Lissu achana na stori za risasi, panga hoja zako utawafanyia nini Watanzania

Wajumbe

Senior Member
Jul 26, 2020
136
500
Achana na stori za kupigwa risasi, mara nani sijui haonekani, sijui nani katekwa, sijui risasi 16. Kamanda piga chini hizo stori. Mshukuru upo hai. Je waliokufa wanamsimulia nani? Mshukuru Mungu, samehe na sahau. Watanzania wameshasikia sana hayo.

Sasa hivi jipange na useme utawafanyia nini watanzania katika elimu, afya, ajira, fao la kujitoa, mikopo ya elimu ya juu, elimu ya sekondari, kilimo, maji, miundombinu, demokrasia, nk

Lisu piga chini stori. Watanzania wameshazisikia sana
 
MKANDAHARI

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
3,624
2,000

Sasa wewe kinachokuwasha ni nini hasa? Hiyo ni historia ya maisha yake, hapangiwi na mtu yeyote namna ya kuzungumza. Sisi mashabiki ndio tunapenda kusikia hizo story
 
Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
8,343
2,000
Achana na stori za kupigwa risasi, mara nani sijui haonekani, sijui nani katekwa, sijui risasi 16. Kamanda piga chini hizo stori. Mshukuru upo hai. Je waliokufa wanamsimulia nani? Mshukuru Mungu, samehe na sahau. Watanzania wameshasikia sana hayo.

Sasa hivi jipange na useme utawafanyia nini watanzania katika elimu, afya, ajira, fao la kujitoa, mikopo ya elimu ya juu, elimu ya sekondari, kilimo, maji, miundombinu, demokrasia, nk

Lisu piga chini stori. Watanzania wameshazisikia sana
Kwani akipoteza muda kuongea kuhusu kushambuliwa kwake wewe unapoteza nini?
 
Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
5,724
2,000
Ukimpeleka Lissu kwenye mashule, afya, uchumi nk.. maji marefu sana kwake, hawezi kupiga mbizi.

Kumbuka alivyokuwa bungeni muda mwingi alikuwa anatoa malalamiko tu bila kuwapa wananchi kesho yenye matumaini.
 
Cicadulina

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
792
1,000
Achana na stori za kupigwa risasi, mara nani sijui haonekani, sijui nani katekwa, sijui risasi 16. Kamanda piga chini hizo stori. Mshukuru upo hai. Je waliokufa wanamsimulia nani? Mshukuru Mungu, samehe na sahau. Watanzania wameshasikia sana hayo.

Sasa hivi jipange na useme utawafanyia nini watanzania katika elimu, afya, ajira, fao la kujitoa, mikopo ya elimu ya juu, elimu ya sekondari, kilimo, maji, miundombinu, demokrasia, nk

Lisu piga chini stori. Watanzania wameshazisikia sana
hata wewe lete story nyingine siyo kuongelea habari za watu
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,756
2,000
Achana na stori za kupigwa risasi, mara nani sijui haonekani, sijui nani katekwa, sijui risasi 16. Kamanda piga chini hizo stori. Mshukuru upo hai. Je waliokufa wanamsimulia nani? Mshukuru Mungu, samehe na sahau. Watanzania wameshasikia sana hayo.

Sasa hivi jipange na useme utawafanyia nini watanzania katika elimu, afya, ajira, fao la kujitoa, mikopo ya elimu ya juu, elimu ya sekondari, kilimo, maji, miundombinu, demokrasia, nk

Lisu piga chini stori. Watanzania wameshazisikia sana
Kweli kabisa.
Yani Mbowe na konyagi zake anakaa pembeni anakenua menu kusikiliza stori anazozifahamu na zisizo na majibu.
Hakuna haja ya kupiga stori za aina moja kila siku.
Yapo Mambo mengi yanayotakiwa yajengeke katika fikra za watanzania.
Mfano :- Mfumo wa Elimu.
Mfumo wa uchumi na biashara za ndani na nje,
Kodi kubwa kwa wafanyabiashara.
Mifumo ya Sheria za ardhi.
Mifumo ya makazi. Namna ya kuliwezesha shirika la nyumba kujenga nyumba maeneo ya watu wa chini ili waishi kwa gharama nafuu.
Mifumo ya wananchi kujiletea maendeleo wenyewe na kisheria baada ya kupata ushauri na utaalama toka kwa wataalam bila kutegemea hisani ya wanasiasa hasa watawala; Mfano watu wanakaa sehemu haina daraja na barabara zisizopitika kipindi cha mvua lakini hawana uwezo wa kujipanga na kujenga Daraja lao bila kuingiliwa na Serikali.
Mifumo ya kuyatumia Majeshi yetu kwa ajili ya teknolojia na uzalishaji badala ya siasa.
Kutambua rasmi matumizi ya dawa za asili kwenye hospitali rasmi za dawa za asili huku serikali ikiwa inawafadhili katika tafiti na kuzigharamikia.
Kupunguza mshahara ya Wabunge na Mawaziri na wateule wote serikalini ili fedha hizo ziende kuwalipa Wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wa nyumba kumi mana wao ndio wanaolinda amani katika jamii zetu kabla ya vyombo vya dola kufikiwa.

Kujenga shule za English Medium kila Tarafa ili watoto wa Watumishi na watu wa kipato cha kati wapate shule za kuwapeleka watoto wao kwa gharama nafuu Let say 1,000,000/- kwa mwaka jambo litakaloiongezea serikali mapato lakini kuongeza ajira kwa wasomi wetu.
Kuweka mitaala ya kilimo ,uvuvi na biashara kuanzia shule ya msingi mana imeonekana dhahiri kuwa matajiri wengi wakulima na wafanyabiashara na wafugaji wana Elimu ya Msingi.
 
Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
993
1,000
Achana na stori za kupigwa risasi, mara nani sijui haonekani, sijui nani katekwa, sijui risasi 16. Kamanda piga chini hizo stori. Mshukuru upo hai. Je waliokufa wanamsimulia nani? Mshukuru Mungu, samehe na sahau. Watanzania wameshasikia sana hayo.

Sasa hivi jipange na useme utawafanyia nini watanzania katika elimu, afya, ajira, fao la kujitoa, mikopo ya elimu ya juu, elimu ya sekondari, kilimo, maji, miundombinu, demokrasia, nk

Lisu piga chini stori. Watanzania wameshazisikia sana
Kwa kiasi ninakubaliana na hoja yako kwamba hiyo habari ya kunusurika kifo ya Bwana Tundu Lisu inatosha sasa ikiwa anataka kuchukua nchi.sababu tayari waTanzania wanajua yaliyompata.Ila pia asisahau kuna mambo mengi makubwa kwa wananchi yanayo hitaji kutatuliwa na raisi ajaye.Kimsingi Mwanadamu ana hulka ya ubinafsi ,kwa hiyo ikiwa huonyeshi namna yeye binafsi atakavyofaidika na wewe kuwa madarakani ,hawezi kukupa kipaumbele.maana yake ni nini?ni kwamba kuna yaliyompata Tundu lisu ,yapo mengine yanaendelea kuwapata watanzania wa kawaida katika maisha yao ya kila siku mfano katika sekta za elimu,afya,usalama,ajira,kilimo.na mengine yanayofanana na hayo.kama utatumia muda kidogo kujadili namna utakavyotatua kero hizi na kuzungumzia zaidi alivyonusurika kufa,tunaweza mhesabu ni mtu mwenye kutaka uraisi ili aende akapambane na wale walitaka kumua(kulipa kisasi).kitu ambacho hakina maslahi mapana kwa wananchi.sababu kama nilivyosema watu ni wabinafsi.Kama hawatafaidika wao,watakuacha mwenyewe.

So Chadema na vyama vingine vya upinzani jikiteni kutengeneza sera na hoja za msingi. Huu siyo wakati wa uwanaharakati,ukileta jaziba hufiki popote,watanzania wa siku hizi wana uelewa mpana sana.

Lastly.Muda ni mchache mambo ni mengi so tumieni muda vizuri kuwaelewesha wanachi ,wapiga kura wenu kwamba mnaleta kitu gani kipya.
 
nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
2,398
2,000
Wana ccm wanaogopa siku jembe atakapopanda jukwaani na kuwaga uchafu unaofanywa na wanywa kikombe cha babu wa loliondo. Atawakaanga na mtakubali tu kuwa mwenyekiti wenu hatumpendi. Atatuambia kama sio yeye aliyetaka kumuuwa lissu kwanini alizuia wabunge kwenda kumuona huko hospitali.
 
Wajumbe

Senior Member
Jul 26, 2020
136
500
Kwa kiasi ninakubaliana na hoja yako kwamba hiyo habari ya kunusurika kifo ya Bwana Tundu Lisu inatosha sasa ikiwa anataka kuchukua nchi.sababu tayari waTanzania wanajua yaliyompata.Ila pia asisahau kuna mambo mengi makubwa kwa wananchi yanayo hitaji kutatuliwa na raisi ajaye.Kimsingi Mwanadamu ana hulka ya ubinafsi ,kwa hiyo ikiwa huonyeshi namna yeye binafsi atakavyofaidika na wewe kuwa madarakani ,hawezi kukupa kipaumbele.maana yake ni nini?ni kwamba kuna yaliyompata Tundu lisu ,yapo mengine yanaendelea kuwapata watanzania wa kawaida katika maisha yao ya kila siku mfano katika sekta za elimu,afya,usalama,ajira,kilimo.na mengine yanayofanana na hayo.kama utatumia muda kidogo kujadili namna utakavyotatua kero hizi na kuzungumzia zaidi alivyonusurika kufa,tunaweza mhesabu ni mtu mwenye kutaka uraisi ili aende akapambane na wale walitaka kumua(kulipa kisasi).kitu ambacho hakina maslahi mapana kwa wananchi.sababu kama nilivyosema watu ni wabinafsi.Kama hawatafaidika wao,watakuacha mwenyewe.

So Chadema na vyama vingine vya upinzani jikiteni kutengeneza sera na hoja za msingi. Huu siyo wakati wa uwanaharakati,ukileta jaziba hufiki popote,watanzania wa siku hizi wana uelewa mpana sana.

Lastly.Muda ni mchache mambo ni mengi so tumieni muda vizuri kuwaelewesha wanachi ,wapiga kura wenu kwamba mnaleta kitu gani kipya.
Kabisa, mpaka sasa wananchi hawajui Lisu atawafanyia nini. Stori telling kuhitaji huruma hazitasaidia. Angeanza kupambania changamoto zinazowakumba wananchi.mfano kufungua kesi kupinga kufutwa fao la kujitoa....

Hata hivyo, kama alishindwa kumtaja aliyetaka kumuua akiwa nje ya nchi ataweza akiwa nchini. Acheni kumdanganya Lisu. Deal na issues, zungumzia kero, changamoto, na ufumbuzi wake....be presidential material....
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
7,287
2,000
Hiyo stori ya risasi ni muhimu sana ili kuwajulisha wananchi hatari ya utawala wa kikatili.

Kila mtu anaweza kuzungumza ajira na uchumi, lakini ni watu wachache wanaweza kuzungumza athari za utawala wa kikatili kwa mifano hai wananchi wakaelewa kama Lissu

Lissu aendelee kulizungmzia tukio lile, lakini lazima azungumzie masuala ya Ugali wa wananchi kwa mapana kabisa badala ya kuishia kupapasa papasa tu
 
LURIGA

JF-Expert Member
May 26, 2013
1,623
2,000
Ni ushauri mzuri sana kwa Lissu na wapinzani kwa ujumla. Nikiutazama upinzani wa sasa ni kama umekosa hoja kabisa za kitu gani wataifanyia hii nchi yetu. Wamebaki kulialia tu kwa mambo ambayo hayana tija kwa taifa. Siamini kabisa kwamba kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania ambazo zimejaa matatizo na changamoto za kiuchumi, kisiasa na kijamii wapinzani wakose hoja kiasi hiki. Hata kama serikali iliyopo madarakani inafanya mazuri kiasi gani bado upinzani imara na ulio na dira ya maendeleo ya nchi hauwezi kamwe kukosa hoja za kui-challenge serikali iliyoko madarakani.

Sera pekee waliokuwa nayo chadema wakati wa dr. Slaa ilikuwa ni ufisadi, elimu bure, na kuboresha makazi ya wananchi kwa kushusha gharama za vifaa vya ujenzi. Hizi hoja zilikuwa na mashiko lakini chadema ya sasa sijui inatoka wapi ana inaelekea wapi kisera na hoja za maendeleo ya nchi. CHADEMA NA UPINZANI KWA UJUMLA NJOONI NA SERA NA HOJA MBADALA KWA MAENDELEO YA NCHI ACHENI UANAHARAKATI NA KULIALIA KWA WANANCHI.
 
Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
2,813
2,000
Itasaidia nini hii stori, au itainua uchumi...anapoteana. Huu sio muda wa stori. Ajipange aje na mikakati ya ushindi
Hapo ndipo waafrika tupo nyuma. Nasema waafrika na sio Tanzania maana tatizo la umasikini lipo Afrika nzima kutokana na kukosa ueleo wa neno maendeleo.

Nikufahamishe, maendeleo nambari moja ni kulilia uhai wako au haki ya kuishi kama ukipenda. Kama Einshtein, Isak Newton, Galileo nk wangeuwawa na watawala wa wakati huo sijui ugunduzi huo ungefanywa na nani? Hao wote hasa Galileo alikwenda kinyume na tamaduni za wakati huo na kwa ukweli wengi walipenda auliwe.

Myahudi mpaka leo anapiga kelele ya kuuliwa watu wake na mjerumani. Mpaka leo kuna gumzo kali la kifo cha Yesu msalabani, Olof Palme, Martin Luther king just name them. Kwanini watu wanafanya hivyo? Kwasababu hapo ndipo maendeleo yanapoanzia.

Umesema azungumzia Demokrasia! Hapo nacheka, utazungumziaje Demokrasia bila kutaja kupigwa risasi kwa Lissu? Hapo umebugi, Tafadhali tafakali! Jaribu kurudi nyuma na tafuta sababu za kufuatwa fuatwa kwa Lissu. Naishia hapo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom