Nashukuru sana mkuu. Nilikuwa sijui kama karanga inawahi kuharibika kiasi hicho. Sasa mbona ukiuonja huo uji wa huo mchanganyiko una ladha nzuri na ni mtamu?Achana na habari za uji huo mnaouita wa "lishe", kiukweli hauna lishe yoyote!! Wataalamu wa magonjwa ya watoto, na wataalamu wa lishe hawashauri kabisa matumizi ya hiyo kitu kwa sababu zifuatazo,
1.Contents za huo uji mnaoita wa "lishe" ni kama 6 hivi (mahindi,soya,ulezi,karanga,n.k.) ambapo hivyo vitu kila kimoja kinaiva katika temperatures tofauti. Kwa hiyo ukichanganya huo mchanganyiko unakuwa katika hatari ya kumlisha mtoto baadhi ya content ambazo eidha zinakuwa zimeiva kupitiliza na hivyo kuharibu virutubisho, au kumlisha contents ambazo hazijaiva.
2.Mchanganyiko wa hivyo vitu pia mara nyingi zinakuwa na virutubisho vile vile (mara nyingi ni wanga, na protini kwa kiasi, hivyo basi hakuna haja ya kuchanganya vitu vingi ambavyo vinakaribiana au kulingana aina ya virutubisho)
3.Pia ukichanganya mseto huo, contents za huo mseto pia zinakuwa na different shelf lives (muda wa kuweza kukaa bila kuharibika), hivyo basi unaweza kuwa unamlisha mtoto vitu vilivyooza. Mfano, karanga huwa zinaoza ndani ya wiki 1-2 tuu; hivyo component ya karanga ndani ya mseto huo, within 2 weeks tuu zinakuwa zimeshaoza tayari!!
Je, kitu gani cha kumlisha mtoto ambae tayari amefikisha umri wa miezi 6 na kuendelea?
Wataalamu wa lishe huwa wanashauri kuwa mtoto apewe a variety of foods (sio kupewa huo uji wa "lishe" kila saa, kila siku,asubuhi hadi jioni). Pia, inashauriwa mtoto apewe chakula mabacho familia inakula, ila kiweze kuandaliwa katika hali ya ulaini ambayo itampelekea mtoto aweze kula vizuri bila kukabwa; Pamoja na kuongezewa "snacks" yaani, milo midogo katikati mara 3-4. Kwa mfano: asubuhi kabisa mtoto akiamka, say saa 1 asbh anaweza akapewa uji wa unga wa mahindi, halafu labda saa nne akanywa chai pamoja na familia (labda akapewa slesi ya mkate uliolainishwa kwa kuchovya kwenye chai ya rangi,kwa mfano), halafu saa saba akala chakula cha mchana ambacho familia inakula (mfano kama familia inakula ugali maharage,ugali ukapondwa pondwa na kulainishwa na mchuzi wa maharage), then saa kumi mtoto akapewa uji wa unga wa ulezi kwa mfano, na kwenye saa moja wakati familia inakula pia akala chakula cha familia (mfano kama familia inakula wali samaki, wali ukachanganywa kwenye mchuzi wa samaki hadi ulainike, na mtoto akapewa pamoja na vipande vya samaki pia).
Hivyo basi, kama una uwezo wa kuwa na unga wa aina tofauti tofauti, ni afadhali ukawa na unga wa aina hizo tofauti tofauti (e.g. unga wa ulezi,unga wa mahindi,unga wa soya separately), halafu ukawa unampa mtoto uji wa tofauti tofauti ili kumbadilishia ladha; kuliko kuchanganya mseto wote huo na kumlazimisha mtoto kunywa uji huo huo, kila saa, kila siku; ndio maana watoto wengi muda wa kunywa huo mseto mnaouita "lishe" inakuwa ni kama vita kwa sababu na wao pia wanachoka ladha hiyo hiyo kila saa. Kama hauna uwezo wa kuwa na unga wa aina hizo tofauti tofauti pia, sio ishu kabisa mtoto wako anaweza kukua vizuri tuu kwa kula chakula cha familia ambacho kiko modified kidogo ili kilainike, na uji mmojawapo kati ya wa mahindi/ulezi au pia hata maziwa kama mtoto wako ni moenzi wa maziwa!!
Ni hayo tuu, mnisamehe kwa maelezo marefu.
chifu77