Tundu Lissu: Hotuba ya Rais Magufuli kuhusu Makontena ya Mchanga, inatia shaka ya rule of state

wewe ukituliza ubongounaweza hata mshauli rais.
ila kwa domo lako bovu lisilo na staha ,hata mimi diwezi kukusikiliza hata uje na point.
we msomi uchwars ebu toa udhauri kwa staha.
we unafikiri kuongea ovyo ndio kiki?

Ndiyo maana hata darasani kuna wanaopata ZERO si sababu hawajui sababu wanafikiria kama wewe,anamchukia Mwalimu na somo pia matokeo yake anazungusha
 
Kama mkataba/sheria inamruhusu kusafirisha makinikia na badala yake anasafirika mchanga wenye dhahabu na wala si makinikia then mwenye kosa ni mwekezaji mwenyewe. Kwenye hili Lissu amakurupuka au anataka wampe kazi au tayari wameshampa kazi ya kuwa tetea mafisadi wa dhahabu

Umeshausoma huo MKATABA?Wanaotoa ushauri wameusoma na wanatuelekeza nini tufanye.Uko busy kuangalia yuko Chama gani
 
Nnchi ni yetu sote,madini yapo nchini kwetu. Ni muhimu sana rasilimali hii inufaishe wote tujaribu kutafuta njia ya kusaidia ili mali hii inufaishe uma wa watanzania na si vinginevyo.
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Basi utakua hujui maana ya upinzani, washauri wake wapo, huyu ni mpinzani ni mkosoaji sio waziri au katibu wa madini.
 
Hawa wa upinzani si walipiga kelele kabla nchi inapoteza pesa, sasa haya wanayoyaongelea now je waliwahi kupendekeza bungeni kabla!?
kipi ambacho upinzani inapendekeza bungeni wabunge wenu wa CCM wakakubali? Kwanza juzi si JPM kasema hakuna kuwapa airtime upinzani? Nyinyi endeleeni kunyoosha nchi halafu tuone kama haijakatika.

Makonda Oyeeeeee(kwa sauti yako)
 
Kama mkataba/sheria inamruhusu kusafirisha makinikia na badala yake anasafirika mchanga wenye dhahabu na wala si makinikia then mwenye kosa ni mwekezaji mwenyewe. Kwenye hili Lissu amakurupuka au anataka wampe kazi au tayari wameshampa kazi ya kuwa tetea mafisadi wa dhahabu
unaambiwa 70% ya extraction na pu rification ya dhahabu inafanyika hapa na miche ya dhahabu inapakiwa kwenye ndege inaondoka.

mchanga ambao una perentage ndogo ya dhahabu na madini mengine ndo una pelekwa japan

wewe badala ya kuhoji tunanufaikaje kwenye hiyo 70% ya dhahabu ambayo inaondoka bila kificho unahoji makombo yenye 30% nyie mna akili kweli?? ccm imewaroga
 
Very sorry kwa vijana WA Lumumba waliomo humu! Mada kama hii imewashinda kuielewa, hawaoni hoja zozote, wameishia kwenye kuonesha Ubashite wao! Tulieni, someni tena na tena,ili tuvuke kuna mambo ya Muhimu sana Lissu kashauri!
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Rais mwenyewe kushauriwa sasa lissu akae kimya bila kusema ukweli,naona pombe imekaa kichwan
 
Umaarufu ule ule wa waafrika, anasubiri jambo litokee ndipo ajichukulie maujiko mbele ya watu wasioweza kuyatazama mambo kwa jicho la tatu.

Waafrika tunao ugonjwa wa kuwa reactive badala ya kuwa proactive. Wazungu waliotutawala hujifunza kuwa proactive, hujitahidi kadri wawezavyo ili wawe ni waanzilishi na ideas za kwao wenyewe badala ya kuwa wakosoaji wa ideas za wengine.
 
CHADEMA WAMEPOTEZA UELEKEO
HAWAONGEI KWA FAIDA YA NCHI
WANAPINGA MAZURI YA SERIKALI
PUMBAVU KABISA
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Utamshauri mtu ambaye hashauriki? Kwa akili unashinda kuelewa kuna mtu analipwa mshahara kwa kodi kazi yake kumshauri raisi anakula mshahara bure.
 
TUNDU LISSU NDO KIGEUGEU KABISA HANA AKILI
MAMBO YA TAIFA ANALETA UCHAMA
PUMBAVU KABISA
ACHA UJINGA TUNDULISU NA CHADEMA KIUJUMLA
NYIE NI MAJAMBAZI AMBAO HAMJAPEWA BUNDUKI
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Hashauriki, hapangiwi na hajaribiwi.
 
CHADEMA MMEPOTEZA UELEKEO
Tundu hayo unayoyatetea kwa maslahi ya nani,utadai mikataba ndio inayolinda yote hayo ,je mbona tuna mikataba mingi mibovu iliyotiwa saini kwa njia za rushwa kwa hiyo tuache tu kwa kuwa akina Kafumu waliruhusu,kwa mpango huu nashukuru Mungu ,Chadema mtaiona tu ikulu ,zamani mlijipambanua kama watetea haki na maslahi ya nchi ,siku hizi Chadema inateteta kila aina ya uozo,ufisadi.Chadema mshakuwa chama cha hovyo kabisa.
Tatizo siyo nyie tatizo ni akili zenu "
Hawa wa upinzani si walipiga kelele kabla nchi inapoteza pesa, sasa haya wanayoyaongelea now je waliwahi kupendekeza bungeni kabla!?
Lisu anapoteza mwelekeo japo mkulu kapotea zaidi


CHADEMA WAMEPOTEZA UELEKEO
HAWAONGEI KWA FAIDA YA NCHI
WANAPINGA MAZURI YA SERIKALI
PUMBAVU KABISA
 
Binafsi sioni kosa la Lissu, ameeleza ni nini Rais alipaswa kufanya kabla ya kuzuia mchanga kusafirishwa.. Magufuli ana nia nzuri lakini njia anazotumia zinaweza zikaliingizia taifa hasara zaidi badala ya faida kwa sababu ya mikataba iliyoingiwa na serikali zilizopita na wawekezaji hawa..
Tusiwe mashabiki wa watu, tuwe mashabiki wa ukweli.. Tanzania ni yetu sote
Anatumia mbinu za kibashite bashite. Mara ooh yumo kjgogo kwenye orodha
 
Hotuba ya jana ya Rais Magufuli ni ushahidi mwingine, kama bado kuna shaka, ya rule of state lawlessness ambayo mtukufu anatuingiza kama taifa. Natumia marufuku yake ya kusafirisha mchanga wenye madini nje ya nchi kama mfano.

Zaidi ya dhahabu, mgodi wa Bulyanhulu unazalisha pia madini ya fedha (silver), cobalt, copper na cadmium (ya mwisho kama sikosei!). Bulyanhulu ni mgodi pekee nchini wenye madini yote hayo na mchanga unaosafirishwa nje unatoka Bulyanhulu. Madini yote hayo, kwa mujibu wa Sheria ya Madini na Mikataba ya Uendelezaji Madini (MDAs) waliyopewa na Rais Ben Mkapa na kurudiwa na Jakaya Kikwete, ni mali ya wawekezaji.

Mgodi wa Bulyanhulu unafanya smelting ya dhahabu tu (takriban 70% ya processing yote). 30% iliyobaki inafanyikia Japan ambayo ina hiyo capacity ya smelting ya hayo madini mengine.

Ndio maana mchanga huo umekuwa unasafirishwa kwenda Japan tangu 2001. Sasa a smart president angewaelekeza wawekezaji wajenge kwanza hiyo capacity ya smelting ndani ya nchi kabla ya kupiga marufuku export ya mchanga. Kwa kuzingatia kwamba wawekezaji hawa wanalindwa kisheria na kimkataba, a smart president would've renegotiated the MDAs or changed the relevant law ili kufanya processing yote ifanyike internally.

Badala ya a smart president, tuna JPM anayeamini kwamba ametumwa na Mungu kuinyoosha nchi hii na neno lake ndio sheria. Matokeo yake, atagombana na wawekezaji na serikali zao na mabwana wakubwa wa kifedha duniani ambao ndio wamiliki halisi wa rasilmali zetu.

Watampeleka kwenye arbitral tribunals za kimataifa ambazo Mkapa na Kikwete walizikubali kuwa ndio mahakama za migogoro kati yetu na hao tuliowapa rasilmali zetu. Na tukipelekwa huko hatuponi kwa sababu tutakuwa tumevunja mikataba na sheria zinazolinda wawekezaji. More importantly, hatapata hicho anachokifikiria, i.e. internal capacity ya mineral processing yote kwa sababu we simply don't have that capacity currently.

Na, kwa taarifa ya wale wasiojua mambo haya, huo mchanga unaosafirishwa nje sio magwangala. Magwangala ni rock waste yanayotupwa pembeni ya migodi baada ya dhahabu kutolewa. Yana madini kiasi kidogo sana ambayo sio commercially viable kwa wawekezaji kuyavuna. Hayo ndio madini Magufuli 'aliyowagawia' wananchi jana. Ni makapi yanayoachwa nyuma baada ya karamu ya wawekezaji. Hiyo, kwa busara za John Pombe Magufuli, ndio stahili ya waTanzania waliomchagua.

Evo Morales wa Bolivia alikuwa na mikataba kama ya kwetu alipochaguliwa in December ya 2006. Cha kwanza alichofanya ni kuiondoa Bolivia kwenye MIGA Convention na kwenye bilateral investment treaties (BITs) zilizokuwa zinalazimisha international arbitration kwenye migogoro ya uwezekaji. Baada ya hapo ndio akabadilisha sheria na mikataba ya uwekezaji iliyoipa Bolivia sehemu kubwa ya umilikaji wa gesi na mafuta ya nchi yake. Of course, Morales is a Bolivarian na rafiki wa Castro, marehemu Hugo Chavez na wakushoto wengine. Magufuli is none of the above. He's a proto-fascist who believes in nothing but violent state power.

TUNDU LISSU
Mwanasheria mkuu
CHADEMA

Huoni aibu kuandika hayo uliyoyaandika kwenye nyekundu hapo?
 
Hawa wa upinzani si walipiga kelele kabla nchi inapoteza pesa, sasa haya wanayoyaongelea now je waliwahi kupendekeza bungeni kabla!?
Bunge gani? Bunge hili la Tulia? Thubutu yako!! Tulia akikalia kiti cha speaker anajiona yeye =mungu =bashite. Acha muisome namba
 
67 Reactions
Reply
Back
Top Bottom