Straight Talk Africa na Shaka Ssali: Tundu Lissu jino kwa jino na Balozi Wilson Masilingi

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,072
103,284
Ssali.PNG

Mwanasiasa maarufu duniani Tundu Lissu leo atakuwa akihojiwa na mwanahabari nguli Africa Mzee Shaka Ssali kuhusu demokrasia ya Afrika.

Ssali anayeheshimika kuendesha vipindi makini vya Straight Talk Afrika anampa heshima Tundu Lissu kutokana na kukunwa na maono yake

Kipindi hiki kinaweza kurushwa saa 3:30 kupitia Star TV au Kiss Fm

======
VIDEO:




Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilson Masilingi jana usiku walihojiwa katika kipindi cha Straight Talk Africa kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Sauti ya Marekani (VOA), huku kila mmoja akipangua hoja za mwenzake.

Masilingi amekuwa balozi wa pili kumjibu Lissu baada ya siku tano zilizopita Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk Abdallah Possi kumjibu Lissu baada ya mbunge huyo kueleza madai mbalimbali kuhusu Serikali na jinsi alivyoshambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 Septemba 7, 2017 wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha

Deutsche Welle cha nchini humo.

Katika kipindi cha jana kilichoongozwa na mtangazaji maarufu, Shaka Ssali kilichokuwa na mada ya ‘Haki ya Uhuru wa kujieleza’, kilikuwa na wanajopo wengine ambao ni Jon Temin kutoka taasisi ya Freedom House na mwanasiasa wa upinzani wa Uganda, Robert Chagulani maarufu kama Bobi Wine.

Akijibu maswali ya mtangazaji huyo kuhusu uhuru wa kujieleza na sababu ya Lissu kushambuliwa kwa risasi, Balozi Masilingi amesema licha ya eneo aliloshambuliwa kuwa ni la nyumba za Serikali lakini halina uhusiano na kubanwa kwa uhuru wa kujieleza.

Lissu alikuwa nchini Ubelgiji akipatiwa matibabu alikokwenda Januari 6, 2018 akitokea hospitalini Nairobi, Kenya.

Mnadhimu mkuu huyo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni nchini alipelekwa Nairobi akitokea Hospitali ya Rufaa ya Dodoma baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 mchana wa Septemba 7, 2017 akiwa katika makazi yake Area D jijini Dodoma akitoka kuhudhuria vikao vya bunge.

Lissu ambaye Desemba 31, 2018 alieleza kwamba amehitimisha shughuli za utabibu na sasa anaendelea na mazoezi ya kutembea, hivi karibuni alifanya ziara nchini Uingereza na kufanya mahojiano na Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC). Pia amefanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa.

“Huwezi kuhusisha hilo moja kwa moja na uhuru wa kujieleza bila kuweka uthibitisho. Ndugu yangu alishambuliwa na Rais (John Magufuli) alitoa tamko la kulaani tukio hilo na kutaka vyombo vya dola kuchunguza tukio hilo. Kila mtu aliguswa na tuko hilo.”

“Uchunguzi bado unaendelea, wanamsubiri arudi (Tanzania) atoe ushirikiano, dereva wake anasubiriwa kutoa ushirikiano. Sasa utakuwaje jaji kuhukumu hilo?” alihoji Masilingi.

Katika majibu yake Lissu amesema, “Nilishambuliwa kwenye nyumba za Serikali, nilipigwa mara 16 na nimefanyiwa operesheni 22. Swali la kujiuliza, nani aliyetoa agizo la kuondoa ulinzi katika nyumba za Serikali?”

“Pili, hilo eneo linalindwa na CCTV (kamera) ziliondolewa siku moja kabla ya tukio. Hakuna anayejua zilikopelekwa kwa sababu polisi hawasemi walizipeleka wapi. Ninazungumza na watu, hakuna mtu aliyehojiwa.”

Chanzo: Mwananchi
 
View attachment 1015111

Mwanasiasa maarufu duniani Tundu Lissu leo atakuwa akihojiwa na mwanahabari nguli Africa Mzee Shaka Ssali kuhusu demokrasia ya Afrika.

Ssali anayeheshimika kuendesha vipindi makini vya Straight Talk Afrika anampa heshima Tundu Lissu kutokana na kukunwa na maono yake

Tuwe pamoja

Weraweraaaaaaa!

Kuna watu wanajinyea aiseee!
 
View attachment 1015111

Mwanasiasa maarufu duniani Tundu Lissu leo atakuwa akihojiwa na mwanahabari nguli Africa Mzee Shaka Ssali kuhusu demokrasia ya Afrika.

Ssali anayeheshimika kuendesha vipindi makini vya Straight Talk Afrika anampa heshima Tundu Lissu kutokana na kukunwa na maono yake

Tuwe pamoja
Baada ya ziara hizo ndiyo anaapishwa kuwa rais?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom