchi hii. Karibu wote bado wako huru na wengine, kama Chenge, wamepanda vyeo na kuwa Mwenyekiti wa Bunge.

Pia kuna taasisi inayoitwa Simba Trust ambayo PAC ilisema inamiliki 50% ya IPTL. Serikali ya Kikwete ilikataa katakata kusema hawa Simba Trust ni akina nani.

Mpaka sasa serikali ya Rais Magufuli haijasema Simba Trust ni akina nani ili tuweze kujua nusu ya mgawo wa Tegeta Escrow ulichukuliwa na nani.

Kwa sababu zote hizi, nadhani ni mapema sana kuanza kumshangilia Magufuli kwa ajili ya Harbinder Singh Seth na James Rugemalila kushtakiwa mahakamani leo.

Badala ya kushangilia, tunapaswa kumuuliza Rais Magufuli kwa nini amekamata wafanya biashara waliochotewa mabilioni ya Tegeta Escrow lakini ameacha mawaziri na maafisa wa serikali walioruhusu uchotwaji wa fedha hizo, au wote waliopata mgawo wa fedha hizo.

Tunapaswa tumhoji kwa nini anaelekea kukwepa watu fulani fulani lakini wengine anawakaba koo? ??

Tumwambie kwamba katika sheria za haki za binadamu za kimataifa, mahakama za kimataifa zimesema kwamba, kama ambavyo marais hawana kinga kwa makosa dhidi ya ubinadamu au uhalifu wa kivita, marais pia hawana kinga dhidi ya mashtaka kwa uhalifu wa kiuchumi dhidi ya nchi zao.

Magufuli hastahili kupewa hata benefit of the doubt.

Kumbukeni ya Kikwete na mashtaka ya hujuma ya uchumi dhidi ya Prof. Mahalu na akina Mramba na Daniel Yona.

Kikwete huyo huyo ndiye baadae alimteua Prof. Mahalu kwenye Bunge la Katiba.

Na Magufuli ndiye aliyemrudisha Prof. Muhongo wizarani baada ya Bunge kumlazimisha Kikwete kumfukuza kazi kutokana na kashfa ya Tegeta Escrow.

We'd not allow ourselves to be taken in and/or fooled by these gimmicks again.

Usiku mwema.
 
Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
18,139
2,000
Na Tundu Lissu

Harbinder Singh Seth na James Rugemalira walikuwa ni sehemu muhimu ya mtandao uliokwapua shilingi bilioni 306 zilizokuwa Benki Kuu.

Ni sawa, kwa hiyo, wakifunguliwa mashtaka ya jinai ya uhujumu uchumi.
Hata hivyo, tusije kusahau kwamba walikuwa ni sehemu tu ya mtandao wa ufisadi. Vipande vingine vya chain hiyo viko wapi???

Ili bilioni 306 zitoke Benki Kuu ilikuwa lazima Gavana wa BoT Prof. Benno Ndullu na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Paymaster General, Dr. Servacius Likwelile watoe ridhaa yao.

Gavana Ndullu bado yuko ofisini kama Gavana. Dr. Likwelile ametumbuliwa ili kumpisha mpwa wa Bwana Mkubwa kuwa Katibu Mkuu na Paymaster General.

Ili bilioni 306 zitoke BoT ilikuwa lazima Waziri wa Fedha Saada Mkuya ajue na aridhie. Vinginevyo alikuwa ni Waziri wa Fedha wa aina gani asiyejua jambo kubwa kama hilo ndani ya Wizara yake.
Saada Mkuya sio Waziri wa Fedha tena lakini bado ni mbunge na yuko huru hadi sasa.

Ili bilioni 306 za umma zitoke ilikuwa lazima Rais Jakaya Kikwete afahamu na atoe ridhaa yake.

In fact, ripoti ya Kamati ya PAC ilionyesha ushahidi kwamba Prosper Mbena, wakati huo Msaidizi wa Rais Kikwete na sasa mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, aliandika dokezo kwa Gavana Ndullu kwamba Rais ameridhia mabilioni hayo yatoke.

Prosper Mbena sasa ni mheshimiwa mbunge na Kikwete ni mzee ambaye tumeambiwa tusimzungumzie bungeni wala magazetini, tumwache apumzike. Nje ya hawa niliowataja, wapo wale waliopokea mgawo wa mapato ya udhalimu wa mabilioni hayo.

Wapo waliothibitika kuchukua tuhela twa mboga kama Prof. Anna Tibaijuka na Andrew Chenge (bilioni 1.6 kila mmoja); majaji wa Escrow, watumishi wa serikali na hata wa Ikulu ya Kikwete kama Shabani Gurumo, mapadre na maaskofu, n.k.

Wote hawa ni wahalifu kwa mujibu wa sheria za jinai za nchi hii. Karibu wote bado wako huru na wengine, kama Chenge, wamepanda vyeo na kuwa Mwenyekiti wa Bunge.
Pia kuna taasisi inayoitwa Simba Trust ambayo PAC ilisema inamiliki 50% ya IPTL.

Serikali ya Kikwete ilikataa katakata kusema hawa Simba Trust ni akina nani.
Mpaka sasa serikali ya Rais Magufuli haijasema Simba Trust ni akina nani ili tuweze kujua nusu ya mgawo wa Tegeta Escrow ulichukuliwa na nani.

Kwa sababu zote hizi, nadhani ni mapema sana kuanza kumshangilia Magufuli kwa ajili ya Harbinder Singh Seth na James Rugemalila kushtakiwa mahakamani leo.
Badala ya kushangilia, tunapaswa kumuuliza Rais Magufuli kwa nini amekamata wafanya biashara waliochotewa mabilioni ya Tegeta Escrow lakini ameacha mawaziri na maafisa wa serikali walioruhusu uchotwaji wa fedha hizo, au wote waliopata mgawo wa fedha hizo.

Tunapaswa tumhoji kwa nini anaelekea kukwepa watu fulani fulani lakini wengine anawakaba koo? ??

Tumwambie kwamba katika sheria za haki za binadamu za kimataifa, mahakama za kimataifa zimesema kwamba, kama ambavyo marais hawana kinga kwa makosa dhidi ya ubinadamu au uhalifu wa kivita, marais pia hawana kinga dhidi ya mashtaka kwa uhalifu wa kiuchumi dhidi ya nchi zao.

Magufuli hastahili kupewa hata benefit of the doubt.
Kumbukeni ya Kikwete na mashtaka ya hujuma ya uchumi dhidi ya Prof. Mahalu na akina Mramba na Daniel Yona. Kikwete huyo huyo ndiye baadae alimteua Prof. Mahalu kwenye Bunge la Katiba. Na Magufuli ndiye aliyemrudisha Prof. Muhongo wizarani baada ya Bunge kumlazimisha Kikwete kumfukuza kazi kutokana na kashfa ya Tegeta Escrow.

We'd not allow ourselves to be taken in and/or fooled by these gimmicks again.

Usiku mwema.
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,316
2,000
Huyo ndio Lissu,kamanda wa ukweli asiemung'unya maneno wala kuremba.

Niliwahi sema na leo narudia.Lissu ulipaswa kuzaliwa katika nchi za wenzetu wanaojielewa lakini sio Tanzania hii na nina hakika huko leo hii ungekuwa umeshapata recognition.

Watu wa Singida Mashariki hatuna cha kuwalipa zaidi ya kusema asanteni kwa kutupa Mbunge wa aina hii.
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,092
2,000
Ni wenye akili timamu tu ndio tunamuelewa Lisu anasimamia nini, lakini usitalajie kundi la mazezeta lenye kaswende ya ubongo kumuelewa Lisu ameandika nini.

Hatutaki double standard kwenye vita dhidi ya ufisadi au maigizo katika vita hii, wahusika wote wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,092
2,000
KAFULILA:LEO NI SIKU MUHIMU KWANGU NA VITA DHIDI YA UFISADI!

Hatimaye imekuwa! Vinara katika ufisadi wa IPTL/ESCROW Singasinga Sethi na Rugemalila watiwa nguvuni. Huu ni uamuzi mkubwa uliosubiriwa sana. Na siku zote sikujua kwanini Mhe Rais alikuwa anahofu kuagiza hatua hii.

Sikujua kwanini kwasababu wakati wa mnyukano wa hoja hii, Mhe Rais alikuwa bungeni na alikuwa sehemu ya maazimio ya Bunge kutaka mitambo ya IPTL itaifishwe na wahusika watiwe nguvuni..

Nakumbuka nikiwa kwenye kipindi kigumu hata kutishwa kuondolewa kichwa na kuitwa majina ya wanyama, yeye alikuwa miongoni mwa mawaziri 5, walionidokeza kwamba ESCROW ni dili.nikomae tu mpaka kieleweke!

Nampongeza Mhe Rais kwa uamuzi huu muhimu uliosubiriwa siku nyingi kuamua hatma ya ufisadi huu uliomshinda vibaya mtangulizi wake.

Singasinga huyu alinifungulia kesi kunidai Sh300bn Mahakama Kuu ya Tanzania mwaka 2014, Agust2015 nikamshinda lakini akamua kunifungulia upya Mahakama ya Kisutu akidai Sh100m, zote akidai nimsafishe kuwa yeye na wenzake hawakuchota zaidi ya 300bn kifisadi.

Kifupi naomba PCCB na DPP wasituangushe watanzania. Nilipata kuwaza kumwomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali anipe kibali niendeshe kesi na hawa majabali wa escrow kwani nina ushahidi wakutosha,Sasa nina furaha kwamba PCCB wameamua kuwaburuza.

Nashauri mambo machache;

1.Mall zote za wahusika hawa ziwekwe chini ya ulinzi kabla hawajahamisha umiliki kwani nimuhimu zikakamatwa kusubiri hukumu ya kesi hii ya Tanzania lakini pia kesi iliyopo Mahakama ya kimataifa ya International Centre For Settlement of Investment Disputes (ICSID).Ambako Sept2016, iliamuliwa tulipe Bank ya SCB-HK kiasi zaidi ya 400bn kwakua ndio wamiliki halali wa IPTL na wenye share certificate za IPTL..

Mwaka huu TANESCO imekata rufaa.Najua TANESCO hawajakata rufaa kushinda kesi bali kuomba wapunguziwe hukumu ifanane na uamuzi wa ICSID wa Feb2014.

Lakini kwakuwa Singasinga Sethi alisaini hati na Bank Kuu ya Tanzania, kwamba deni lolote lotakalotokana na migogoro ya IPTL atawajibika yeye na wenzake wanaomiliki kampuni PAP, ndio maana nasisitiza Mali za watu hawa zishikiliwe.

2.Mtambo wa IPTL uwekwe chini ya TANESCO kama ilivoazimiwa na Bunge Nov2014, tuachane kabisa na kulipa matapeli 7bn kila mwezi ambazo ni malipo ya capacity charges walizokuwa wanalipwa na serikali hii bila kujali IPTL imezalisha au haijazalisha umeme.

3.Mwisho watanzania watambue kwamba huyu Singasinga anaetambulishwa kama mmiliki wa PAP iliyopora 300bn za escrow kama mmiliki mpya wa IPTL,mpaka pesa hizo zinaporwa alikuwa anamiliki asilimia50% tu yakampuni.lakini asilimia 50% zilikuwa zikimilikiwa na kampuni ijulikanayo kama SIMBA TRUST, inayomilikiwa na watu wasiojulikana. Hawajawahi kutajwa popote kwenye report zote.

Nilijaribu kutaka majina yao kwenye Kamati ya Viwanda wakati tukiwahoji BRELA na hata baadae bungeni Serikali iliendelea kusisitiza kuwa majina hayo ni SIRI.Hawa ni wahusika muhimu sana wajulikane kwani inawezekana ndio msingi wa serikali ya awamu ya nne kuibeba IPTL kama mtoto!

Naam, Hongera Mhe Rais kwa hatua hii, nazidi kuomba Mungu kesi hizi zifike mwisho kwani kwangu leo ni siku muhimu katika kumbukumbu zangu kuliko Aprili28,2015, siku niliyopewa tuzo kwa mapambano dhidi ya Ufisadi kwa rejea ya sakata la ESCROW. Kwani tuzo haina maana kama vita haifiki mwisho!

Mwisho nishauli asiwepo yeyote wakulindwa kwa Kinga yoyote kwani Katiba na Sheria vipo kwajili ya watanzania na sio watanzania kwajili ya Katiba na Sheria. Tusipofika huko vita ya UFISADI mkubwa itakuwa ngumu sana kufika mwisho!
David KAFULILA
JUNE19,2017
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom