Lissu acha kudandia, hoja ya mfumuko wa bei ni ya Mpina. Alikwisha ifikisha Bungeni miezi 8 iliyopita!

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,550
11,879

Huu ndio ukweli halisi!

Mheshimiwa Luhaga Mpina, mbunge wa Jimbo la kisesa, alijitoa kafara,bila kupepesa macho bungeni,na kuichana Live, serikali ya chama chake cha CCM. Akatohoa kila kitu kutokana ndhila wanayopitia Watanzania.
Kutokana na upandaji holela wa bei za bidhaa nchini.

Lissu na Chadema meelewe hilo. Suala la mfumko wa bei,Lissu na Chadema wamedandia hoja ambayo tayari,wabunge wa CCM yenyewe!, walikwisha liona na kuibana serikali hii,ambayo imelalia kwa Upper Class na walamba asali.

Badala ya wananchi na wapiga kura. Tuaenda kwa hoja na uthibitisho mpaka kieleweke. Na wakati Mpina akijitoa muhanga!takribani miezi nane iliyopita!

Lissu alikuwa akipigania kulipwa mafao yake,akiwa huko huko Ulaya,nchini Ubelgiji. Lakini #Mpina alikuwa hapahapa, tena ndani ya bunge, akiichachafya serikali ya chama ambacho ndio pia kimempa nafasi ya kugombea ubunge na kuupata!

Na hilo limemgharimu mpaka kufyekwa jina lake, katika kugombea kuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM pamoja na U-NEC wa CCM.

My take:
Hawa watu kama Mpina. Ndio waterezi halisi wa wananchi ambao tunaowataka Tanzania hii. Na sio wale cwa Msimu kama Lissu, wanaogeresha,huku familia zao zikiwa Ughaibuni.

Na wakishakosa malengo yao wanarudi Ulaya kama kawaida yao.

Asubuhi njema!

10101.
 
Mpina ameisajili Brela?
Jibu unalo kwamba amekwisha isajili Bungeni!

Achana na Brela ya wafanyabiashara. Tutaenda kwa uthibitisho ili kuondoa uongo uongo wa wanadiasa waongo waongo pia walamba asali kwa mkono na ulimi!
 
Akatohoa kila kitu kutokana ndhila wanayopitia watanzania. Kutokana na upandaji holela wa bei za bidhaa nchini.

Lissu na Chadema meelewe hilo! Suala la mfumko wa bei,Lissu na Chadema wamedandia hoja ambayo tayari,wabunge wa CCM yenyewe!, walikwisha liona na kuibana serikali hii,ambayo imelalia kwa Upper Class na walamba asali.
Siyo mashindano tunahitaji solution ya tatizo
 
Hivi mtu akishazungumzia suala lolote lile kuhusu changamoto ziendanazo na ugumu wa maisha nalo pia lina umiliki binafsi kiasi kwamba mtu akishalizungumzia sehemu fulani, basi wengine waliobakia walazimike kukaa kimya, na mjadala wake ndiyo uwe umekwisha!?

Duh! Wakati mwingine nchi siyo ngumu, ila raia wenyewe ndiyo wagumu. Yaani kiongozi akiwa bungeni tena akiwakilisha wananchi wa jimbo lake akitoa mchango wake, basi hoja yenye maudhui sawa na yake isifanyiwe mjadala na watu wengine katika hadhira tofauti!

Je! Hansard za Bunge zinamfanya awe na "copy right" ama "patent right" kuhusu jambo hilo!?
 
Utakuwa umekunywa maji ya chooni wewe. Yaani Mpina ana hatimiliki ya hoja ya mfumuko wa bei kwani ni yeye tu anayeathirika na huo mfumuko wa bei au yeye ndiye ameutengeneza? Badala watu tuunganishe nguvu kuikabili Serikali juu ya madhila haya azungumze Mpina peke yake. Sukuma Gang mna ushamba na ulimbukeni mwingi sana. Kila mwenye pumzi akemee ubadhirifu serikalini ambao unachangia kwenye huu mfumuko wa bei.
 
What is freedom of speech🗨?

Screenshot_20230201-072745_Chrome.jpg
 
Hivi mtu akishazungumzia suala lolote lile kuhusu changamoto ziendanazo na ugumu wa maisha nalo pia lina umiliki binafsi kiasi kwamba mtu akishalizungumzia sehemu fulani, basi wengine waliobakia walazimike kukaa kimya, na mjadala wake ndiyo uwe umekwisha!?

Duh! Wakati mwingine nchi siyo ngumu, ila raia wenyewe ndiyo wagumu. Yaani kiongozi akiwa bungeni tena akiwakilisha wananchi wa jimbo lake akitoa mchango wake, basi hoja yenye maudhui sawa na yake isifanyiwe mjadala na watu wengine katika hadhira tofauti!

Je! Hansard za Bunge zinamfanya awe na "copy right" ama "patent right" kuhusu jambo hilo!?
Halafu mwenyewe kakaa na simu yake anatype huku anatabasamu anajua anaandika cha maana JF watafurahia tutafika nchi ya ahadi tumechoka mkuu😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom