Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Dawa ya upuuzi huu wa CCM ni serikali za majimbo tu. Leo hii Kuna sehemu hazina hata barabara kisa tu zinaongozwa na upinzani alafu kibaya watu wanajisifu mchana kreupel Eti ole wenu mchague upinzani kama mtapata maendeleo!!!Serikali ya majimbo ndiyo majibu ya kuondokana na huu umasikini unaotengenezwa na mfumo wa kigandamizaji. Sasa hivi kila mtu anajitoa fahamu kumshukuru Rais wakati na yeye mtumishi tu wa wananchi kwa sababu yeye ndiye anaamuwa wapi kuendelezwe na wapi kusiendelezwe hadi anasema wasipochagua CCM hawawezi kujengewa lami bunda hivi kodi inayokusanywa pale bunda anahaki ya kwenda kuendelezea majimbo ya CCM badala ya Bunda ilipotoka kodi. Ni sawa kabisa kuwa na serikali za majimbo kwanza kutakuwa na kushindana kwa maendeleo kati ya jimbo na jimbo na hivyo kuchochoa kasi ya maendeleo. Hata viongozi wa hayo majimbo watawajibika kwa wananchi wa kwenye majimbo husika badala ya kuwa na hao mapandikizi ambao hawana uchungu wowote na maeneo wanayoyaongoza sababu wanawajibika kwa aliyewateua. Hata Haya maamuzi ya kutumia polisi kupiga wananchi yatakomeshwa kabisa sababu viongozi wote watakuwa wanawajibika kwa wananchi kama ilivyo katika katika kuwa mamlaka inatoka kwa wananchi siyo kwa Rais.