Uchaguzi 2020 Lissu anapouaminisha Umma kuwa atakuwa Rais bora kupitia hulka za mtu aliyesomea Sheria

Mchimwachimego

JF-Expert Member
Jun 15, 2020
358
271
Kwanza nikiri wazi kwamba mtaji wa siasa ni maneno matamu, lakini siasa ni adui mkubwa wa ufahamu na nirafiki wa shetani, mwanasiasa si wa kumwamini 100% kwa sababu siasa ndio chanzo mabaya yote duniani.

Tokea nimemfahamu mtu aitwaye Tundu Lissu nimejifunza kitu baada ya kufuatilia watu dizaini yake ambao wamesomea sheria ambao katika jamii tunawaita maneno mengi na wajuaji lakini si watendaji, nje ya maneno ni watu ambao hawawezi kutatua shida yoyote iliyo nje ya alichokisomea, kwa ufupi ni "TEGEMEZI"

Katika mtiririko huo ndio bwana Tundu Lisu anautumia kwenye kampeni zake kuwashawishi wa kifikra na wavivu wa kazi kwamba maisha ni rahisi sana na pesa au maendeleo ya mtu au nchi yanapatikana kirahisi, pia anatumia taaluma yake ya uwakili kuonesha kuwa yeye mtetezi wa wanachi dhidi ya sheria atakazozitumia kuongoza nchi na anajua wazi kuwa hakuna sheria isiyomuhusu mwananchi na ata hakuna nchi yoyote isiyo na sheria za kuendesha nchi.

Wanasheria ni waongeaji sana na wabishi sana na sababu mkubwa ni kwamba wamekariri sheria na matukio ni ngumu kumuingizia jambo jipya la ubunifu wa mawazo katika akili zake yeye umelitoa umelitoa wapi? Halifanywi hivi ngoja nikaangalie kwenye kitabu hivyo kupitia andiko hili nawashauri watanzania kamwe tusimwamini mtu aliyezoea kulishwa, asiyejua kutafuta kwa akili zake, anayetegemea kuongozwa na miongozo kutoka Belgium.

Tumchague mwanasayansi ambao ni waanzilishi wa vitu vyote hapa duniani vinavyokupa kiburi mjini, Gari, simu, kompyuta, madaraja, meli, ndege, viwanda nk: na siyo mwingine ni DR JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI+ mtekelezaji wa bwawa kubwa la kufua umeme, mjenzi wa barabara na madaraja 80% Tanzania nzima, mjenzi wa reli baada ya mjerumani, mjenzi wa hospitali, meli, bandari, viwanja vya ndege, ndege, stand za mabasi, elimu bure, mwanzilshi wa masoko ya madini, ujenzi wa mji wa serikali, ikulu mpya,Nk.

Huyu anatufaa kwa sababu anaimiza kazi na si kuwa mjuaji na muongeaji "NO PAIN NO GAIN"

Asanteni.
 
Siwezi kumchagua mtu asiyejali utu wa mwingine.
Magufuli katutesa watumishi wa umma kwa miaka mitano pasi kutupatia nyongeza ya mishahara wala kutupandisha vyeo.

Hayo madaraja yake aliyoyajenga hayawezi kunifanya mimi nipate kiinua mgongo kikubwa pale nitakapostaafu isipokuwa upandaji vyeo kwa wakati utaniwezesha kukomba mamilioni ya kutosha wakati wa kustaafu.

Meko ana hali ngumu sana uchguzi huu.
 
WATANZANIA wana imani na JPM, kuwavusha mpaka uchumi wa kati wa juu. Kazi iendelee.. Tano tena.
 
Kwahiyo hapa unasema tuchague mwanasayansi mara zote?2005 ulikuwa wapi kushauri hayo?1995 ulikuwa wapi kushauri hayo?
Hapa unajaribu kusema waliosoma sayansi kwasababu ndio wagunduzi wa magari na madaraja basi ndio wawe marais!

Hizi akili za kuvukia barabara mnazitoa wapi?

Shame!
 
Watanzania tunajitambua atuwezi mchagua Lissu ambae kwa miaka zaidi ya 7 kashindwa kupeleka maendeleo kwenye jimbo lake,jimbo lake kashindwa kujenga hata ofisi ya Chama chake.anaropoka tu hana sera na ushawishi wa kuongoza nchi.
Anakusanya kodi?Haya kaomba apewe ridhaa akusanye kodi ili awaletee watanzania maendeleo,uhuru na haki!
Ilaumu serikali yako ya CCM kwa mapungufu yoyote katika nchi hii!
 
Kwahiyo miaka saba alikuwa anakusanya kodi hapo jimboni kwake?
Watanzania tunajitambua atuwezi mchagua Lissu ambae kwa miaka zaidi ya 7 kashindwa kupeleka maendeleo kwenye jimbo lake,jimbo lake kashindwa kujenga hata ofisi ya Chama chake.anaropoka tu hana sera na ushawishi wa kuongoza nchi.
 
Ngoja waje wale wa kushindwa kujibu hoja ispokua kejeri na matusi ,si wengine ni ufipa jazz band
 
Siwezi kumchagua mtu asiyejali utu wa mwingine.Magufuli katutesa watumishi wa umma kwa miaka mitano pasi kutupatia nyongeza ya mishahara wala kutupandisha vyeo....
Acha kulialia. Fanya maamuzi, km kazi haikulipi achananayo, njoo ukaze msuli kitaa. Mbona watu kibao tu hatuna ajira na tunadumu?
 
Siwezi kumchagua mtu asiyejali utu wa mwingine. Magufuli katutesa watumishi wa umma kwa miaka mitano pasi kutupatia nyongeza ya mishahara wala kutupandisha vyeo..
Bora kumpigia Rungwe kuliko Magufuli
 
Watanzania tunajitambua atuwezi mchagua Lissu ambae kwa miaka zaidi ya 7 kashindwa kupeleka maendeleo kwenye jimbo lake,jimbo lake kashindwa kujenga hata ofisi ya Chama chake.anaropoka tu hana sera na ushawishi wa kuongoza nchi.
Mbunge ndo anapeleka maendeleo jimboni??? Hilo ndo jukumu la mbunge??
 
Siwezi kumchagua mtu asiyejali utu wa mwingine. Magufuli katutesa watumishi wa umma kwa miaka mitano pasi kutupatia nyongeza ya mishahara wala kutupandisha vyeo...
Kuchagua Lissu ni kupoteza kura bure. Akaanze kwanza kugombea, UENYEKITI pale Ufipa ndio tumjue ni bora au sio bora.
 
Watanzania tunajitambua atuwezi mchagua Lissu ambae kwa miaka zaidi ya 7 kashindwa kupeleka maendeleo kwenye jimbo lake,jimbo lake kashindwa kujenga hata ofisi ya Chama chake.anaropoka tu hana sera na ushawishi wa kuongoza nchi.
Kweli kabisa. Tunataka wabunge kwa ajili, ya kutatua changamoto za wananchi.Mafiga matatu, safari hii hakuna kuweka gunzi katikati...
 
Watanzania tunajitambua atuwezi mchagua Lissu ambae kwa miaka zaidi ya 7 kashindwa kupeleka maendeleo kwenye jimbo lake,jimbo lake kashindwa kujenga hata ofisi ya Chama chake.anaropoka tu hana sera na ushawishi wa kuongoza nchi.

Wabongo tunavichwa vibovu na vigumu ana ...one of the issues that has kept cmm over here in Tanzania is ignorance level and this has allowed the feet of cmm to be on our to be on our necks for a longer period...
 
Back
Top Bottom