Lissu awalipua mawaziri, wabunge kwa unafiki wao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii

Status
Not open for further replies.
zulma zinafanywa sana juu ya wafanyakazi wa taifa hili,na sijui kama wafanyakazi wanalijua hili jambo la kuzulumiwa na mifuko hii ya jamii.
 
Siasa za kujenga jina kwa mambo ya uongo kama kweli yuko sawa kwa nini asiweke majina hapa hii tabia ya kuongea vitu hewa bila kutaja majina ni jambo la kihuni huwezi kusema yote haya bila kututajia wahusika ni kudanganya watu ili uonekane mzuri.

dah inatia uchungu sana hii,, yaaani unabisha kila kitu kinachoikosoa CCM na serikali, inaonekana hata siku uliyoambiwa MWALIMU NYERERE amekufa wewe ulibisha.... inaonekana hata tukikwambia kuna ghorofa la mhindi linajengwa pale UVCCM nyuma utabisha tu....

wazazi, dada, kaka, baba zetu ambao ni walimu huchangia sana hii mifuko.... wananaufaikaje??
madaktari, manesi,polisi,, wanajeshi, wananufaika nini na hii mifuko?
wafanyakazi wa sekta mbalimbali ambao huchangia pia wananufaikaje na hii mifuko??

NSSF imejenga nyumba sehemu mbalimbali za nchi hii, je hizo nyumba huyu mwalimu na mfanyakazi wamenufaikaje?
kwa mfanyakazi aliyefanya kazi miaka 30 akastaafu, unajua riba ni kiasi gani??
Miradi wanayofanya NSSF na hizi hela zetu nani ananufaika???
Unajua skendo ya MANJI na NSSF?, Iliishia wapi?? inamaana ile hela yetu ndio ilipotea hivihivi???
kwa nini wateja wa nssf wasikopeshwe hizi nyumba kwa dhamana ya hela zao??? na wakawa wanakatwa kwenye mishahara yao??
unajua bei ndogo kabisa ya zile nyumba kigamboni ni MIL46 tena vyumba viwili, na sio mkopo, mwalimu gani mwenye hiyo CASH? na nyingine zinauzwa mpaka mil120, je ni kweli tunamthamini mwananchi mzalendo na hizi bei, au ndio za kina fulani??

tuwe na huruma basi kwa hawa wazalendo wanaoteseka, tuwasaidie basi hata kusema na sio kuwa wanafiki kwa kushabikia vitendo viovu wanavyofaidika navyo wanaume wenzako na familia zao.....
 
Lissu ni mropokaji, anaongoza kwa siasa za matusi.

inapendeza sana hii,, " ukweli kwenu huwa ni matusi makubwa saana" kwani alichoongea TL sio kweli, mara ngapi haya husemwa, sakata la MANJI,QUALITY GROUP na NSSF ni uongo ule au nalo tusi??, dowans ni uongo au nalo tusi, kagoda ni uongo au nalo ni tusi??? marehemu BALALI na BOT yake yale ni matusi makubwa eeeeeeh....
Yangekuwa haya hayapo tungesema kweli TL ni mropokaji, ingenguwa NSSF ina faida kwa wazalendo masikini wa nchi hii kweli tungesema TL ni mlopokaji,,, ingekuwa zile nyumba wanazojenga NSSF wanapewa walimu kwa dhamana ya michango yao, na kukatwa kwa riba ndogo sana kwenye mishahara yao tungesema TL ni mlopokaji....

KWELI UKUBWA WA KICHWA SIO WINGI WA AKILI,,, jaribu kutumia mawazo yako kuchangia vitu kama hivi na sio kuchangia kwa kutumia akili za wanaume wenzioooo,,, mjini hapa kaka,, watu huwa wanatabia mbaya shauri yako,, JARIBU KUWA SHAABABI...
 
Kumbe wanaomba fedha kwa maendeleo mm nikajua wanaomba wakanunue mboga za majumban kwao

Sasa kama mifuko wanatoa kwa nini tuwe na wabunge na mfuko wa jimbo?????!!!!!
Mkurugenzi wa wilaya kwa kushirikiana na mfuko husika wangweweza kuendesha tu!!!!!
 
Siasa za kujenga jina kwa mambo ya uongo kama kweli yuko sawa kwa nini asiweke majina hapa hii tabia ya kuongea vitu hewa bila kutaja majina ni jambo la kihuni huwezi kusema yote haya bila kututajia wahusika ni kudanganya watu ili uonekane mzuri.
ata angeataja usingekosa cha kusema.....wallah
 
Kuelekea uchaguzi mkuu tutasikia mengi sana.Taasisi za kifedha ziwe makini dhidi ya wanasiasa wanaotaka kujipatia fedha kwaajili ya kampeni za uchaguzi mkuu.Taarifa zitolewe na zisambae kwa haraka ili kuwasaidia wapiga kura kuweza kuwaangusha kupitia masanduku ya kura.
 
Wanachama wa chadema jitahidini kukifanya chama kuwa Tass nasio maliyawatu -3 siokila analofanya mbowe na slaa
 
Kwa hiyo haya mashetani yamefikia kutafuna viinua mgongo vyetu! bila kuzipiga hakuna heshima hapa!
 
Siasa za kujenga jina
kwa mambo ya uongo kama kweli yuko sawa kwa nini asiweke majina hapa hii
tabia ya kuongea vitu hewa bila kutaja majina ni jambo la kihuni huwezi
kusema yote haya bila kututajia wahusika ni kudanganya watu ili
uonekane mzuri.

kweli tupu, anataka iundwe tume nae akapige hela, mbona kafulila alitaja, sasa ninachomfanya amumunye ni nini kama sio unafiki.
 
tatizo kubwa ni kwamba ccm imeweka mizizi yake kwenye sehemu zote nyeti wakati haya mambo yanafanyika tuna vyama vya wafanyakazi ambavyo pia vina wawakilishi kwenye mifuko ya hifadhi wako kimya nimeshangaa kusikia nssf itatoa pesa kwa ajili ya kujenga ofisi za wabunge majimboni
nani kawapa kibali wabunge cha kuchota pesa za wafanyakazi lakini kila siku tunasikia wakina Mgaya wako kimya duniani kote ukigusa pesa za wafanyakazi ndio mwisho wa utawala uliopo madarakani lakini huku wanavyochezea pesa za wafanyakazi inasikitisha
tunahitaji vyama huru vya wafanyakazi,wakulima na wafanyabiashara
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom