Lissu azuru Kenya, asema hataki wala hajawahi kutaka kuishi uhamishoni

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
34,962
70,472
Haya ameyaongea leo Bwana Tundu Lissu hii leo kupitia chaneli ya KTN Kenya!
Amewashukuru sana wakenya kwa kujitolea kumchangia damu!

VIVA TUNDU!




Baada ya miaka miwili tangu kupigwa risasi, Tundu Lissu amsema amefika Nairobi kwakuwa hali yake ya kiafya imetengemaa, na kwamba madaktari wake wamemwambia sasa ana ruhusa yao ya kwenda nyumbani.

Kuhusu kuvuliwa ubunge

"Watu wengi wanafahamu nilipokuwa tangu tarehe 7 ya Septemba 2017 isipokuwa Spika wa Bunge la Tanzania, yeye hana taarifa kuwa nipo wapi nina hali gani, ninafanya nini. Ndiyo maana kanifuta ubunge."

Kuhusu rufaa dhidi ya kuvuliwa ubunge

"Tayari kuna rufaa mahakamani. Mbunge akiondolewa ubunge wake namna hiyo halafu akanyamaza kwasababu muda umebaki mfupi, maana yake ni kwamba anaweka mfano kwa Spika na watu wengine kwamba, inawezekana kuondoa mbunge usiyemtaka au wabunge usiowataka na kusiwe na madhara yoyote -- kwasababu kama huyu ameachia, na yule ataachia."

"Tumepinga uamuzi wa Spika, mahakama imekataa kuturuhusu, ila tumekata rufaa. Lazima kuwe na msimamo sahihi wa kisheria na kikatiba wa namna ya kushughulikia matatizo ya wabunge ya aina ya yaliyonitokea mimi. Tusipoweka msimamo huo maana yake ni kwamba kutakuwa na mfano (precedence) kwamba kumbe inawezekana kumfuta mbunge ubunge wake kwa Spika kuamua tu. Hiyo siyo sahihi na haitaniumiza mimi tu, bali na wengi wanaokuja."

"Lazima tuwe na namna ya kuamua nani awe na nani asiwe mbunge katika mazingira ya aina hiyo.
Wanaoweza kupima athari za mimi kutokuwepo bungeni siyo mimi, bali ni wale waliyokuwepo kwa kipindi hicho ambacho sikuwepo."

Wapinzani kujiondoa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Chama kilijiandaa na uchaguzi ila wagombea wetu wamefutwa kwa asilimia 96. Katika wagombea zaidi ya 3300 tuliokuwa nao, wamefutwa wagombea zaidi ya 3200 nchi nzima, na wa vyama vingine vilevile.

Sasa ilikuwa ni aidha tukubali kushiriki tukiwa na asilimia 4 tu ya wagombea na kubariki uhuni huu wa kisiasa, au tuwaambie watu na dunia kuwa huu siyo uchaguzi. Hatujawahi kuona kitu cha namna hii katika historia ya nchi yetu.
Tumefikia wakati ambao chama ambacho kipo madarakani karibu miaka 60 kinaogopa hata uchaguzi wa kijiji. Kinaogopa ushindani kwenye uchaguzi wa mtaa.

Maana yake ni nini kwa uchaguzi ujao, mimi nina hofu sana. Kama huu ndiyo utamaduni wao mpya, huko tunapoenda mambo yatakuwa mabaya sana kwa nchi ambayo imekuwa ya amani kama Tanzania.

Yote yanayohusu mimi kupigwa risasi, viongozi wengine kukamatwa na kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara ni utekelezaji wa azma ya Rais Magufuli ya kutokuwepo chama cha upinzani katika uchaguzi wa 2020.

Wakati wa Kikwete tulikuwa tunafanya mazungumzo na serikali na ya kutatuliwa yalitatuliwa. Huyu anatuwinda ili atuue, atufunge, atuumize au anunue wanachama wetu.

Kuhama kwa viongozi wa upinzani

“Siwezi kusema halijatuathiri. Unapopoteza viongozi wako waliochaguliwa katika mazingira magumu kabisa, kama mazingira ya kiuchaguzi ya Tanzania, alafu wanajiuza kirahisi namna hiyo, lazima unaathirika”

Utayari wa kuwania Urais 2020

“Kama chama changu na vyama rafiki vitaona ninafaa kuwa rais, nipo tayari kuitikia wito huo”

Lini anarudi nyumbani?

“Hali ya usalama wangu bado siyo nzuri. Watu hawataki kuona nikirudi alafu kesho yake nipigwe risasi tena”

“Katika hali hii lazima watu wenye busara wakae na waone namna ya mimi kurudi nyumbani niendelee na shughuli zangu, lakini usalama wangu ukihakikishwa.”

“Katika hali hii lazima watu wenye busara wakae na waone namna ya mimi kurudi nyumbani niendelee na shughuli zangu, lakini usalama wangu ukihakikishwa.”

“Mimi sitaki wala sijawahi kutaka kuishi uhamishoni. Sipo Uhamishoni.”

"Nimewasiliana na taasisi mbalimbali ulimwengu ya kuhakikisha tunatengeneza mazingira salama ya mimi kurudi nyumbani."

Awashukuru Wakenya

“Nawashukuru Wakenya kwa kunichangia damu. Mimi ni Mkenya. Inawezekana sina tu passport ya Kenya lakini nina damu ya Wakenya waliyonipa nilipoletwa hapa”
 
Kabla ya kuwaza urais, wapinzani wanapaswa kutafuta namna ya kudeal na hawa wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wakurugenzi wa Halmashauri na wanachama hai kabisa wa CCM. Otherwise ni kujidanganya na kutupotezea muda sisi wapiga kura.

I also think wapinzani wanalitambua hili vizuri sana ila nguvu ya ruzuku inawasukuma kuendelea na uchaguzi tu ili kutimiza wajibu. Siasa kwao ni ajira za kudumu.
 
Kumbe mnashindana hahaha hiyo timing ni coincidence au?, kuna watu maisha magumu sana aisee, naona walipoona P.Kabudi kapewa steji na kujadiliwa huko Kenya hawakulala, sasa unashindana na mtu hata asiyejua wala kujali kama wewe ni mshindani wake? I mean Kabudi sidhani hata kama anajua mnashindana naye, yeye yuko kazini na wala hashindani mtu, kujitesa tu buree!
 
Kumbe anashindana hahaha hii ni coincidence au?, huyu jamaa ana maisha magumu sana, naona alipoona P.Kabudi kapewa steji na kujadiliwa huko Kenya hakulala, sasa unashindana na mtu hata asiyejua wala kujali kama wewe ni mshindani wake? I mean Kabudi does not care about you, yeye yuko kazini na wala hashindani na wala hata siajabu hajui kama kuna mtu anashindana naye, kujitesa tu buree!
Kabudi siyo size ya Tundu Lissu. Usilazimishe kumpadisha hadhi mtu wa jalalani.
 
Kabudi siyo size ya Tundu Lissu. Usilazimishe kumpadisha hadhi mtu wa jalalani.


Hata mimi nashangaa sasa kuna haja gani ya kushindana? I mean P.Kabudi wala hata hajui kama mnashindana naye kwanza.
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Back
Top Bottom