Lissu hategemei huruma, lakini Ni laIazima atapata kura nyingi za huruma

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,115
33,077
Ni ukweli usiopingika kuwa Sehemu mbalimbali duniani kunapofanyika kampeni kwa ajili ya Uchaguzi sio kila mtu anasikiliza au anafuata Sera za Mgombea,hapana.

Ni hulka ya binadamu kuwa na utashi,maana yake kila mtu Ana utashi wake.

Hivyo katika muktadha wa Uchaguzi hufanyika kampeni sio watu wote hufuatilia kampeni,Bali watu tayari hua na maamuzi Yao mioyoni bila. Hata kushawishiwa.

Hivyo Basi Kuna watu huangalia Haiba ya mgombea, kwa mfano wengine humchagua mgombea kwa sababu tu Ni Mzuri wa sura(handsome) nina mifano hai juu ya hili,wanawake wengi na baadhi ya wanaume na vijana Marekani humchagua mgombea hata kwa sura.

Maraisi waliofaidika na kura za Aina hii Ni Bill Clinton na Barack Obama,lakini pia kwa Tanzania Ni Jakaya Kikwete.

Sasa Basi katika wapiga kura wengi Ni wanawake,kwa asili wanawake Ni viumbe wenye huruma,upendo na sononeko au maumivu ya ndani kwa ndani, na hii Ni kwa sababu wao ndio hukaa mda mwingi na mtoto,kuanzia tumboni hadi duniani.

Hivyo Basi sio siri ijapokua Tundu Lissu hategemei kura za huruma kwa sababu jamaa Ni nguli wa kujenga hoja kuongea,kujieleza,kujitetea na kushawishi Ni lazima tutaketusitake wanawake wengi Sana watampigia kura za huruma tu kutokana na kunusulika kwake na kifo.kwakitendo alichofanyiwa Cha kupigwa risasi Ni wanawake wachache Sana waliofurahia hata wa CCM.

Lissu anazo kura za huruma hata kutoka kwa wanaume,ingawa akianza kujenga hoja watu wataweza kumwacha mgombea wao na kumpigia Lissu.
 
Umeanza kurukaruka kama maharage kwenye sufuria?
Kataka wembe mwenyewe wacha umkate
Mmeona watu wachache kwenye maandamano yenu mmeanza eti watu wamemuweka moyoni tu watampigia?
Poleni sana.
 
Umeanza kurukaruka kama maharage kwenye sufuria?
Kataka wembe mwenyewe wacha umkate
Mmeona watu wachache kwenye maandamano yenu mmeanza eti watu wamemuweka moyoni tu watampigia?
Poleni sana.
Alaa kumbe Yale yalikua maandano eeeh.

Uvccm bana.
 
Amini amini nakwambia, Tundu Antipas Lissu ndo Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania hapo October 2020.
 
Hiyo ni lazima kwani kitendo alichofanyiwa hakikubaliki kwa kila mwananchi asiye taka mambo ya kishetani
 
Wenye huruma kwa Lissu hawajajiandikisha so hawatamsaidia kwa lolote.
 
Hiyo ni lazima kwani kitendo alichofanyiwa hakikubaliki kwa kila mwananchi asiye taka mambo ya kishetani
Wamama wengi Sana wa CCM watampigia kura nakuambai.
Katika siasa kuna watu

Wanaoaikiliza Sera
Wasiojali mambo ya sera,Hawa wanataka mabdiliko tu,Mimi mmojawapo,Hawa ndio husema kuchagua CCM na gogo watachagua gogo,

Kuna wanaoangalia Haiba,

Na kwa madhira aliyopitia Lissu wapo watakaompigia kura kwa huruma,huwezi kudharau hili, hata watu wa mfumo wanalijua na wanajuta sana kwa hili.
 
Back
Top Bottom