Lissu: Kama ACACIA ni wezi, kwanini Polisi wamewapiga Mabomu wananchi wa Tarime?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,651
2,000
"Tumeambiwa Acacia ni wezi, hawana leseni ya uchimbaji, hawajasajiliwa nchini. Wananchi wa Tarime walipoamua kuchukua hatua wamepigwa mabomu.

Kama Acacia ni wezi na hawajawahi kuwa na leseni kwa nini polisi wa Magufuli wanawapiga wananchi wa Tarime mabomu? Nani anayetetea wezi hapa

Nani mchochezi kati ya Rais aliyelia hadharani kuwa Acacia wezi, na mbunge wa Tarime aliyewaambia wananchi kuchukua hatua dhidi ya wezi hao?"

Tundu Lissu amehoji hayo baada ya Polisi kuanza kumtafuta John Heche kwa kuchochea wananchi wavamie Migodi ya dhahabu.

Akiwa bungwni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche alifunguka na kusema kwa kuwa Rais Magufuli kupitia ripoti ya pili ya mchanga amesema kampuni ya ACACIA ni feki na haipo basi yeye anawaambia wananchi wa jimbo lake wajiandae kuingia mgodini kuchukua kila kitu.

Heche alisema hayo bungeni na kudai kuwa atasimamia zoezi hilo na kuhakikisha kuwa ndege za kampuni hiyo zikitua mgodini kwa ajili ya kubeba madini basi zinapigwa mawe kwa kuwa wananchi wa jimbo lake la Tarime ambapo hiyo migodi ipo wameumizwa sana kusikia hiyo kampuni inayochukua mali zao ni feki na hewa.

"Kampuni ile ya ACACIA Rais amesema feki na hakuna 'formula' ya kukamata mwizi mlisema wenyewe, formula ya kukamata mwizi ni kupambana naye sisi hatutaruhusu madini yatoke pale ndege ikitua itapigwa mawe, magari yao tutayakamata kwanza tunawadai fidia nyingi kweli kweli pale Tarime. Mhe. Spika sisi tulitegemea Mhe. Rais aseme madini yasiondoke nchini mpaka mambo hayo yote yapitiwe, tutazuia mchanga madini yanaondoka. Rais amesema ACACIA ni mwizi wewe unataka utaratibu wa kukamata mwizi Tarime, sisi watu wetu wameumia sana na maji ya sumu, ng'ombe wamekufa, watu wamepigwa risasi kwa mujibu wa ripoti ya Waziri wa Nishati na Madini watu wa Tarime zaidi ya 64 wameuawa pale mgodini" alisema Heche

Mbali na hilo John Heche alisema kuwa kama serikali itamkamata kwa maamuzi ambayo atafanya basi Watanzania watajua kuwa serikali haipo tayari kupigana vita hii ya kupigania rasilimali za nchi hii, hivyo amewataka watu wa jimbo la Tarime wajiandae na kuanza maandalizi ya kupigania rasiliamali zao ili waone kama serikali itapeleka jeshi la polisi kulinda mali za wezi hao.

Kwa siku tatu mfululizo wananchi wa Tarime wamekuwa wakivamia Mgodi wa dhahabu usiku na mchana huku Polisi ikiwapiga Mabomu na kuwatawanya.
 
Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,806

Kama Heche kaamuru hivyo basi anastahili kuchukuliwa hatua kali. Vipi aliwaamuru wakavamie pia majumbani ya Masamaki? Mbunge wa ajabu Sana huyu
 
Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
35,296
2,000
Cc: jingalao, MOTOCHINI, Troll JF, Lizaboni, utaifakwanza, cocochanel, Ghosryder.......
 
minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
15,709
2,000
Penzi la Lissu kwa Acacia ni zaidi ya Mahaba Niuwe.
Kivipi? Kumbuka Lisu kaanza vita zamani wewe unakuja kukomaa na makapi yenye 5% tu lakini kule kwenye 95% bado wizi unaendelea ndege zinatua kuchukua madini na kwenda nje wizi wa mgoni jikoni ni mkubwa kuliko hata hiyo michanga ambayo lisu kanipigia kelele miaka 18 leo hii mnajidai kuwa CCM ndiyo inapiga vita wezi huku wananchi wenye Dhanana wameamua kuchukua chao lakini CCM mnawapiga mabomu, waacheni wachukue kwani mwizi kawanunua CCM kuwapiga watanzania?
 
minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
15,709
2,000
Bwana Mpya... Acacia anamzuzua amekuwa haambiliki.
lisu hana Mahaba na Acacia yy aliamua kusimama kwenye kutengua sheria na mikataba mibovu waliyopewa na CCM kwanza kabla ya chochote ili kulinda masilahi ya Nchi endapo Acacia wataamua kwenda mahakamani, cha Ajabu wale CCM Wajanja wapigani wameamua kueneza propaganda juu ya Lisu ili kumtoa kwenye njia baadae CCM wajidai wao ndiyo wanapigana vita kweli, watanzania wa sasa wameamka wanajua kila kitu wanafahamu kuwa kama si wabunge wa CCM wa ndiyoooo..Leo hii kusingekuwa na mjadala juu ya hilo watu wangekuwa busy na mengineyo ya maendeleo.
 
Mama Obama

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
1,571
2,000
Lissu anaongea kama sio wakili. Hata kama tunasema Acacia wezi, Hakuna sheria ya kuingia migodini na kufanya fujo, hii ni mob justice. Ukiibiwa unapeleka mashitaka yako serikali na huruhusiwi kujichukulia sheria mikononi mwako. Uingereza mwizi akikuingilia nyumbani kwako huwezi kumpiga zaidi ya kujikinga asikuumize.
 
minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
15,709
2,000
Ripoti kutoka lumumba inaseje kwan
Wao napo wanajichukulia chao mapema kwa kutengeneza michango mbalimbali ikiwemo Dili za lipumba kuwakomoa kuwakoroga Wapinzani pia kupitia kwa msajili wa vyama kuruhusu Luzuku kuibiwa na Lipumba kwa sasa CCM kila mmoja yupo busy kutengeneza fursa mapema maana hawajui siku wala saa ya kuleteana soo.
 
cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,518
2,000
Huyo sasa anahitaji kumuona daktari, hakuna lingine. Mumshauri awahi mapema

Magufuli amebana watu hadi wanaisoma namba kisa yale ya awamu zilizopita za bahasha nje nje hakuna tena, hadi anajaribu tena na tena ni hatari.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom