Kaazi kweli kweli. Mpaka ifike 2015. Legitimacy ya CCMABWEPANDE itakuwa 0 hakutakuweko na sababu ya uchaguzi. Yule kiazi mwanasharia mkuu aliweza kujibu kitu kweli!!! he he!!! Wanachowaza ni kuvizia na kuteka na kupeleka MABWEPANDE yameamua kuwa majambazi hayana kitu tena,Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, (Chadema), amesema kitendo cha wabunge wameteuliwa kuwa wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kuendelea kuruhusiwa kushiriki katika vikao vya Bunge ni kinyume cha Katiba.
Lissu ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi bungeni, alitoa kauli hiyo, wakati alipokuwa akiulizwa maswali ya papo kwa papo bungeni mjini Dodoma jana.
Alisema Katiba inakataza mtu ambaye ni afisa mwandamizi katika utumishi wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano kuwa mbunge ama inamnyanga sifa yule ambaye ameteuliwa kuwa afisa mwandamizi kwenye utumishi wa serikali kuendelea kuwa mbunge.
Alisema kuna wakuu wa wilaya na mikoa ambao wamechaguliwa wakiwa wabunge na kwa hiyo wananyanganywa sifa za kuendelea kuwa wabunge.
Alihoji kwa nini serikali inaendelea kuwaruhusu wakuu wa mikoa na wilaya hao kuendelea kuja bungeni wakati ni maofisa wa serikali.
Akijibu Pinda, alisema hana uhakika na linalosemwa kama ndio lilivyo. Lakini kama ndivyo lilivyo bahati nzuri Mwanasheria Mkuu wa Serikali yupo hapa analisikia atalifanyia kazi.
Hivi hapa lisiloeleweka ni nini ?
Tunaweza kujitungia sheria au kanuni halafu tushindwe kuzifuata, lakini sheria mama kama katiba! Inatisha!
Uelewa wa viongozi wa ccm na washauri wao ni mdogo mno... !! ni wavivu na wadhaifu katika mambo ya muhimu.
Mwanasheria mkuu wa serikali ya ccm sijui atakuja na maelezo gani hapo!!
Hivi hapa lisiloeleweka ni nini ?
Tunaweza kujitungia sheria au kanuni halafu tushindwe kuzifuata, lakini sheria mama kama katiba! Inatisha!
66. (3) Where a Regional Commissioner is elected a Member of Parliament representing a constituency or where a Member of Parliament representing a constituency is appointed a Regional Commissioner, the National Assembly shall be deemed to consist of the requisite number of members and its proceedings shall be valid notwithstanding that the ordinary total number of members in terms of this Article shall have been reduced by reason of such election of the Regional Commissioner or such appointment of a constituency member.