Lissu karibu nyumbani kwa amani usifuate nyayo za Raila Odinga

Albert Einstein

JF-Expert Member
Aug 24, 2017
384
1,000
Baada ya dosari za uchaguzi mkuu wa Kenya wa 2017, kiongozi wa upinzani alisusia uchaguzi wa marudio na kuanza ziara nje ya nchi akitafuta uungwaji mkono kutoka mataifa na mashirika ya nje.

Tarehe 17.11.2017 zaidi ya wafuasi walifika uwanja wa ndege wa Kenyata wakihimiza kuwa wamefika kumpokea kiongozi wao.

Wahenga walinena, palipo na wengi hapakosi mengi, hivyo ndivyo siku ya ijumaa ya tarehe 17 Nov 2017 ilivyogeuka kuwa siku ya vilio na kuomboleza.

Vurugu kubwa zilizuka baina ya waandamanaji waliojikusanya nje ya uwanja wa ndege dhidi ya vyombo vya ulinzi na usalama.

Waandamanaji walirusha mawe, huku polisi wakijibu kwa mabomu ya machozi, waandamaji walichoma gari la polisi huku polisi wakitumia kila mbinu zikiwemo maji ya washawasha ili kuzuia maandamano yasifike katikati ya jiji la Nairobi, wafuasi wa Raila nao hawakubaki nyuma kuchoma matairi moto na kila aina ya hekaheka ilimradi waweze kuibuka washindi wa vurugu.

Shirika la utangazaji la Ufaransa (Reuters) liliripoti kuwa zaidi ya watu 5 walipoteza maisha kwa risasi za moto kutokana na vurugu zilizozuka pale uwanja wa ndege wa Kenyata japo wafuasi wa Raila waliaswa na kuombwa mapema kujiepusha na maandamano yale.

Polisi walijitetea kuwa watu 5 waliopoteza maisha walipigwa kwa mawe na wanachi wenye hasira kali baada ya kukutwa wakiwa wanapora bidhaa ktk sehemu za biashara, palipo na wengi mengi hutokea.

Unaweza kuuona kama utetezi mwepesi lakini ukweli ni kwamba, katika vurugu za aina hiyo chochote kinaweza kutokea, ikumbukwe kuwa ktk maandamano na mikusanyiko kila mmoja anawaza lake kichwani ndiyo maana huwa kuna uporaji, kuharibu mali za watu na hata ubakaji.

Lakini katika historia, itakumbukwa kuwa watu 5 walipoteza maisha siku hiyo kufuatia maandamano hayo ya kwenda kumpokea Raila Odinga na wengine wengi kujeruhiwa vibaya, lakini kama viongozi wa upinzani wangetumia busara na kuacha maonyesho ya kisiasa yote hayo yasingetokea siku hiyo.

Baada ya mvutano wa muda mrefu leo Raila Odinga anaendelea vyema na Uhuru Kenyata katika ulaji wa keki ya taifa, hakuna kati yao aliyechubuka hata kucha wala kuteguka nyonga kutokana na vurugu hizi za Novemba 2017 wala zile za 2007 baina ya Raila Odinga na Mwai Kibaki enzi za mwenyekiti wa tume ya uchaguzi marehemu Kivuitu.

Tundu Lissu anatarajia kurejea nchini akitokea Ubelgiji ambapo alikuwa akipata matibabu pamoja na kuendelea na ziara za kisiasa ktk mataifa mbalimbali duniani, ni jambo la heri hatimaye Lissu kurejea nyumbani na watanzania wote tumkaribishe Lissu ili aendelee kutoa mchango wake ktk ujenzi wa taifa.

Lakini pia taifa tuko ktk maombolezo ya msiba mkubwa wa kuondokewa na Rais Mstaafu Mzee wetu Mkapa, ni bahati mbaya kuwa msiba huu umetokea katikati ya mipango ya mapokezi ya Lissu.

Matumaini yangu ni kuwa, kama Tundu Lissu au Chadema walikuwa wamepanga ujio wa Lissu uambatane na kishindo kikubwa cha mapokeo, vurugu au shamrashamra basi ingekuwa busara wasogeze mbele kidogo mpaka atakapohifadhiwa mzee Mkapa ndipo mipango yao ya maonyesho iendelee, maana palipo na wengi hapakosi mengi.

Ila kama Chadema na Lissu ni waungwana basi wanaweza kuvunja hizo ratiba za kusherehekea ili Lissu awasili kawaida na ajumuike ktk kumuaga mzee wetu, kisha hayo ya maonyesho yafanyike siku nyingine, mathalani siku ya kuchukua fomu ya kugombea urais pale tume ya uchaguzi nk.

Haitakuwa picha nzuri ujio wa Lissu usababishe vurugu zisizokuwa na sababu, Watanzania wamesubilia muda mrefu huku wakimuombea Lissu apone, basi ni vyema ujio wake uambatane na amani na utulivu, ni vyema kukumbushana ili baadae tusije tukaanza kulalamika kuwa kwanini yametokea ilihali wenyewe mngeweza kuyazuia yasitokee.

Kwa muktadha huo, kuna wakati kila mtu mmoja mmoja anao wajibu wa kujilinda yeye mwenyewe kwa kufanya maamuzi sahihi, pia kuna wakati jamii inapaswa kukumbushana kwa kurejea historia ya matukio yanayofanana na hayo ili linapotokea jambo lisionekane kuwa ni jambo jipya.

Kwa kufanya hivyo kila mtu atachagua anachokiona kinamfaa ili matokeo ya mwishoni yaonekane ni stahili ya kila mtu kulingana na uchaguzi wake yeye mwenyewe, na asilaumiwe mtu mwingine.

Nawasilisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom