Lissu juu ya kauli ya Rais kwenye sherehe za Siku ya Sheria

Blessed Jr

Senior Member
Nov 17, 2016
134
235
Na TUNDU LISSU

Nimesikiliza sehemu ya hotuba ya Rais Magufuli wakati wa sherehe za Siku ya Sheria leo. Nimemsikiliza aliposema wanaokamatwa na nyara za Serikali au madawa ya kulevya wanastahili kuchukuliwa hatua bila kufuata taratibu za kawaida za kisheria hasa pale wanapokamatwa 'red-handed.'

Amesema na mawakili wanaowatetea nao wanastahili kukamatwa na kuwekwa rumande ili na wao 'waisome namba' ili, pengine, waache kuwatetea 'wakosaji' hawa. Wote waliokuwa wanamsikiliza Rais, akiwemo Kaimu Jaji Mkuu na Majaji wenzake wa Rufaa na wa Mahakama Kuu, mawakili na wageni wengine waliokuwapo pale, waliangua kicheko kikubwa. Wanafikiri alichokisema ni cha kuchekesha.

It's not funny at all. Jeshi letu la polisi limekubuhu katika kusingizia watu vitu vya uongo.

Kwa polisi wa nchi hii, planting evidence, kuwekea watuhumiwa nyara za serikali au madawa au silaha ili wawakamate na kuwafungulia mashtaka mazito ili kuwakamua watoe pesa, ni kitu cha kawaida sana. Polisi wetu wamekubuhu katika kusachi watu bila kuwa na search warrants na bila kufuata sheria na taratibu za kufanya sachi.

Hivi ndivyo wanavyopandikiza ushahidi. Polisi wetu wamekubuhu katika kutesa watuhumiwa ili wakiri makosa ambayo, mara nyingi, hawakuyafanya. Yote haya tunayafahàmu na mawakili, majaji na mahakimu wa nchi hii wanayafahamu sana. Wanakutana nayo kila siku mahakamani.

Kauli ya Rais wetu kwamba watuhumiwa hawa washughulikiwe mara moja bila kujali taratibu za kisheria zilizopo ni baraka kwa matendo haya machafu ya jeshi letu la polisi. Ni presidential blessings for state lawlessness na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

Ndicho kitakachofuatia bila shaka yoyote. Yamekuwa yanatokea muda wote, sasa yataongezeka kwa sababu yana baraka za Rais.

Kilichonishangaza mimi sio alichosema Magufuli, huyu tumeshamzoea, bali reaction ya waliokuwa wanamsikiliza ambao wanafahamu fika madhara ya kauli hii ya Rais. Kwingineko duniani mawakili wangetoka nje in protest na Rais angeshambuliwa vikali kila mahali kwenye vyombo vya habari, kama tunavyoona yanayomtokea Donald Trump Marekani. Sio Tanzania.

Kwetu kila anaona ni kichekesho. Kuhusu mawakili kukamatwa. Miezi kadhaa iliyopita Kamanda wa Polisi Zanzibar Ahmed Msangi, kama sikosei, alitoa kauli ya kuwatisha mawakili wa Zanzibar waliokuwa wanawatetea watuhumiwa wa kesi za kisiasa walizofunguliwa viongozi na wanachama wa CUF huko Zanzibar.

Kamanda huyo alisema mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao nao watakamatwa na kuwekwa ndani. Kauli hiyo ilishambuliwa vikali, na kwa usahihi kabisa, na Chama cha Mawakili Zanzibar na wenzao wa TLS.

Leo Magufuli ametoa kauli hiyo hiyo, na waliokuwa wanamsikiliza wamechekelea badala ya kutoka nje ya ukumbi in protest!!!! Tusubirie tuone kama TLS watadiriki kutoa kauli ya aina waliyoitoa wakati wa sakata la Zanzibar au wakili mwenzao alipokamatwa Loliondo.

Mimi binafsi nina mashaka makubwa kama watadiriki kufungua mdomo. Katiba yetu inatamka wazi kwamba kila mtuhumiwa anahesabika kuwa hana hatia mpaka mahakama zitakapothibitisha vinginevyo. Rais Magufuli haamini hivyo.

Kwake kila mtuhumiwa sio tu ana hatia bali pia hastahili kusikilizwa wala kupata utetezi wa wakili mahakamani. Anachostahili ni adhabu tu, and the bigger the punishment the better. Katiba yetu inasema kila mtuhumiwa ana haki ya 'kusikilizwa kwa ukamilifu.'

Haki hii, kama ambavyo mahakama zetu za juu zimesema mara kwa mara, inajumuisha kusikilizwa kupitia kwa wakili. Na juzi Jumanne tumepitisha haraka haraka na kwa mbwembwe nyingi Sheria ya Msaada wa Kisheria. Sheria hiyo inasema kila mtuhumiwa wa kesi ya jinai ana haki ya kupatiwa wakili bila malipo yoyote kama Jaji au hakimu akiona inafaa.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama, mteule wa Rais, amepewa mamlaka ya kuwalipa mawakili watakaowatetea watuhumiwa hawa. Kwa hiyo fedha za umma zitatumika kuwalipa mawakili watakaowatetea watuhumiwa hawa wa makosa ya jinai. Bila shaka Muswada wa Sheria hii ulipitia kwenye Baraza la Mawaziri kama ilivyo kawaida.

Leo Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri anatamka hadharani kwamba mawakili watakaowatetea watuhumiwa wanaokutwa na nyara za serikali au madawa ya kulevya nao wakamatwe na kutiwa ndani.

Waziri ambaye juzi alikuwa anashadidia watuhumiwa hawa wapatiwe msaada wa kisheria bila malipo anachekelea kauli ya Rais. Majaji na mahakimu watakaoamua watuhumiwa hawa wapatiwe msaada wa kisheria nao wanachekelea.

Na mawakili ambao wanatakiwa na sheria watoe msaada wa kisheria na ambao watakuwa victims wa kauli ya Magufuli nao wanachekelea. I can only imagine Rais Uhuru Kenyatta angetoa kauli ya aina hii mawakili, wanasiasa, waandishi habari na wananchi wa kawaida wa Kenya wangemfanyaje. Wa kwetu wanachekelea. This happens only in Tanzania.

 
Tundu anawakilisha akili za upinzani a nataka kupata hela kwa kuwatetea akina peti man walioshikwa red handed....hao ndio wapinzani wanaotoka dola.......njaa kichwani bora tu wa endelee kuwa wapinzani MILELE. .....Leo wameshinda wakampinga Makonda kwa kushika wauza unga...chadema ni genge la wahalifu
 
Tundu anawakilisha akili za upinzani a nataka kupata hela kwa kuwatetea akina peti man walioshikwa red handed....hao ndio wapinzani wanaotoka dola.......njaa kichwani bora tu wa endelee kuwa wapinzani MILELE. .....Leo wameshinda wakampinga Makonda kwa kushika wauza unga...chadema ni genge la wahalifu
Hujakutwa na kesi za kubambikiziwa.Na kama.issue ni ufisadi.Mwenyekiti wenu msafi??Hebu muulize zile.Bilioni nane za meli.mbovu nani yuko nyuma yake??Lugumi na Escrow je??

Kabla hujamnyooshea adui yako kidole angalia vidole vyako vingapi.vinakusuta.Jaribu leo uone
 
Nyie ccm team police wa Tanzania wanaweza kukubambika kisa mnagombea bibi sasa mahakama ifanye kazi yake
 
Tundu anawakilisha akili za upinzani a nataka kupata hela kwa kuwatetea akina peti man walioshikwa red handed....hao ndio wapinzani wanaotoka dola.......njaa kichwani bora tu wa endelee kuwa wapinzani MILELE. .....Leo wameshinda wakampinga Makonda kwa kushika wauza unga...chadema ni genge la wahalifu
Hapana, lissu anazungumza nini sheria inasema, wewe unazungumzia hisia zako..

Hii nchi inaendeshwa kwa misingi ya sheria,na ni takwa la kisheria kuwepo kwa "presumption of innocence"..sasa kama utampandisha mtu kizimbani alafu umnyime haki ya kutetewa na mtu mwenye kuijua sheria kulikuwa na haja gani ya kumpandisha kizimbani?? Si ungeagiza akafungwe moja kwa moja?

Rais anatakiwa aangaike na polisi wake kama wanakula rushwa au wanafanya upelelezi wenye matege waache na sio kuwanyima watu haki ya kupata mawakili!

Kama umemkamata mtu na una ushahidi wa kutosha kumtia hatia kwanini uogope yeye kupata wakili??

Ujinga!
 
Akili ya kawaida hutafakari alichokisema Rais.

Akili finyu zitalaumu alichokisema Rais.

Naamini Polisi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ofisi ya Mwendesha mashitaka wa Serikali, na Mahakama, ina watumishi wenye weredi, taaluma na watenda haki.

Hivyo shutuma za Mh Lissu ni za ajabu na kudharirisha watumishi wote katika hivyo vyombo alivyovitaja vya kulinda na kutetea haki.

Mh Lissu, kama mwanasheria na Mbunge anayo nafasi ya kupeleka hoja zake hizo mahakamani au kwenye Bunge.

Hakika Mh Lissu, katika taaluma yake ya uanasheria na nafasi yake ya Ubunge, hajijui.
 
Mheshimiwa wakili Lissu, tunaokutana na polisi kila siku tumekuelewa sana. Hili wala haliitaji shule ya darasani. Wasio na uelewa watakuelewa muda ukifika.
Maana hata Bwana Yesu, kuna waliomkili kwamba alikuwa Mfalme wa Wayahudi baada ya kuwa ameishakufa msalabani. Mfano mzuri ni yule askari wa kiyahudi aliyebaki akilinda mpaka mauti inamfika.
 
Ningependa tu watu wote wanyamaze tuangalie mwisho wa kuingilia Bunge na mahakama kama kuanweza kuleta faida kwa serikali "
wote tunajua mwisho huwa mbaya. kwa hiyo hakuna sababu ya kufanya hiyo experiment hatari.
 
Tundu anawakilisha akili za upinzani a nataka kupata hela kwa kuwatetea akina peti man walioshikwa red handed....hao ndio wapinzani wanaotoka dola.......njaa kichwani bora tu wa endelee kuwa wapinzani MILELE. .....Leo wameshinda wakampinga Makonda kwa kushika wauza unga...chadema ni genge la wahalifu
Unajua ulichoandika mkuu
 
Kuna watu wana hoja za ajabu sana sijui hii elimu yetu imewasaidia vipi.
 
Back
Top Bottom