Lissu: Hakuna upelelezi unaoendelea kuhusu shambulio dhidi yangu; Ndugai adai vurugu zilimzuia kwenda Nairobi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Rais wa TLS na Mbunge wa Singida Mashariki, Mh. Tundu Lissu anahojiwa na Azam Two wakati huu.

Nakuletea kuanzia nilipoikuta interview hii


======
UPDATES:

Lissu:
Nimepigwa risasi 16 na bado napumua. Naona Mungu ameamua niishi.

Natambua jitihada za madaktari na wauguzi wa Dodoma hospital, pia nawashukuru wa Nairobi hospital.

Katika miaka yangu zaidi ya 50 sijawahi kuona madaktari, wafanyakazi na wauguzi wazuri kama wa Nairobi Hospital. Tumekuwa na kasumba ya kufikiria mambo yote wanajua wazungu lakini hawa wahudumu wa hapa wana huduma nzuri na sijaona mzungu yeyote kati yao.

Swali: Je tangu uliposhambuliwa hadi kupelekwa hospitali ulikuwa na fahamu?

Lissu: Nilikuwa na fahamu muda wote ninapopelekwa hospitali. Nakumbuka kumwambia dereva ampigie Mwenyekiti na Msigwa. Nilipofika hospitali niliwaona wabunge waliokuwa pale na niliwatambua. Nilitaka wanikalishe kitako maana nilikuwa na maumivu sana.

Swali: Ni lini ulikuja kutambua kuwa uko hapa Nairobi hospital?

Lissu: Nilikuja kujua niko Nairobi hospital tarehe 14 Septemba.

Kuna watu wananiambia walikuja kuniona na nilitikisa kichwa nilipowaona lakini baadhi siwakumbuki. Nilimtambua Mzee Jaji Chande Othman alipokuja. Viongozi wa Kenya waliokuja nakumbuka kuwaona pia.

Hivi sasa sina uhitaji wa daktari. Nauguzwa na manesi na mamama cheza wangu wa viungo 'wanaoniliza' kila siku lakini kila siku naamshwa na daktari. Wana upendo sana na wanasema mimi ni mgonjwa wao.

Nadhani sitakosea kusema hii ni hospitali bora kwa Afrika Mashariki na Kati. Hapa nilipo niko Presidential Suite ya hospitali hii, wenzetu hawapeleki viongozi wao nje.

Swali: Hadi sasa umefanyiwa operesheni ngapi?

Lissu: Hadi sasa nimefanyiwa operesheni 17, ya juzi kati hapa ilikuwa ya 17. Kuhusu maumivu ya operesheni siwezi kuyasikia sana maana operesheni unakuwa huna fahamu.

Wiki ya kwanza baada ya kuamka nilikuwa na maumivu makali sana. Sijawahi kusikia maumivu kama yale maishani mwangu. Ila sasa sina maumivu yoyote.

Swali: Hapa mkononi naona una kovu, je ni la kabla au baada ya shambulio?

Lissu: Hapa mkononi (anaonesha mshono wa mkono wa kulia) ilipigwa risasi na madaktari wanasema risasi zilichakaza mfupa kabisa hivyo umeungwa na chuma.

Mkono wa kushoto haunyooki zaidi ya hapa maana kwenye kiwiko kuna vyuma.

Huu mguu niliouweka juu(wa kulia) ulipigwa kwenye nyonga hadi goti. Umeshikiliwa na vyuma. Madaktari wanasema kwenye goti pakishikilia sawa sawa basi nimepona. Wananifanyisha mazoezi ya kukunja na kukunjua(yanauma kwelikweli).

Mguu wa kushoto uko vizuri kabisa naweza hata kucheza mziki.

Nyuma ya goti la kulia kulikuwa hakuna nyama kabisa baada ya kupigwa risasi. Imebidi watoe nyama na ngozi sehemu nyingine za mguu ili kurudishia.

Swali: Unavyoonekana una nafuu na unaendelea kupona. Mbona kuna taarifa kuwa unapelekwa nje ya Nairobi kwa matibabu zaidi?

Lissu: Hiki kitendo kiliwakera watu wengi hasa marafiki zetu wa nje na wameomba nikitoka hapa niende kwenye hospitali zao wakanicheki na kunifanyisha mazoezi ili nikirudi nchini niwe salama.

Swali: Hadi sasa gharama kiasi gani zimetumika kukuuguza?

Lissu: Siwezi kusema kiasi exactly lakini ukweli ni kwamba mpaka sasa mamilioni mengi ya shilingi yameshatumika kunitibu.

Swali: Mara tu baada ya shambulio lako kulikuwa na Utaratibu wa kuchanga kwa wananchi lakini kwa sasa kama umepungua nguvu au umezorota, kwanini?

