Lissu aibua bungeni mauaji ya Nyamongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lissu aibua bungeni mauaji ya Nyamongo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 17, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  [​IMG]
  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, (Chadema

  Spika wa Bunge Anne Makinda, ametaka Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, (Chadema), apeleke kwa maandishi malalamiko yake ya kutoridhishwa na kukataliwa kujibiwa kwa swali lake alilouliza kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kuhusiana na mauaji ya wananchi katika mgodi wa North Mara uliopo Nyamongo, wilayani Tarime mkoani Mara.  Hatua hiyo ilifuatia Lissu kuomba mwongozo kutoka kwa Spika Makinda baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika bungeni jana baada Spika kumkatalia yeye na Mbunge wa Viti Maalum kupitia chama hicho, Esther Matiku kujibiwa maswali yaliyohusiana na mauaji ya raia yanayodaiwa kufanywa na polisi kwenye mgodi huo. Spika alikataa kujibiwa kwa maswali hayo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwa maelezo kesi ipo mahakamani. "Mheshimiwa Spika hadi sasa hakuna kesi hata moja inayowahusu waliohusika na mauaji haya na hakuna hata polisi mmoja aliyeshtakiwa," alisema.

  Spika alisema kuwa wamepokea malalamiko kutoka katika muhimili huo wa dola (Mahakama) kuwa wamekuwa wanaingilia uhuru wa mahakama na hivyo kukataa swali hilo. Akiomba mwongozo, Lissu alisema ingawa Spika alikataa swali lake lakini, hakuna kesi ya mauaji inayohusisha mgodi huo labda kama Spika Makinda anafahamu uwepo wa kesi.

  Alisema yeye na Matiku wanashitakiwa, lakini kesi yao haihusiani na mauaji.
  Akijibu muongozo huo, Spika alimtaka kuandika kwa njia ya maandishi kwa Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, iwapo watahisi uamuzi wa Spika haukuwatendea haki, na suala hilo litajadiliwa na kuamuliwa na Kamati ya uongozi wa Bunge.

  Lissu katika swali lake alimtaka Waziri Mkuu afafanue juu ya taarifa ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ya mwaka jana iliyotolewa Mei mwaka huu na kuungwa mkono na taarifa ya Mambo ya Nje ya Marekani kuwa polisi nchini wanashiriki katika kuua raia 52. Pia alisema kwa upande wa Tarime polisi wameua wanakijiji 26 wa mgodi wa North Mara.

  Kabla Spika hajajibu mwongozo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, alitoa utaratibu kwa kutumia kifungu cha kanuni za Bunge na kueleza kuwa anaamini kuwa Lissu na Matiko maswali yao yaligusa kesi zinazowakabili kwa kuwa yote yanahusu mambo yanayoendelea katika mgodi wa North Mara Tarime. "Mheshimiwa Spika ni kweli Lissu ameshtakiwa na ni kweli kesi inahusu mgodi wa Nyamongo na Tarime na kanuni inasema, mbunge hatazungumzia jambo lolote linalohusiana na mahakama, ushauri wangu mheshimiwa asubiri mahakama imalize kesi hii, iwe ya mgodi au polisi maswali haya yanaingilia uhuru wa mahakama," alisema.

  Awali Lissu, katika kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alimwuliza kuwa serikali imehalalisha mauaji ya raia yanayofanywa na Jeshi la Polisi kwani matokio hayo yamekuwa ya kawaida. Akijibu mwongozo na utaratibu wa wabunge hao, Spika alisema "Waheshimiwa wabunge tusijifanye sisi tunajua kila kitu na kuhukumu, Matiko na Lissu wako nje kwa dhamana sasa wao ndio waulizaji wa maswali haya ni haki kweli hiyo? Ndio maana ninasema jambo hili tuliache huko huko lisuluhishwe tuwaachie mahakama. Spika Anne Makinda alikataa swali hilo lisijibiwe na Pinda kwa kuwa suala la mauaji bado liko mahakamani na Bunge lisingependa kuingilia mihimili mingine ya dola.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Sijasikia shauri la mauaji Tarime kufunguliwa katika mahakama ya Tanzania, sasa Spika anapokataza kwamba shauri liko mahakamani ni ipi?
   
 3. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,206
  Likes Received: 3,771
  Trophy Points: 280
  Watayafunika weee mauaji ya nyamongo lakini mwisho sheria itafuata mkondo wake!!! Serikali ya ccm ni genge la wauaji! Hii haina chenga kabisa.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kwani wa kufungua ni nani?? serikali ijifungulie mashitaka au wananchi icnluding wawakilishi wao ndio waifungulie serikali mashtaka?
   
 5. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Kwako Anne Makinda, ogopa Mungu. Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo anakuonya, Kilio cha watu wake amekisikia. Kama alivyowasikia watu wake waebrania katika Misri ya Farao, amewasikia watanzania wakilia. BWANA, Mungu wa Majeshi amesikia kilio cha watu wake na maombi ya watakatifu wake. Kumbuka, alimwambia Kaini damu ya ndugu yako inanililia toka aridhini. Wewe ANNE MAKINDA na serikali yenu yote, na wakuu wa polisi mahakama, Mungu aliyehai, Yeye aishiye, ameisikia damu ya watanzania inayomlilia, Bulyanhuru, Ubaruku, Dar, Nyamongo, Arusha,nk nk. BWANA anawaambia siku zote YEYE ni Mungu wa haki na kweli.

  Kwa ushauri wangu soma:Mithali 24:24 " Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Kabila za watu watamlaani, taifa watamchukia."
   
Loading...