Lissu achana na stori za risasi, panga hoja zako utawafanyia nini Watanzania

Kwahiyo unaumia Lissu akiwaeleza watanzania namna alivyoshambuliwa kwa risasi? Huu ni ushuhuda hata kwa vizazi vijavyo kuepuka Vitendo vya kinyama alivyofanyiwa Mh.TL
Wewe hujui lolote maumivu aliyoyapata Tundu lissu unaeza yalinganisha na Dr. Olimboka ya kung'olewa meno na kucha bila ganzi?

Siku zote Mwanaume halisi hatakiwi kulialia hata Kama kapatwa na matatizo maana huo ndo uanaume wenyewe.
 
Kabisa, mpaka sasa wananchi hawajui Lisu atawafanyia nini. Stori telling kuhitaji huruma hazitasaidia. Angeanza kupambania changamoto zinazowakumba wananchi.mfano kufungua kesi kupinga kufutwa fao la kujitoa....

Hata hivyo, kama alishindwa kumtaja aliyetaka kumuua akiwa nje ya nchi ataweza akiwa nchini. Acheni kumdanganya Lisu. Deal na issues, zungumzia kero, changamoto, na ufumbuzi wake....be presidential material....
Waliotaka kumuua lisu ni serikali ya ccm hili linajulikana na ndio maana siku anauliwa katika nyumba za serikali walinzi waliondolewa na CCTV footage ziliondolewa. Hii ni "common sense " tu mengine ya uchunguzi ambayo mpaka leo hatuambiwi yamefikia wapi nakuachia wewe mleta mada.
 
Wewe hujui lolote maumivu aliyoyapata Tundu lissu unaeza yalinganisha na Dr. Olimboka ya kung'olewa meno na kucha bila ganzi?

Siku zote Mwanaume halisi hatakiwi kulialia hata Kama kapatwa na matatizo maana huo ndo uanaume wenyewe.
Huna akili kwakifupi wewee ni mjinga.kwahiyo kama ulimboka alitolewa meno maumivu yake unataka nilinganishe na risasi alizopigwa TL?
Hoja hapa ni kwanini tumzuie TL asiyaseme aliyoyapitia na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na serikali mpaka sasa ?
 
Huo ushuhuda akawape polisi, tumechoka na stori za jaribio la kuuliwa.
Dogo acha dharau ingekuwa alopigwa risasi nikaka yako au baba yako sidhani kama ungekuja na kalu za dharau kiasi hiki.
 
Achana na stori za kupigwa risasi, mara nani sijui haonekani, sijui nani katekwa, sijui risasi 16. Kamanda piga chini hizo stori. Mshukuru upo hai. Je waliokufa wanamsimulia nani? Mshukuru Mungu, samehe na sahau. Watanzania wameshasikia sana hayo.

Sasa hivi jipange na useme utawafanyia nini watanzania katika elimu, afya, ajira, fao la kujitoa, mikopo ya elimu ya juu, elimu ya sekondari, kilimo, maji, miundombinu, demokrasia, nk

Lisu piga chini stori. Watanzania wameshazisikia sana
Mshauri na jiwe aachane na Story za kupewa sumu!
 
Kwahiyo unaumia Lissu akiwaeleza watanzania namna alivyoshambuliwa kwa risasi? Huu ni ushuhuda hata kwa vizazi vijavyo kuepuka Vitendo vya kinyama alivyofanyiwa Mh.TL

Ujumbe huu uwe tu maeneo ya salamu kwa kuwa ni kweli ni jambo la kutisha na lazima umma ujue. Lakini usibebe agenda ya mikutano wala kampeni. Anatakiwa kufanya tafiti za kisomi ili abaini (kama hajui) hali halisi ya taifa katika mambo yote. Kisha apate team ya wataalamu wamshauri namna ya kuyatatua hayo matatizo kwa misingi na hoja sanifu, za msingi na za kitaalm zenye kuleta tija katika maendeleo na ustawi ya taifa kwaleo na vizazi vijavyo.

Aondoe sura ya visasi na ajikite kuendeleza nchi kwa kuweka mizizi ya anachotaka kukifanya. Kusema tu nitaleta ajira, nitaongeza mishahara, nitatoa mikopo wanachuo wote, matibatu bure ni kujikosesha kura kwa sababu ni sawa na mtu anayesema atakata mti wakati hana hata kifaa cha kukatia. Ku address matatizo haya kwa juu juu is too temporary and unrealistic sawa na kukata matawi bila kutoa shina.,

Aepuke kutumia muda mwingi wa kuwaa attack watu na aapreciate mazuri waliyofanya, aonyeshe namna gani atayaendeleza na kuyaboresha na hata kufanya mengine zaidi ya hayo na siyo kudharau, kukandia na kudhihaaki mambo aliyofanya Rais wetu kwa muda mfupi ambayo mtangulizi wake hauwa na hata uwezo wa kuyafikiria kama yanawezekana.

Aache kabisa kumbeza rais Magufuli kwa kazikubwa nzuri alizofanya. Siasa za fitina chuki, hadaa na upotoshaji ni dharau kwa wapiga kura. HATUTAKI
 
Achana na stori za kupigwa risasi, mara nani sijui haonekani, sijui nani katekwa, sijui risasi 16. Kamanda piga chini hizo stori. Mshukuru upo hai. Je waliokufa wanamsimulia nani? Mshukuru Mungu, samehe na sahau. Watanzania wameshasikia sana hayo.

Sasa hivi jipange na useme utawafanyia nini watanzania katika elimu, afya, ajira, fao la kujitoa, mikopo ya elimu ya juu, elimu ya sekondari, kilimo, maji, miundombinu, demokrasia, nk

Lisu piga chini stori. Watanzania wameshazisikia sana
Mabaya aliyotendewa na akina Bashite Cyprian Musiba le mutuz Jerry muro , Heri kisanduku , Nyaulingo na wasiojulikana hana budi ayaseme kwa uwazi ili watanzania wajue ukweli iwe fundisho kwa wengine wenye nia ya uovu uonevu kama huo.
 
Wana ccm wanaogopa siku jembe atakapopanda jukwaani na kuwaga uchafu unaofanywa na wanywa kikombe cha babu wa loliondo. Atawakaanga na mtakubali tu kuwa mwenyekiti wenu hatumpendi. Atatuambia kama sio yeye aliyetaka kumuuwa lissu kwanini alizuia wabunge kwenda kumuona huko hospitali.
Hayo ndio ambayo Lisu ataifanyia tz akiwa rais?
 
Hiyo stori ya risasi ni muhimu sana ili kuwajulisha wananchi hatari ya utawala wa kikatili.

Kila mtu anaweza kuzungumza ajira na uchumi, lakini ni watu wachache wanaweza kuzungumza athari za utawala wa kikatili kwa mifano hai wananchi wakaelewa kama Lissu

Lissu aendelee kulizungmzia tukio lile, lakini lazima azungumzie masuala ya Ugali wa wananchi kwa mapana kabisa badala ya kuishia kupapasa papasa tu
Mwanaharakati yeyote aina ya Lisu hawezi kuingelea sera maana hayo ni kama mbingu na ardhi kwake.

Yule mpe mambo ya kulalamikia basi
 
Swal ni kwamba hakuna nani atampa kura kwa kumuonea huruma ety kisa alishambuliwa?

Hata yeye hanashida na kura za huruma. Kama ungelikuwa wewe, usingependa kuwapa watu picha ya udhaifu wa mifumo na udhibiti ili wajue kuna sababu ya kuiimarisha? Ukiwa mkweli na ukavaa kiatu chake utaona ana kila sababu ya kuzungumza. Ila tu agawe mada vizuri isije hii ikabeba sehemu kubwa na akaacha masuala ya 2021 - 2025.
 
Itasaidia nini hii stori, au itainua uchumi...anapoteana. Huu sio muda wa stori. Ajipange aje na mikakati ya ushindi
Bado hajateuliwa kuwa mgombea! Usiwe na haraka, sasa hivi ni mda wa kusimulia yaliyompata!
Alipozinduka kule Nairobi alisema wazi kuwa 'I have survived to tell the tale'.
So acha atuambie ni akina nani hao wenye roho za dubu waishio miongo mwetu!
 
Nye ndo mgeacha kumpiga risasi ili asiongelee kupigwa risasi

Back
Top Bottom