Tundu Lissu: Hotuba ya Rais Magufuli kuhusu Makontena ya Mchanga, inatia shaka ya rule of state

unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Amshauri?? Amshauri nani? Huyo aliekwenda mwenyewe kuchukua fomu za Urais? ..umeshawahi kumpigia mbuzi gitaa wewe?
 
I wonder someone is crawling back the old story authored by Lissu, what is the motive?
 
Hawa wa upinzani si walipiga kelele kabla nchi inapoteza pesa, sasa haya wanayoyaongelea now je waliwahi kupendekeza bungeni kabla!?
Usiwe unaandika wakati unakung'utwa.....sii hizi serikali zenu zilishakataa mikataba kujadiliwa kwenye bunge, wakato huo huo imefanywa kiusiri ili zipatikane hela zenu za kampeni??? Sasa hilo bunge unaloliongelea kujadili ni lipi?? Hili la atickson mwansasu?? Mmelewa sana nyie....vidole mnavyovikalia...vikiwanukia...mnalaumu wapinzani
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Hauna sababu ya kuwa na Hasira
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Angetaka ushauri angewashirikisha wapinzani sio kuwakandamiza na kuwafanya maadui.
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Kwani huwa hasomi humu? Si ataona mwenyewe
 
Kama mkataba/sheria inamruhusu kusafirisha makinikia na badala yake anasafirika mchanga wenye dhahabu na wala si makinikia then mwenye kosa ni mwekezaji mwenyewe. Kwenye hili Lissu amakurupuka au anataka wampe kazi au tayari wameshampa kazi ya kuwa tetea mafisadi wa dhahabu
Hakuna mpumbavu wa kusafirisha mchanga. Mchanga usafirishwe kwa madhumuni gani? Kinachosafirishwa ni concentrate ila kwa sababu kwa watanzania kila saloon car ni taxi, hata concentrates wanaita mchanga. Barrick/Acacia hawajawahi kusafirisha mchanga.
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Kama huna data mkuu usiongee sawa raisi kaisha sema hashauriki yeye ndio anapanga nani akae wapi na nani afanye mini na yeyote atakaye kuwa na kiherehere kumshauri raisi atakiona cha mtema kuni. Sasa mh. Tundu hana damu au?
 
Tundu hayo unayoyatetea kwa maslahi ya nani,utadai mikataba ndio inayolinda yote hayo ,je mbona tuna mikataba mingi mibovu iliyotiwa saini kwa njia za rushwa kwa hiyo tuache tu kwa kuwa akina Kafumu waliruhusu,kwa mpango huu nashukuru Mungu ,Chadema mtaiona tu ikulu ,zamani mlijipambanua kama watetea haki na maslahi ya nchi ,siku hizi Chadema inateteta kila aina ya uozo,ufisadi.Chadema mshakuwa chama cha hovyo kabisa.
sikuhizi wameacha kuimba reggae wanaimba ndombolooo
 
Hotuba ya jana ya Rais Magufuli ni ushahidi mwingine, kama bado kuna shaka, ya rule of state lawlessness ambayo mtukufu anatuingiza kama taifa. Natumia marufuku yake ya kusafirisha mchanga wenye madini nje ya nchi kama mfano.

Zaidi ya dhahabu, mgodi wa Bulyanhulu unazalisha pia madini ya fedha (silver), cobalt, copper na cadmium (ya mwisho kama sikosei!). Bulyanhulu ni mgodi pekee nchini wenye madini yote hayo na mchanga unaosafirishwa nje unatoka Bulyanhulu. Madini yote hayo, kwa mujibu wa Sheria ya Madini na Mikataba ya Uendelezaji Madini (MDAs) waliyopewa na Rais Ben Mkapa na kurudiwa na Jakaya Kikwete, ni mali ya wawekezaji.

Mgodi wa Bulyanhulu unafanya smelting ya dhahabu tu (takriban 70% ya processing yote). 30% iliyobaki inafanyikia Japan ambayo ina hiyo capacity ya smelting ya hayo madini mengine.

Ndio maana mchanga huo umekuwa unasafirishwa kwenda Japan tangu 2001. Sasa a smart president angewaelekeza wawekezaji wajenge kwanza hiyo capacity ya smelting ndani ya nchi kabla ya kupiga marufuku export ya mchanga. Kwa kuzingatia kwamba wawekezaji hawa wanalindwa kisheria na kimkataba, a smart president would've renegotiated the MDAs or changed the relevant law ili kufanya processing yote ifanyike internally.

Badala ya a smart president, tuna JPM anayeamini kwamba ametumwa na Mungu kuinyoosha nchi hii na neno lake ndio sheria. Matokeo yake, atagombana na wawekezaji na serikali zao na mabwana wakubwa wa kifedha duniani ambao ndio wamiliki halisi wa rasilmali zetu.

Watampeleka kwenye arbitral tribunals za kimataifa ambazo Mkapa na Kikwete walizikubali kuwa ndio mahakama za migogoro kati yetu na hao tuliowapa rasilmali zetu. Na tukipelekwa huko hatuponi kwa sababu tutakuwa tumevunja mikataba na sheria zinazolinda wawekezaji. More importantly, hatapata hicho anachokifikiria, i.e. internal capacity ya mineral processing yote kwa sababu we simply don't have that capacity currently.

Na, kwa taarifa ya wale wasiojua mambo haya, huo mchanga unaosafirishwa nje sio magwangala. Magwangala ni rock waste yanayotupwa pembeni ya migodi baada ya dhahabu kutolewa. Yana madini kiasi kidogo sana ambayo sio commercially viable kwa wawekezaji kuyavuna. Hayo ndio madini Magufuli 'aliyowagawia' wananchi jana. Ni makapi yanayoachwa nyuma baada ya karamu ya wawekezaji. Hiyo, kwa busara za John Pombe Magufuli, ndio stahili ya waTanzania waliomchagua.

Evo Morales wa Bolivia alikuwa na mikataba kama ya kwetu alipochaguliwa in December ya 2006. Cha kwanza alichofanya ni kuiondoa Bolivia kwenye MIGA Convention na kwenye bilateral investment treaties (BITs) zilizokuwa zinalazimisha international arbitration kwenye migogoro ya uwezekaji. Baada ya hapo ndio akabadilisha sheria na mikataba ya uwekezaji iliyoipa Bolivia sehemu kubwa ya umilikaji wa gesi na mafuta ya nchi yake. Of course, Morales is a Bolivarian na rafiki wa Castro, marehemu Hugo Chavez na wakushoto wengine. Magufuli is none of the above. He's a proto-fascist who believes in nothing but violent state power.

TUNDU LISSU
Mwanasheria mkuu
CHADEMA
Acha kushindana na kila kitu raisi anachotolea maamuzi. Tumekuchoka. Acha kutafuta sifa za kitoto. U r too radical.
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Anaweza kumuandikia Kitabu lakini anashaurika! !
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Sasa huyo unayemtetea anashaurika au unataka kumlaumu Lissu bure?
 
Maelezo ya lisu ni mazuri sioni alipo kosea kwani tiyari Mkuu kaishapiga stop ila hi ni eidha kutotaka
na kukosa ushauri kutoka kwa wataalam au kuona yeye kauli yake inatosha bila kuangalia athari za badae.

Nilichogundua kutokana na ushauri wa lisu tunaweza kubadili mikataba hii ya madini kwa kufuata taratibu bila kukurupuka na isiwepo athari yoyote kwa taifa.
 
Hivi kwa nn watu mnatoa povu sana kuwatetea hawa jamaaa????? hv watanzania tutaendeshwa sana na hawa wanasiasa maana ndo hao walikua wanapiga kelele kua mikataba ya madini ni mibovu leo wanawatetea !!!!hapo mm ndo hua nachoka na tz jamaan wanatuachia mashimo tu hao mm naona rais kaanza vizuri na hilo ili wasione tz ni shamba la bibi yao
 
Nasikia harufu ya kudaiwa fidia kama ile meli ya samaki.
Ni kweli, japo watajua kuwa yule kipofu kapata macho! Wametuibia sana aiseee!!! Mchana kweupe mtu anatorosha dhahabu haijalipiwa kodi wala nini halafu wanadai Mchanga!!!!
Sikubalini na mkuu kwa suala la Bashite lakini kwa kuzuia huu wizi wa mchana nampongeza sasa
 
Tundu hayo unayoyatetea kwa maslahi ya nani,utadai mikataba ndio inayolinda yote hayo ,je mbona tuna mikataba mingi mibovu iliyotiwa saini kwa njia za rushwa kwa hiyo tuache tu kwa kuwa akina Kafumu waliruhusu,kwa mpango huu nashukuru Mungu ,Chadema mtaiona tu ikulu ,zamani mlijipambanua kama watetea haki na maslahi ya nchi ,siku hizi Chadema inateteta kila aina ya uozo,ufisadi.Chadema mshakuwa chama cha hovyo kabisa.
NAsubili kuona la shonga jemsi wakilikumbatia
 
Tundu hayo unayoyatetea kwa maslahi ya nani,utadai mikataba ndio inayolinda yote hayo ,je mbona tuna mikataba mingi mibovu iliyotiwa saini kwa njia za rushwa kwa hiyo tuache tu kwa kuwa akina Kafumu waliruhusu,kwa mpango huu nashukuru Mungu ,Chadema mtaiona tu ikulu ,zamani mlijipambanua kama watetea haki na maslahi ya nchi ,siku hizi Chadema inateteta kila aina ya uozo,ufisadi.Chadema mshakuwa chama cha hovyo kabisa.
Mkuu, mkataba ukishatiwa saini basi unakua valid, whether mchakato wake ulikua au haukua na rushwa. Maamuzi yanayokwenda kinyume nao basi sheria zipo zinazoongoza.
 
Back
Top Bottom