Lissu: Utaratibu haujaisha kabisa bali umezorota. Na hii ni sababu Bunge lilisema kuwa litagharamia matibabu yangu. Kwa hali ilivyo sasa, wananchi waliona wamepata ahueni. Lakini hadi sasa Bunge halijatoa hata senti 1.

Swali: Familia yako inazungumziaje?

Lissu: Familia yangu inasema tangu Septemba 7, Spika wala Naibu wake wala Tume ya huduma ya wabunge hawajaja kuniona ilhali mimi ni mbunge halali.

Swali: Zile fedha zilizochangwa na cheki kuoneshwa na hospitali kusema imepokea zilikuwa fedha zipi?

Lissu: Zile ni fedha za michango binafsi ya wabunge. Ni nusu ya posho ya siku ya wabunge.

Ndugu yangu alikuwa na hapa kwa mashauriano na tukajadili tunafanyaje maana Bunge halijasema halitochangia lakini hawajatoa pesa hizo.

Swali: Umewahi ongea na Spika kirafiki?

Lissu: Mimi sijaongea nae kirafiki maana mimi siombi fadhila. Ndugu yangu msemaji wa familia ni wakili na amewaandikia procedure za kisheria lakini hawatoa stahiki zangu hadi sasa.

Swali: Ulichukuliaje ujio wa Makamu wa Rais na Mzee Mwinyi?

Lissu: Makamu wa Rais kunitembelea ilinipa faraja. Hakuna mgonjwa asiyependa faraja. Nimefurahishwa na ujio wake na aliniambia Rais amesema nije nikuone. Nikamwambia amshukuru Rais kwa niaba yangu.

Mzee Mwinyi kuja pia nilishukuru sana. Kwa umri wake kujitoa kuja kuniona inapendeza.

Nashukuru pia amekuja Mzee Warioba.

Kuna mama alikuja toka Iringa. Kwa kumwangalia atakuwa anatoka Iringa kijijini na alikuja hapa akasema ametembea siku 5 kuja kuniombea. Akaniombea na kuondoka zake.

Nimegundua watu wana upendo mkuu. Sijui nitaulipaje.

Swali: Hadi sasa hakuna aliyekamatwa, unalizungumziaje?

Lissu: Hajakamatwa mtu sababu hakuna upelelezi unaofanyika. Kama aliyefanya tukio kakimbia, mtu wa kwanza kuhojiwa inatakiwa iwe mimi.

Juzi hapa nimesikia Askari wa Interpol walisema wanataka kunihoji. Mimi ni mwanasheria, najua hawana uwezo huo. Natakiwa kuhojiwa na askari wa Kenya baada ya kuombwa na Jaji Mkuu wa Tanzania.

Swali: Jeshi la Polisi lilitaka kumhoji dereva wako lakini Uongozi wa CHADEMA ukasema yuko huku kimatibabu. Je lini ataenda kuhojiwa? Na je bado anaendelea na matibabu au ameamua kubaki huku?

Lissu: Dereva wangu ameniendesha miaka 15, nilitendewa tukio nikiwa nae na nitahojiwa nikiwa nae. Niko nae Nairobi Hospital, nalala nae hapa na nikipona nitarudi nae Tanzania.

Swali: Je unadhani utarejea kwenye umachachari wako?

Lissu: Je wewe una mashaka na hilo?

Mtangazaji: Nataka uuthibitishie umma

Lissu: Ishu ni huu mwili tu kupona, ukishapona nitarejea Tanzania. Madaktari wangu wamesema nitasimama tena.

Swali: Miezi 3 uliyokuwa huku kumekuwa na hama hama ya wanasiasa. Je huu ni uelekeo wa upinzani kufa?

Lissu: Watu wanajisahaulisha tu historia ya vyama vingi. Uhamiaji wa watu kwenda CCM ulianza zamani. Walihama na CHADEMA haijafa.

Swali: Unadhani nini kinatokea watu hawa kuhama. Unadhani sababu ni nini?

Lissu: Njaa, Tamaa, Kuchoka tu.

Swali: Je katika kazi zako, ni ipi unaikumbuka kuliko zote?

Lissu: Hakuna kazi ninayoimiss kama kazi ya Ubunge hasa nikiwa Bungeni. Nijiandae, nisome ili nikiongea watanzania wasikie nikiwatetea. Kulala kitandani miezi 3 ni ngumu kwangu. Na mtu akisema hii ni kutafuta kiki kwakweli hanifahamu au akili yake haiko vizuri.

Baada ya mahojiano na Lissu, Azam TV walimhoji Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Job Ndugai ili kupata upande wake

Mtangazaji: Natumai Spika umemsikiliza Mh. Lissu na kumuona.

Ndugai: Nimemsikiliza Lissu na nashukuru sana kuwa anapewa huduma nzuri Nairobi.

Swali: Baada ya Lissu kushambuliwa, kulikuwa na mvutano kati ya Bunge na Chama kuhusu wapi akatibiwe. Ilikuwaje?

