Lissu kama una lengo la kweli la kushinda Urais 2025, basi njia hii hapa...

Kwanza kabisa napenda kuwasalim wana jf wenzangu mliopo humu. Ama baada ya salam, niende sasa kwenye mada. Ndugu zang leo nimekuja na ushauri, au njia mbadala itakayomsaidia ndugu yetu Lisu na chama chake kuingia Ikulu kiulaini kabisa bila kutumia katiba mpya, tume huru, wala maandamano yoyote yasiokuwa na tija. Njia hizo ni...

(1) Kwanza arudi nchini kukijenga chama na kuendeleza mapambano ya hoja, na kusimamia sera za chama kikamilifu ili kutupa imani kuwa mpambanaji wetu kaamua kusimama na sisi katika nyakati zote za shida na raha kama vile kina mzee Nelson Mandela, Robert Mugabe, Hakainde Hichilema na wengine wa aina hiyo ambao waliweza kupata ushindi wa kuongoza nchi zao kupitia sera zao na mapambano yao ya ndani.

(2) Abadili aina ya siasa zake kutoka katika siasa za chuki, hasira na visasi, hadi katika siasa za upendo, umoja, mshikamano na uvumilivu. Haiwezekani ugomvi wake na hayati Magufuli, au ugomvi wa chama chake na CCM uufanye kuwa ugomvi wa taifa. Yan aufanye ni ugomvi wa watanzania wote dhidi yake au dhidi ya chama chake. Mpaka kufikia hatua ya kuwaomba wafadhili wetu watunyime kabisa misaada ya pesa ambazo huwa zinasaidia kuboresha elimu yetu kwa manufaa ya watoto wetu, au kusaidia kununua madawa kwa ajili ya afya zetu na za watoto wetu nk.. Kibaya zaidi alitaka tuwekewe na vikwazo, ili sisi wenzangu na mimi tusijaribu hata kupata fursa ya kufanya biashara zetu nje ya mipaka ya nchi yetu. Hii ilishangaza sana watanzania kuona mtu mwenye elimu kama Lisu anawezaje kufanya maamuzi ya kipuuzi, na kikatili kwa nchi yako na watanzania wenzako namna ile. Omba msamaha kwa hili, nina imani utasamehewa na kura utapewa.

(3) Ajaribu kuwa na misimamo thabiti isiyoyumbishwa na mtu yoyote, mwenye chochote. Sio leo atuambie hivi afu kesho abadilishe kauli yake atuambie vile, hiyo ni sawa na unafiki, uongo au uzushi. Lazima ajue kuwa siku zote ukweli hujenga, na uongo hubomoa.

(4) Awaombe msamaha wanachadema na watanzania waliomuamini, kwa kitendo chake cha kuwadanganya, na kuwachukulia kama wao ni maboya wasioweza kutumia hata kilo nzima ya akili zao kujua ukweli na uongo wa kauli zake, kama tunavyoona pichani.

(5) Mwisho namshauri ili aweze kujenga siasa zenye malengo, basi akamtafute ndugu Hakainde Hichilema amfunze siasa za kweli. Huu ndio ujumbe wangu kwake, najua hapa kuna wapambe wake watamfikishia. Unajua dunia ya sasa mtu anaweza asikupe chakula, lakini akakuonesha njia nzuri ya kukipata hicho chakula. Na kuna mtu anaweza akakupa chakula lakini akakataa kata kata kukuonesha njia ya kukipata hicho chakula.

Asanteni sana!

UTAKUWA NA MATATIZO YA AKILI, KAMA UNATAKA AU KUWAZA LISSU AJE KUWA RAIS TANZANIA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 
..hawakumaanisha "dikteta" anayedhulumu wapinzani.

..walimaanisha kiongozi mkali atakayewadhibiti wazembe na wabadhirifu waliokuwa serikalini.

..kwa bahati mbaya alipatikana dikteta mbadhirifu wa fedha za umma, na mkatili kwa vyama vya upinzani.
MPAKA UNAKUFA UTAKUWA UPANDE WA LOOSERS TU, KULAUMU TU, MPAKA UPATE KANSA YA VIDOLE
 
Back
Top Bottom