Lissu ambana Mbowe: Aelezea Historia yake, adai hajawahi omba kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, "Nimekijenga chama kwa jasho na nguvu zangu"

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
104,725
2,000
Chadema kila siku mnasisitiza kutengeneza mifumo imara ya uongozi na siyo kutegemea mtu mmoja. Mbona nyie hamuonyeshi mfano kwenye chama chenu? Kwa hiyo Mbowe akifariki leo na Chadema ndo basi tena?
Kwani ccm nayo imekufa?
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,394
2,000
Ningependa niweke wazi na Watanzania wakielewe, sijawahi kuomba kuwa mwenyekiti kwa mtu yeyote, mwaka 2004 nilikuwa Mwenyekiti baada ya wajumbe wa kamati kuu na wazee wa Chadema kunipendekeza kutokana na historia na commitment yangu ya chama.

Nilianza harakati za kuijenga Chadema baada ya kuona kinasinzia mwaka 2000, nikiwa na Dk. Wilbrod Slaa na wengine watatu, tulitoa magari yetu tukatembea nchi nzima kufanya mikutano. Nikaenda vyuo vikuu kutafuta wanafunzi walioonesha mwelekeo wa kuwa viongozi.
View attachment 1774522
Rubbish in this is the way Lissu tries to glorify Nyerere by a way of association with Mbowe. Ni lissu aliyesema yote ya hovyo juu ya Nyerere wakati wa Bunge la katiba.
 
Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,154
2,000
Katika vetting bora Kuwai kufanyika Tanzania ni hii ya mbowe kuwa mwenyekiti

Other wise chadema ingekuwa tayari ni historia.

Kama ilivyo kwa CUF, NCCR, TADEA, UDP na ACT

kabisa sawa na vetting ya CCM kwa Tanzania, ni vetting bora kabisa kuwahi kufanyika

usihamishe goli
 
cocastic

JF-Expert Member
Nov 30, 2019
18,544
2,000
Mwamba anaunguruma .
Mwenyekiti wangu mie huyo.
Yaani utabaki kuwa Mwenyekiti ili MaCCM yaendelee kuzima mmoja bada ya mwingine .. DADEKI..

leo lumumba na Chamwino washapata kazi yakuwaingizia hela. Ni kumtukana Mzee Mbowe, mpaka vijasho vya kwapani viwatie fangasi.
MaCCM yanamuogopa sana Mbowe.
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
104,725
2,000
CCM Wana mfumo mzuri wa kuachiana madaraka kila baada ya miaka kumi, ndiyo maana wanapeta tu.
Kwani kwa miaka 60 ya uhuru wa nchi hii ccm imewafanyia nini watanzania zaidi ya kuwatia umasikini ulio topea?
 
Mnyanyembe wa Mboka

JF-Expert Member
Feb 10, 2017
2,047
2,000
Kwa hiyo Mbowe akifa na chadema inakufa?
Of coz asipopatikana mtu kama MBOWE chama kinakufa hilo lipo wazi

Na ni ngumu sana kumpata mtu kama mbowe otherwise Mungu mwenyewe aamue kumleta wa kufanana nae

Na ndio maana and anibidi awe mwenyekiti yeye tu kwa sababu hakuna mbadala wake kwa sasa
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
6,248
2,000
CCM Wana mfumo mzuri wa kuachiana madaraka kila baada ya miaka kumi, ndiyo maana wanapeta tu.
Usitudanganye. CCM inabadilisha Mwenyekiti kila baada ya miaka kumi kwa sababu Rais mpya anaingia madarakani. Isingekuwa hivyo nao wangebaki na yule aliyeshindwa uchaguzi.
Tofauti kubwa na CCM ni kuwa Chadema wanakubali mtu ambae sio Mwenyekiti kugombea urais. Ni lini CCM wameruhusu mwanachama mwingine kushindana na Mwenyekiti aliyepo kugombea urais kwa niaba yao? Hiyo inatokea pale tu ambapo Mwenyekiti anakuwa hawezi kugombea tena urais kikatiba. Na hata hivyo, kama JK, alivyotufahamisha Mwenyekiti ana maamuzi makubwa kuhusu nani agombee.

Waacheni Chadema waendelee na mfumo ambao wao wanaona unawafaa. Ni wao peke yao ndio wenye maamuzi, sio wapinzani wao.

Amandla...
 
Kohelethi

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
2,219
2,000
We ni moja ya kundi la watu wajinga ambao hata Mwenda alipokuwa anauwa watu na bado mlimshangilia. Lini uliona mbowe akitoa maneno ya Dharau kwa Dr slaa?.
Leo hii dr Slaa anaitwa dr Mihogo na misukule yako huku wengine wakiambatanisha na matusi, ww kama mwenyekiti umeshindwa kutoka hadharan kuwakemea hao mbwe.ha koko waliokuwa wanamchafua yule mzee alietumia nguvu zake na mali zake kupigania chama. Ilifikia kipindi dr Slaa alionekana hana thaman hata mbele ya "mr zero" kisa tu mshiko wake aliotumia kuhonga chama. Ki ukweli na bado dhambi ya kumtukana na kumdhalilisha dr Slaa itaendelea kukitafuna chama na wanachama kwa ujumla. Hongera pesa kwa kutuonesha ni nani mwenye roho ya utu na nani mwenye roho ya kutu.
 
Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
2,072
2,000
Usitudanganye. CCM inabadilisha Mwenyekiti kila baada ya miaka kumi kwa sababu Rais mpya anaingia madarakani. Isingekuwa hivyo nao wangebaki na yule aliyeshindwa uchaguzi.
Tofauti kubwa na CCM ni kuwa Chadema wanakubali mtu ambae sio Mwenyekiti kugombea urais. Ni lini CCM wameruhusu mwanachama mwingine kushindana na Mwenyekiti aliyepo kugombea urais kwa niaba yao? Hiyo inatokea pale tu ambapo Mwenyekiti anakuwa hawezi kugombea tena urais kikatiba. Na hata hivyo, kama JK, alivyotufahamisha Mwenyekiti ana maamuzi makubwa kuhusu nani agombee.

Waacheni Chadema waendelee na mfumo ambao wao wanaona unawafaa. Ni wao peke yao ndio wenye maamuzi, sio wapinzani wao.

Amandla...
Inawezekana ikawa hivyo kweli, lakini kuna kigezo kimoja ambacho lazima Mgombea Urais anapaswa awe nacho Kaka Mbowe hana.

Hitaji la Mgombea lazima awe na Elimu ya Degree kutoka katika chuo kinacho tambulika.
 
Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
3,045
2,000
Chadema kila siku mnasisitiza kutengeneza mifumo imara ya uongozi na siyo kutegemea mtu mmoja. Mbona nyie hamuonyeshi mfano kwenye chama chenu? Kwa hiyo Mbowe akifariki leo na Chadema ndo basi tena?
Akikujibu nitagi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom