Lissu achana na stori za risasi, panga hoja zako utawafanyia nini Watanzania

- Tanzania inahitaji mtu ambae atakua asset na sio liability.

- Lissu anatakiwa ajionyeshe kwamba yuko fit kimwili, kiakili na kisera, na aondoe habari za huruma huruma.

- Aache habari za kutangazia umma kwamba mwili wake umejaa vyuma na viungo havijikunji maana anakua ameanza kujitangaza kwamba yeye ni dhaifu.

- Anatakiwa awe raisi kwa sababu anauwezo wa kuongoza na kutatua matatizo makubwa ya wananchi na sio kua raisi kwa sababu amepigwa risasi.
Sasa mtu ni dhaifu hivyo harafu umpeleke kwenye kampeni...kweli hii. Lisu ashauriwe apumzike aisee
 
Mbona wewe ni mpumbavu kama yale majuha yasiyotaka kupata habari kwa undani badala yake yanadandia treni kwa mbele? Too shallow to understand things. Wewe beba bango tu. Huna uwezo wa kuingia kwenye vikao vya mijadala.
Tunawaogopa yawezekana mnaumwa corona toka ubelgiji. Nendeni karantini kwanza.
 
Sasa mtu ni dhaifu hivyo harafu umpeleke kwenye kampeni...kweli hii. Lisu ashauriwe apumzike aisee

Kiongozi unasahau vile alita kiwa akamatwe kwa uzembe na uzururaji? Au ni ile ya ukinipiga umenionea na uke iniacha umeniogopa? Mimi naomba tumuache kumwamulia. Mvaaji ndiye anajua wapi kiatu kinambana, akivue ama akiache. Sisi tuombe Mungu kampeni za amani na Mungu atupe raisi safi atakayeendelea na kuboresha maajabu yaliyofanywa na Rais Magufuli katika miaka 5 hii.
 
Achana na stori za kupigwa risasi, mara nani sijui haonekani, sijui nani katekwa, sijui risasi 16. Kamanda piga chini hizo stori. Mshukuru upo hai. Je waliokufa wanamsimulia nani? Mshukuru Mungu, samehe na sahau. Watanzania wameshasikia sana hayo.

Sasa hivi jipange na useme utawafanyia nini watanzania katika elimu, afya, ajira, fao la kujitoa, mikopo ya elimu ya juu, elimu ya sekondari, kilimo, maji, miundombinu, demokrasia, nk

Lisu piga chini stori. Watanzania wameshazisikia sana
Hili niliwahi kumuonya Lema baada ya kutoka Gerezani.Lema kila alipopata nafasi ya kuongea ilikuwa na simulizi za jela na watu aliowaona kule wakiteseka. TL hakatazwi ila anatakiwa a strike a balance kwa kila fursa anayopata kuongea na wananchi,kuhusu risasi kidogo lakini aweze kutuonyesha vision yake.Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa yeye kurudi salma lakini ajitahidi asiwe obsessed na tukio.Kwa viongozi wa marekani amabo walipigana Vietnam na wengine walitekwa na kuteswa lakini mara nyingi wana focus katika wakati uliopo na ujao.
 
Mlamu unachanganya mambo ya kitaifa na maisha binafsi, unapotaka ridhaa ya wananchi kuwa kiongozi wao ni lazima ionekane kujitoa kwa ajili ya wengi sio kulilia au kutetea uhai wako binafsi.

Kama ni risasi ni wangapi wametandikwa na hata kuuawa, sawa si kitu chema ila mbona kukirejea kila unapopata nafasi!

Pamoja na huruma anayoitarajia kutokana na shambulizi lake, yapo mengi ya kuwaambia wananchi yenye maslahi kwa wengi.
Nikuulize swali moja tu. Hivi asingepona, leo hii angewaambia nini wananchi? Tafakari!

Ninachotaka kusema ni kuwa hapo kinchozungumziwa si tu risasi alizopigwa, bali kikubwa ni sababu ya kupigwa risasi.

Ni wangapi wakisema kama alivyosema watapigwa risasi? Halafu mimi nawewe tukae tu na kusema endeleeni kutetea wananchi bila kujali kupigwa risasa? Nakuhakikishia ndugu yangu, kuwa AKILI HIYO WENZAKO BADO HATUJAIPATA NA HATUTAIPATA. Kwetu lamuhimu ni kukemea mpiga risasi kwa kulizungumzia tukio hilo mara kwa mara mpaka wananchi wote wazomee na kukataa kwa akili zote za master minders wa idiolojia hiyo.
 
Ila Lumumba mnawashwa! mbona hunwambii m/kiti stori za madaraja na zahanati tumezichoka
 
Ushauri mzuri japo wengi wamechukia kisa mtu wao kaambiwa ukweli. Akiufanyia kazi atatoa upinzani wa maana mno
 
Utawafabyia nini watanzania ukichaguliwa kuwa Rais?

Lissu; Nilipigwa Risasi!
 
Back
Top Bottom