Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,498
- 51,092
Akizungumza mbele ya umati wa wananchi huko Babati, Lissu amesema wamepata taarifa za vikao vya wakubwa na vibaraka wao wanaohofia kimbunga chake huko mikoani.
Lissu anasema mkakati huo wa kumuengua ulijenhwa juu ya hoja mbili.
1. Ya kwanza ni wao kutaka kupitia kichaka cha maadili, kwamba kwa kuwa alifutwa Ubunge na Ndugai kupitia hoja mfu za maadili basi asiruhusiwe kugombea urais. Lissu anasema hoja hiyo wameshaifuta kwa sababu sheria inataka mtu awe amefungwa ndo hilo takwa linakamilika.
2. Pili kuhusu nia yao ovu ya kumuengua kuhusu kuanza kampeni mapema Lissu kasema kuwa kisheria Mtu haanzi kampeni mapema mpaka awe tayari ameshapitishwa na tume huru ya uchaguzi kuwa mgombea na kisha tarehe ya kampeni iwe imetangazwa ndo unaweza kusema kuwa huyu kaanza kampeni mapema! Kama Tume haijapitisha wagombea basi kisheria hakuna cha suala la kuanza kampeni mapema.
Hoja kuntu za Lissu unaweza kuzisikiliza hapa chini: