Lissu achana na stori za risasi, panga hoja zako utawafanyia nini Watanzania

Kabisa, mpaka sasa wananchi hawajui Lisu atawafanyia nini. Stori telling kuhitaji huruma hazitasaidia. Angeanza kupambania changamoto zinazowakumba wananchi.mfano kufungua kesi kupinga kufutwa fao la kujitoa....

Hata hivyo, kama alishindwa kumtaja aliyetaka kumuua akiwa nje ya nchi ataweza akiwa nchini. Acheni kumdanganya Lisu. Deal na issues, zungumzia kero, changamoto, na ufumbuzi wake....be presidential material....
Siyo lazima kumtaja aliyetaka kumuua akiwa nje ni vyema amtaje akiwa Tanzania ingawa waliotekeleza tukio lote wanajulikana vizuri, kero zote ambazo CCM wameshindwa kuzitatua ikiwemo uhuru wa habari Elimu bure hadi chuo kukuu, kujenga viwanda kila kata, vyuo vikuu kila wilaya, Hosptal za rufaa kubwa zenye madaktari Bingwa kila mkoa, daraja toka Dsm mpaka Zanzibar na pemba na mengineyo mengi yatafanyika endapo CCM itakubali kukaa pembeni baada ya kuacha uchakachuaji
 
Hata yeye hanashida na kura za huruma. Kama ungelikuwa wewe, usingependa kuwapa watu picha ya udhaifu wa mifumo na udhibiti ili wajue kuna sababu ya kuiimarisha? Ukiwa mkweli na ukavaa kiatu chake utaona ana kila sababu ya kuzungumza. Ila tu agawe mada vizuri isije hii ikabeba sehemu kubwa na akaacha masuala ya 2021 - 2025.
Kikubwa kilicho mludisha home ni malengo yake kama alivyo sema ila amekuwa mtu wa kuzungumzia lile tukio na sio malengo yake yaliyo mludisha hiv ni nani leo hii asiye jua kama lissu kweli hakufanyiwa fear..ss ilibidi alichukue hili liwe moja ya sera zake kuwa ata dhibiti vitu kama vilivyo mkuta yy visitokee kwa wengine lakin yy kila mda anataka kutia huruma watanzania hatuta mpigia kura kwa kuwa alionewa
 
Rais wetu akiongea habari ya sumu, anaweka tu kama kionjo ili watu wajue kubadili mifumo ya umafia siyo lelemama ni kazi inayohitaji watu na supports sahihi.
Ila Lissu haruhusiwi isipokuwa Jiwe! 😁😁
 
Bado hajateuliwa kuwa mgombea! Usiwe na haraka, sasa hivi ni mda wa kusimulia yaliyompata!
Alipozinduka kule Nairobi alisema wazi kuwa 'I have survived to tell the tale'.
So acha atuambie ni akina nani hao wenye roho za dubu waishio miongo mwetu!
Kama upo hapo nyumbani Tanzania jijini Dsm mtafute Le mutuz mpe mwanamke mrembo mkochi jinsi ya kupeleza vizuri mwache akae na Le mutuz hata masaa matatu atampa siri zote kwani ni mdhaifu mno kwa wanawake, Siri nyingi za Bashite zimepatikana kupitia Bashite
 
Kwahiyo unaumia Lissu akiwaeleza watanzania namna alivyoshambuliwa kwa risasi? Huu ni ushuhuda hata kwa vizazi vijavyo kuepuka Vitendo vya kinyama alivyofanyiwa Mh.TL
Lakini stori za risasi hazita ongeza kura mpaka awe Rais! Alivyoshauri mleta mada ni sawa. Lissu ajikite ni nini atafanya kipya ambacho Magufuli hakufanya au alichofanya ndivyo sivyo!
 
Achana na stori za kupigwa risasi, mara nani sijui haonekani, sijui nani katekwa, sijui risasi 16. Kamanda piga chini hizo stori. Mshukuru upo hai. Je waliokufa wanamsimulia nani? Mshukuru Mungu, samehe na sahau. Watanzania wameshasikia sana hayo.

Sasa hivi jipange na useme utawafanyia nini watanzania katika elimu, afya, ajira, fao la kujitoa, mikopo ya elimu ya juu, elimu ya sekondari, kilimo, maji, miundombinu, demokrasia, nk

Lisu piga chini stori. Watanzania wameshazisikia sana
Usijifanye kupotezea issue kubwa Kama hiyo. Kama Umetumwa Wasalimie. Lazima aseme. He survived to tell the tale
 
Aisee wee jamaa ni mchambuzi na mtaalam makini sana sema unabishana na wapumbavu na malofa, wao wanadhani sisi wananchi tutapiga kura za huruma, yaani mmoja analalamika alivyotaka kufa na mwingine anasema mkinichagua ntafanya kadha, kadha na kadha alaf wategemee atachaguliwa malalamikaji, Mkuu mi nimekubaliana na wewe sema unapoteza nguvu kutaka wafunza watu siasa mamboleo wakati wao wanataka kuhurumiwa
Ujumbe huu uwe tu maeneo ya salamu kwa kuwa ni kweli ni jambo la kutisha na lazima umma ujue. Lakini usibebe agenda ya mikutano wala kampeni. Anatakiwa kufanya tafiti za kisomi ili abaini (kama hajui) hali halisi ya taifa katika mambo yote. Kisha apate team ya wataalamu wamshauri namna ya kuyatatua hayo matatizo kwa misingi na hoja sanifu, za msingi na za kitaalm zenye kuleta tija katika maendeleo na ustawi ya taifa kwaleo na vizazi vijavyo.

Aondoe sura ya visasi na ajikite kuendeleza nchi kwa kuweka mizizi ya anachotaka kukifanya. Kusema tu nitaleta ajira, nitaongeza mishahara, nitatoa mikopo wanachuo wote, matibatu bure ni kujikosesha kura kwa sababu ni sawa na mtu anayesema atakata mti wakati hana hata kifaa cha kukatia. Ku address matatizo haya kwa juu juu is too temporary and unrealistic sawa na kukata matawi bila kutoa shina.,

Aepuke kutumia muda mwingi wa kuwaa attack watu na aapreciate mazuri waliyofanya, aonyeshe namna gani atayaendeleza na kuyaboresha na hata kufanya mengine zaidi ya hayo na siyo kudharau, kukandia na kudhihaaki mambo aliyofanya Rais wetu kwa muda mfupi ambayo mtangulizi wake hauwa na hata uwezo wa kuyafikiria kama yanawezekana.

Aache kabisa kumbeza rais Magufuli kwa kazikubwa nzuri alizofanya. Siasa za fitina chuki, hadaa na upotoshaji ni dharau kwa wapiga kura. HATUTAKI
 
Dogo acha dharau ingekuwa alopigwa risasi nikaka yako au baba yako sidhani kama ungekuja na kalu za dharau kiasi hiki.
Ndugu sidhani iwapo kauli yangu ni ya dharau. Kama nimekukwazwa sorry. But, Lisa ataendelea kuongea stori hiyo miaka mingapi na anatarajia kupata nini kutokana na kuendelea na stori hiyo? Kitu cha msingi akubali matokeo alimradi amepona. Ajipange kusonga mbele, ukweli hiyo stori kwa sasa sio mtaji hasa kuelekea kwenye uchagizi. Tulimuonea huruma kwa aliyotendewa, kipindi cha huruma kimepita now alete issue za kutushawishi kwamba yeye ni chaguo sahihi kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi ujao
 
Achana na stori za kupigwa risasi, mara nani sijui haonekani, sijui nani katekwa, sijui risasi 16. Kamanda piga chini hizo stori. Mshukuru upo hai. Je waliokufa wanamsimulia nani? Mshukuru Mungu, samehe na sahau. Watanzania wameshasikia sana hayo.

Sasa hivi jipange na useme utawafanyia nini watanzania katika elimu, afya, ajira, fao la kujitoa, mikopo ya elimu ya juu, elimu ya sekondari, kilimo, maji, miundombinu, demokrasia, nk

Lisu piga chini stori. Watanzania wameshazisikia sana
Mkuu, kwani simulizi za SGR, interchange, makao makuu ya nchi kuhamia rasmi Dodoma, kumengwa kwa viwanda zaidi ya 8,000 na nyingine kama hizo, nazo tayari zimeshachosha kusikika masikioni mwa Watanzania kwa miaka mitano mfululizo?
 
Aisee wee jamaa ni mchambuzi na mtaalam makini sana sema unabishana na wapumbavu na malofa, wao wanadhani sisi wananchi tutapiga kura za huruma, yaani mmoja analalamika alivyotaka kufa na mwingine anasema mkinichagua ntafanya kadha, kadha na kadha alaf wategemee atachaguliwa malalamikaji, Mkuu mi nimekubaliana na wewe sema unapoteza nguvu kutaka wafunza watu siasa mamboleo wakati wao wanataka kuhurumiwa
Ss mwanzo ulikuwa una bisha nn saiz unaongea nn au ndo push to start?
 
Sasa wewe kinachokuwasha ni nini hasa? Hiyo ni historia ya maisha yake, hapangiwi na mtu yeyote namna ya kuzungumza. Sisi mashabiki ndio tunapenda kusikia hizo story
Kinachouma nikwamba Anataka kuwa Rais bila kusema ataendelezaje Taifa letu! Anakalia, nimepigwa risasi 16! Hiyo kila mtu anajua mpaka sasa! Lakini, je! Utaleta maendeleo gani kwa taifa? Kusudi nikupe kura yangu.
 
Back
Top Bottom