Ndugai: Haikuwa mvutano bali suala la utaratibu. Alitakiwa apelekwe Muhimbili. Lakini familia na Kambi ya Upinzani bungeni waliopt aende Nairobi.

Haukuwa mvutano bali hali ya mawazo tofauti.

Swali: Amesema kaka yake mkubwa amekuwa akifuatilia stahiki zake Bungeni na kumekuwa na mvutano. Iko vipi?

Ndugai: Hakuna mvutano. Nishawahi kukaa na watu 3 toka familia yake na tulielewana vizuri na hadi sasa kuna mawasiliano kati yetu ili kuweka mambo vizuri.

Kwa sasa huwezi sema kuna kutoelewana. Lissu yuko Kitandani mambo yanampita hivyo labda ana mawazo hayo.

Swali: Lissu alionesha masikitiko hajakuona wala Naibu wala Tume ya huduma za Bunge kule Nairobi. Vipi mbona hamjamjulia hali?

Ndugai: Wabunge wanaougua na kupelekwa nje ni wengi na tunawatibu kimya kimya. Lissu katembelewa na wabunge wengi na hadi viongozi wa kitaifa. Hakuna mbunge aliyeumwa na kulazwa nje ya nchi na kutembelewa kama yeye.

Kuhusu mimi mwenyewe, muda si mrefu nitaenda Nairobi. Sikuweza fanya hivyo sababu ya hali ya kisiasa Kenya ila sasa nitaenda.

Vilevile Mbowe, Msigwa ni wajumbe wa Tume ya huduma ya Bunge na walikuwa huko muda mrefu na nilituma wabunge 2 huko kumjulia hali. Kama nilivyosema yeye ni mgonjwa hivyo labda mengine yanampita.

Pia tuna balozi wetu Nairobi anayemjulia hali.

Swali: Nini kinaweka ugumu kwa hili suala la Lissu kupata stahiki zake?

Ndugai: Ndani ya Serikali kuna ukiritimba. Ni jambo la kawaida Serikalini. Mchakato ukikamilika mambo yakikaa vizuri au yasipokaa vizuri tutajua.

Pia ukiritimba unazidi kwa suala lake sababu alipelekwa nje bila rufaa toka Muhimbili hivyo makaratasi ya rufaa yale yamekosekana. Haijawahi tokea hvyo hili ni jambo jipya inabidi msingi ujengwe kwa ajili ya cases zijazo kama hii.

Swali: Lissu ana mpango wa kwenda kutibiwa nje ya Nairobi. Je na huko mtagharamia?

Ndugai: Hili suala ni gumu sana. Najua atapelekwa nje, na watakaogharamia walishaongea na sisi na hivyo sisi tutawasiliana nao kuona kipi kitalipiwa na labda tutacover vile vitakavyobaki.

MWISHO!
 
Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu yupo muda huu Azam anahojiwa akiwa Nairobi Hospital.

=============
UPDATES
=============

Tundu Lissu: Nikisimama nikatembea tena Nitarudi Tanzania kuendeleza mapambano

Tundu Lissu: "Nilikuwa nina jitambua mpaka muda nafikishwa Hospitali ya Dodoma, na mtu wa kwanza kumpigia simu alikuwa ni Mwenyekiti wangu, Freeman Mbowe. Dereva wangu alinisaidia kuwasiliana na watu hawa."

Tundu Lissu: "Nisingefika Nairobi bila msaada wa kwanza wa Madaktari wa Dodoma, nilipofika Nairobi Hospital madaktari walifanya kazi kubwa sana kunitibu hadi kufikia hapa nilipo leo."

Tundu Lissu: "Risasi 16 zimetolewa mwilini mwangu tangu nimefika hapa Hospitali ya Nairobi, risasi moja bado ipo mwilini mwangu na risasi zingine 16 zilinikosa siku hiyo ya tukio."

Tundu Lissu: Walionipiga risasi niliwaona lakini siwafahamu.

Tundu Lissu: Mpaka sasa tunapoongea, Bunge halijatoa hata senti moja kwa ajili ya matibabu. Hakuna afisa wa Bunge yeyote aliyekuja kuniona tangu Septemba 7, 2017. Si Spika, Naibu Spika wala Katibu wa Bunge.

Tundu Lissu: "Chadema haiwezi kufa, hao walioondoka waondoke tu wala hatuteteleki, tupo imara. Niwahakikishie Watanzania, sitarudi nyuma, nikipona nitaendelea na kazi yangu. Ninaupenda sana Ubunge."

Mnaweza kufutilia live mahojiano hayo AzamTV
 
Tundu Lissu: "Risasi 16 zimetolewa mwilini mwangu tangu nimefika hapa Hospitali ya Nairobi, risasi moja bado ipo mwilini mwangu na risasi zingine 16 zilinikosa siku hiyo ya tukio."
 
Back
Top Bottom