Lissu atafungua mashauri mbele ya ICC kuchunguza shambulio lake

Yericko Nyerere

Verified Member
Dec 22, 2010
16,782
2,000
Awali wiki hii nilisikia fununu nzuri kutoka viunga vya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya Ubinadamu, ni nzuri kwakuwa Tanzania ni mwanachama wa Mahakama hiyo yenye makazi ya kudumu mjini The Hague

Fununu hizi zikanilazimu kurejea nyaraka zote za ICC zinazoweza kumruhusu Mh Lissu kufungua mashauri hayo mbele yake, na nimejiridhisha bila kuacha chembe kwamba Lissu anaweza kufungua mashauri hayo na yakakubalika na haki ikatendeka kwake.

Kwanza ifahamike kuwa mahakama hii inashughulikia kesi za aina kuu nne,

Article 5
Crimes within the jurisdiction of the Court
1. The jurisdiction of the Court shall be limited to the most serious crimes of concern
to the international community as a whole. The Court has jurisdiction in
accordance with this Statute with respect to the following crimes:
(a) The crime of genocide;
(b) Crimes against humanity;
(c) War crimes;
(d) The crime of aggression.
2. The Court shall exercise jurisdiction over the crime of aggression once a provision
is adopted in accordance with articles 121 and 123 defining the crime and setting
out the conditions under which the Court shall exercise jurisdiction with respect to
this crime. Such a provision shall be consistent with the relevant provisions of the

Katika mchanganuo, kwenye kesi ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kifungu (b) Crimes against humanity) kuna mambo kadhaa, ambayo yameelezwa na mahakama hiyo, ambayo ni kwamjibu wa Article 7
Crimes against humanity

1. For the purpose of this Statute, ‘crime against humanity’ means any of the
following acts when committed as part of a widespread or systematic attack
directed against any civilian population, with knowledge of the attack:
(a) Murder;
(b) Extermination;
(c) Enslavement;
(d) Deportation or forcible transfer of population;
(e) Imprisonment or other severe deprivation of physical liberty in violation of
fundamental rules of international law;
(f) Torture;
(g) Rape, sexual slavery, enforced prostitution, forced pregnancy, enforced
sterilization, or any other form of sexual violence of comparable gravity;
(h) Persecution against any identifiable group or collectivity on political,
racial, national, ethnic, cultural, religious, gender as defined in paragraph
3, or other grounds that are universally recognized as impermissible under
international law, in connection with any act referred to in this paragraph
or any crime within the jurisdiction of the Court;
(i) Enforced disappearance of persons;
(j) The crime of apartheid;
(k) Other inhumane acts of a similar character intentionally causing great
suffering, or serious injury to body or to mental or physical health.

2. For the purpose of paragraph 1:
(a) ‘Attack directed against any civilian population’ means a course of conduct
involving the multiple commission of acts referred to in paragraph 1
against any civilian population, pursuant to or in furtherance of a State or
organizational policy to commit such attack;
(b) ‘Extermination’ includes the intentional infliction of conditions of life,
inter alia the deprivation of access to food and medicine, calculated to
bring about the destruction of part of a population;
(c) ‘Enslavement’ means the exercise of any or all of the powers attaching to
the right of ownership over a person and includes the exercise of such
power in the course of trafficking in persons, in particular women and
children;
(d) ‘Deportation or forcible transfer of population’ means forced displacement
of the persons concerned by expulsion or other coercive acts from the area
in which they are lawfully present, without grounds permitted under
international law;
(e) ‘Torture’ means the intentional infliction of severe pain or suffering,
whether physical or mental, upon a person in the custody or under the
control of the accused; except that torture shall not include pain or
suffering arising only from, inherent in or incidental to, lawful sanctions;

(f) ‘Forced pregnancy’ means the unlawful confinement of a woman forcibly
made pregnant, with the intent of affecting the ethnic composition of any
population or carrying out other grave violations of international law. This
definition shall not in any way be interpreted as affecting national laws
relating to pregnancy;

(g) ‘Persecution’ means the intentional and severe deprivation of fundamental
rights contrary to international law by reason of the identity of the group
or collectivity;

(h) ‘The crime of apartheid’ means inhumane acts of a character similar to
those referred to in paragraph 1, committed in the context of an
institutionalized regime of systematic oppression and domination by one
racial group over any other racial group or groups and committed with the
intention of maintaining that regime;

(i) ‘Enforced disappearance of persons’ means the arrest, detention or
abduction of persons by, or with the authorization, support or
acquiescence of, a State or a political organization, followed by a refusal to
acknowledge that deprivation of freedom or to give information on the
fate or whereabouts of those persons, with the intention of removing them
from the protection of the law for a prolonged period of time.

Naam, baada yakukufafanulia mambo muhimu yanayofaa kufunguliwa mashauri mbele ya mahakama hiyo, Kuna hatu kadhaa za mtu "binafsi" kufungua kesi mbele ya mahakama hiyo ambayo Tanzania ni mwanachama, lakini inakazia kwakusema (Individuals must submit evidence to Prosecutor).1.State party. 2.Security council. 3.Prosecutor

Na kwa nadharia hii ili Lissu afungue kesi inatakiwa aunganishe matukio yote yaliyotokea nchini ambayo yanasifa za kifunguliwa kesi mbele ya mahakama hiyo yanaangukia kwenye kifungu (b) Crimes against humanity; ambapo kwenye section ndogo inaeleza mambo yanayoweza kufunguliwa kesi hapo ambayo ni mauaji kwamjibu wa kifungu ( (a) Murder;) Utesaji, rejea kifungu ( (f) Torture).

Haya mawili tu yanasifa ya kumruhusu Mh Lissu kufungua mashauri mbele ya mahakama hii, lakini ni lazima aunganishe tukio lake na matukio yote yaliyotokea Tanzania kama vile miili ya watu iliyokuwa ikiokotwa cocobeach, mauaji ya kibiti, kupotea kwa Ben Saanane, Azory, kufungwa kwa Mbowe na Matiko (Mahabusu ya kisiasa ni kifungo rasmi), Mateso makubwa kwa watuhumiwa like Mdude Nyangala na mengine yote, kisha awasilishe ushahidi wa hayo kwanza ndipo mwendesha mashitaka ataitisha wachunguzi kuja Tanzania kubaini ukweli huo, jambo ambalo naamini kwa Chadema na Lissu tayari wanaushahidi wote.

Mwendesha mashitaka wa mahakama ya ICC anayo kinga ya kidunia kuchunguza tukio lolote lenye sifa ya kimahakama katika nchi yoyote ile na kitendo chochote cha kufikiria tu kumzuia ni kukiri kuhusika na uhalifu huo na moja kwa moja utaadhibiwa. Rejea kifungu hiki chini...

(Article 48: Privileges and immunities
1. The Court shall enjoy in the territory of each State Party such privileges and
immunities as are necessary for the fulfilment of its purposes.

2. The judges, the Prosecutor, the Deputy Prosecutors and the Registrar shall, when
engaged on or with respect to the business of the Court, enjoy the same privileges
and immunities as are accorded to heads of diplomatic missions and shall, after
the expiry of their terms of office, continue to be accorded immunity from legal
process of every kind in respect of words spoken or written and acts performed by
them in their official capacity).

Na kwa vyovyote vile nawahakikishia, yeyote aliyehusika na jaribio la mauaji ya Lissu, Mauaji ya Kibiti, Mauaji ya Viroba Cocobeach, Aliyemteka Ben Saanane, Azori Gwanda na mwenyekiti wa Halmashauri kule Kigoma, aliyeamuru Mbowe na wenzake kubambikwa kesi na kufungwa na aliyewatesa watuhumiwa wawapo vituoni na uhalifu uhalifu mwingine, atajulikana na kuwajibishwa yeye binafsi bila kujificha kwenye taasisi, idara au popote. ICC haishughuliki na taasisi yoyote bali mtu binafsi. Wale wenye kinga za kikatiba, ICC haizitambui kinga zenu, utashitakiwa kama mtu binafsi.

Namuona Lissu akilikomboa taifa kama vili ilivyo kwa muujiza uliomponya, kupona kwake ni kupona kwa taifa. Zingatieni Lissu ni mwanasheria na anatoka kwenye familia ya wanasheria, wakati mkiendelea kuwatuma wagonjwa wa akili akina Msukuma, Dokita Molel na waropokaji wengine kumtukana Lissu kuwa oooho anaitukana nchi, mara oooho arudi mara anataka ushoga nk, Dunia inajua kiswahili na matusi yote ya kiswahili yanafahamika, Kwenye ICC kuna kipengele kinachoipa mahakama hiyo nguvu kufuatilia na kujumuisha katika uzito wa mashitaka maneno/vijineno/matusi/vitisho nk ya maafisisa wa serikali dhidi ya mlalamikaji (Lissu), hivyo endeleni huku mkijiandaa kisaikolojia...

Kwamtazamo wangu serikali imechelewa, miezi 13 tangu ashambuliwe Lissu, serikali ilikuwa na nafasi kubwa ya kutanzua mgogoro huu iliouzalisha, kwasasa hakuna njia kwa serikali dunuani hadi mbinguni isipokuwa niia ni moja tu, nayo ni kukiri makosa kwakutosimamia usalama na kuchunguza mambo haya, na ianzishe uchunguzi wa wazi wa kimahakama sio kipolisi, ili kurejesha imani kwa watu na jumuiya ya kimataifa,. Nje ya hapo nawahakikishia 2020 haifiki kuna watu watafikishwa mbele ya ICC na kuwekewa vikwazo amq adhabu, hasa hasa maafisa wa kiserikali ambapo wengi hupokea maagizo tu toka juu na kuyatekeleza, hawa wataathirika zaidi ikiwa ICC itatua nchini.

Na Yericko Nyerere

Ninadhani umekurupuka kusoma hii makala, kwamjibu wa Lissu amesema Kibiti kuna kesi za watu zaidi ya 300 wametoweka, hii tu inatosha kuipa nguvu mahakama hiyo kuchunguza waliko watu hawa, mauaji ya viroba cocobeach na Bagamoyo ni kesi zaidi ya 50 ambazo zimeripotiwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyoisha, hili linatosha pia kuipa nguvu mahakama hiyo, vile vile kesi za watu kutekwa ni nyingi, ukijumlisha yote hayo Lissu anawaangusheni wahalifu...

Hotuba ya Lissu jana hii hapa chini...

 

Attachments

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,375
2,000
Saafi...
Na hapa juzi kati wakaua tena raia kanisani mbele ya madhabahu halafu wakambambikizia askari wa uhifadhi wanyama.
Inasikitisha sana.

Siku zote dawa ya jeuri ni kiburi.
Wenye jeuri wa pale mjengo mweupe na mabunduki yao, wamekutana na mwenye kiburi wa pale Singida mwenye brain yake.
Wao wamejaza marisasi kwenye magazine, jamaa kajaza ma-faili kichwani.

Ngoja tuone mwisho wa hii saga.
 

Nnyindojihadini

JF-Expert Member
Nov 12, 2018
644
500
Mwambie TL aulize ushauri kwanza kwa Maalim Seif aliahidi kufungua kesi huko baada tu ya uchaguzi 2015, keshaenda mpaka huko UNO na mwaka huu 2019 tuna ingia duru nyingine ya uchaguzi bila ya mrejesho.

Haya mambo yana gharama zake TL na jeuri na dharau zake tele kainamishwa na sasa bila soni anapigia chapuo Ushoga si mchezo mchezo.
 

Tumbo Tumbo

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
1,283
2,000
Ni propaganda tu maana ,Under international criminal law ICC ina mamlaka (Jurisdiction) ya kuskiiza mashtaka manne tu,
i) Genocide
ii) Aggression
iii) War Crime
iv) Crime against Humanity.
Ambayo hakuna lolote kati ya halo Tanzania au viongoz wake wanaeza kuwa charged of.Pili, ICC kwa mujibu wa Rome Statute ambayo ndio imeanzisha hii mahakama haina primary jurisdiction kudeal na hayo makosa ni mpaka kuwe na mazingira yafuatayo.
i) Trigger mechanism endapo mahakama na mamlaka za ndani zimeshindwa kuendesha mashtaka dhidi ya wahusika wa makoswa tajwa hapo juu,
ii) By UN SECURITY COUNCIL REFERRAL kwamba balaza la usalama la umoja wa mataifa lipitishe azimio na kuiamuru mahakama ya ICC kuanza uchunguzi kitu ambacho pia kwetu hakipo.
Nadhani ni siasa na propaganda tu kama Maalim Seif kwenda ICC kupinga uchaguzi wa Zbar
#MababichaAkiliZaoZimejaaVumbiKichwani

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom