Lissu anyimwa Dhamana, kupelekwa mahakamani kesho

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Mbunge wa Singida Mashariki Wakili Tundu Lissu anatuhumiwa na Jeshi la Polisi kufanya Uchochezi na kutoa lugha ya matusi. Polisi wamemnyima dhamana atafikishwa Mahakamani kesho.

Tundu Lissu amehojiwa na polisi kwa saa tatu kutokana na kauli aliyoitoa jana nje ya mahakama ya Kisutu wakati akiongea na waandishi wa habari. Lissu atalala rumande leo kwa amri ya Zonal Crimes Officer (ZCO) baada ya kukosa dhamana.

Video hii ndo maneno Lissu aliyoyasema jana.
 
Mbunge wa Singida Mashariki Wakili Tundu Lissu anatuhumiwa na Jeshi la Polisi kufanya Uchochezi na kutoa lugha ya matusi. Polisi wamemnyima dhamana atafikishwa Mahakamani kesho.
Saafi sana. Hivi yeye haoni wajanja akina Lowasa na Sumaye wapo kimya, wakiongea wanalinda kauli zao. Upinzani siyo mihemuko, na huwezi kushindana na serikali, maana Lissu akumbuke kuwa wanasiasa huwa wanabadilishana lakini siyo watendaji wa serikali, hao hukaa mpaka kufikia umri wa kustaafu, huwezi ukalikashifu jeshi la polisi au jwt halafu ubaki uraiani wao wanafanya kazi bila kuangalia siasa.
 
Wanadhani hatua hiyo ni kumdhalilisha au kumkatisha tamaa au kumkoma siyo?. Hivi kweli hajui kama watamnyima hiyo dhamana na akawa amejipanga kifikra? Yaani Simba wampeleka zizi la Mbuzi?. Huko ni kuongeza tatizo mahabusu kwa kuwaongezea wale wafungwa/mahabusu morali ya kujisikia nao wako sehemu sahihi.
 
Saafi sana. Hivi yeye haoni wajanja akina Lowasa na Sumaye wapo kimya, wakiongea wanalinda kauli zao. Upinzani siyo mihemuko, na huwezi kushindana na serikali, maana Lissu akumbuke kuwa wanasiasa huwa wanabadilishana lakini siyo watendaji wa serikali, hao hukaa mpaka kufikia umri wa kustaafu, huwezi ukalikashifu jeshi la polisi au jwt halafu ubaki uraiani wao wanafanya kazi bila kuangalia siasa.
Acha kukurupuka ni lini Lissu amelikashifu jeshi la polisi, kama hujui kitu kaa kimya.
 
13528718_738782559596571_6772389937267433792_n-jpg.361217

#FreeKamandaLissu
 
Back
Top Bottom