Lissu asema CHADEMA itaigawa Tanzania kwa Majimbo. Kila jimbo litakula kwa urefu wa kamba yake

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,206
42,067
Wasalaam wana jamvi

Leo Lissu kaendelea na kampeni lakini jambo la kushtua zaidi ni mpango wa CHADEMA wa kuigawa Tanzania kwa majimbo kwa kisingizio kuwa majimbo ndio chanzo cha maendeleo

Lissu ameendelea kusema kuwa nchi ikagawiwa kwa majimbo ndio watu watapata maendeleo na kila mtanzania atakula kwa urefu wa kamba zake.

Wasalaam wana jamvi

 
Yuko sahihi kwa mfano Shinyanga una majimbo ambayo yanatoa madini ya mabilioni lakini Wananchi maskini wa kutupwa. Wakati Dar es salaam hamna rasilimali yoyote ujanja ujanja na utapeli kama wakina Gwajima.

Halafu ndio kuna maendeleo hakuna vumbi barabara zote ziko vizuri.borea kila mtu ale cake alipo...kama uko Jimbo ambalo halizalishi basi hamia lile lenye shughuli za uchumi kubwa.imeisha hiyo
 
Wazo zuri sana hili. Hakuna jimbo masikini kila mtu akijiamulia mambo yake ndipo tutaweza kuendelea.

Sio leo mtu kakurupuka tu huko anachukua hela za gas Mtwara anaenda kujenga International Airport Kijijini kwake Chato ilihali huko kwa wenye gas hakuna hata barabara la lami.

Safi sana CHADEMA TUMAINI LA PEKEE LA WATANGANYIKA NA WAZANZIBAR
 
Hata mgombea wenu wa urais Meko ameshatugawa kikanda.

Kuna kanda ya kubomoleshewa nyumba na kuna kanda ya kulindwa

Kuna kanda ya kuongea kisukuma na kuna kanda ya kuongea broken swahili

Kuna kanda zinapewa ajira serikalini na kuna kanda zimetengwa kwa muda usiojulikana.
 
Ubaguzi na upendeleo wa Maguful kwa kanda ya ziwa na kijijini kwake kumeonesha tena umuhimu wa sera ya majimbo. Kanda ya Ziwa ingekuwa jimbo lenye serikali yake wakaamua kujenga Chato International Airport hamna mtu angeuliza.

Tatizo linakuja anapoamua kupendelea anapotoka na kuona kwingine hawastahili au wasubirie. Siyo haki
 
Hata mgombea wenu wa urais Meko ameshatugawa kikanda.

Kuna kanda ya kubomoleshewa nyumba na kuna kanda ya kulindwa

Kuna kanda ya kuongea kisukuma na kuna kanda ya kuongea broken swahili

Kuna kanda zinapewa ajira serikalini na kuna kanda zimetengwa kwa muda usiojulikana.
Tena alisema kabisa mwanza walinipa kura wasibomolewe!!
 
Yuko sahihi kwa mfano shinyanga una majimbo ambayo yanatoa madini ya mabilioni lakini wananchi maskini wa kutupwa.wakati dar es salaam hamna rasilimali yoyote ujanja ujanja na utapeli kama wakina gwajima halafu ndio kuna maendeleo hakuna vumbi barabara zote ziko vizuri.borea kila mtu ale cake alipo...kama uko Jimbo ambalo halizalishi basi hamia lile lenye shughuli za uchumi kubwa.imeisha hiyo
Hivi unajua bandari inaingiza kiasi gani
 
Serikali ya majimbo ndiyo majibu ya kuondokana na huu umasikini unaotengenezwa na mfumo wa kigandamizaji. Sasa hivi kila mtu anajitoa fahamu kumshukuru Rais wakati na yeye mtumishi tu wa wananchi kwa sababu yeye ndiye anaamuwa wapi kuendelezwe na wapi kusiendelezwe hadi anasema wasipochagua CCM hawawezi kujengewa lami bunda hivi kodi inayokusanywa pale bunda anahaki ya kwenda kuendelezea majimbo ya CCM badala ya Bunda ilipotoka kodi.

Ni sawa kabisa kuwa na serikali za majimbo kwanza kutakuwa na kushindana kwa maendeleo kati ya jimbo na jimbo na hivyo kuchochoa kasi ya maendeleo. Hata viongozi wa hayo majimbo watawajibika kwa wananchi wa kwenye majimbo husika badala ya kuwa na hao mapandikizi ambao hawana uchungu wowote na maeneo wanayoyaongoza sababu wanawajibika kwa aliyewateua.

Hata Haya maamuzi ya kutumia polisi kupiga wananchi yatakomeshwa kabisa sababu viongozi wote watakuwa wanawajibika kwa wananchi kama ilivyo katika katika kuwa mamlaka inatoka kwa wananchi siyo kwa Rais.
 
viongozi wote watakuwa wanawajibika kwa wananchi kama ilivyo katika katika kuwa mamlaka inatoka kwa wa. Hapa Kazi Tuu Ikulu Mtapasikia Tuu
 
Back
Top Bottom