- Source #1
- View Source #1
Nimeona video ikiwa na graphics kwamba Lissu amemtambulisha mganga wake jukwaani
- Tunachokijua
- Makamu Mwenyekiti waChama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu alifanya mkutano wa hadhara uliofanyika mkoani Mara wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa. Akiwa kwenye mkutano huo Lissu alizungumza mambo mbalimbali ikiwemo idadi ya wagombea kwenye Jimbo la Singida Mashariki kuwa ni ya kuridhisha. Mkutano huo umewekwa kwenye chaneli mbalimbali za mtandao wa youtube ikiwemo hapa.
Imekuwepo taarifa ikisambaa ikidai kuwa Lissu amemtambulisha mganga wake jukwaani, mathalani mtu mmoja katika mtandao wa X aliandika;
"Siasa siyo Vita!Viongozi wa chadema wameamua kupanda mpaka na wachawi wao kwenye kampeni zao" Angalia pia hapa na hapa
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji kuhusu taarifa hiyo na kubaini kuwa haina ukweli na imepotoshwa. Tumefuatilia hotuba nzima ya Lissu akiwa kwenye mkutano huo, wakati akiendelea na hotuba yake alisema kuwa;
"Nayasema yote haya kwa sababu nimekuja na mzee wa Singina Mashariki, nimemwambia mzee twende kwa wakwe zangu, twende ukawasalimie wakwe zangu na shemeji zangu uwape salamu za Singida Mashariki. Awasalimie halafu tuendelee, mzee wangu wa chama wa miaka yote sawa sawa? Awasalimie kidogo halafu tuendelee"
Lissu alimtambulisha mzee anayedaiwa kuwa ni mganga wake, kuwa ni mzee wa chama na ametoka naye Singida Mashariki ili kwenda naye katika mkutano huo ili akawasalimia wakwe zake (wa Lissu) na hakuna mahali alipomtambulisha mtu huyo kama mganga wake.
Video pia inayodai Lissu amemtambulisha mganga wake imehaririwa kwa kuongezewa sauti ambazo hazipo kwenye video halisi. Video inayopotosha kuna maneno yanasikika yakisema "mchawi huyo, hiyo ni uongo" yameongezwa na ni maneno ambayo yametolewa kutoka kwenye video iliyosambaa mtandaoni kutokea nchini Kenya.