Lishe kwa mtoto - Unampikia nini mtoto wako (miezi 6-12)

farkhina

Platinum Member
Mar 14, 2012
14,568
16,902
Habari zenu

Leo nimeona ni vyema wana jikoni na wazazi tujadili na tubadilishane mawazo kuhusu lishe za watoto wetu kuanzia umri wa miezi 6 hadi mwaka.....

Nini madhumuni hasa

1)kwa wale watoto ambao hawapendi kula au hatujatambua bado nini wanapenda lakini kuna mzazi yeyote ameona chakula flani kime work kwake basi tu share nasi kujaribu kama kitapendwa pia....


2)tujuzane trick gani unatumia wakati wa kumlisha mtoto binafsi mimi huwa namfunga kwenye kiti chake alafu nampa kijiko au kipaja cha kuku sasa wakati anafungua mdomo kutafuna alichokikamata mie namuwahi kupitisha kijiko cha chakula hii inasaidia sana na tricks nyengine tutazidi kujuzana...


Karibuni wote tujadili au tupia recipe zako.


===============================


Lishe (1) - UJI WA OATS NA NDIZI/APPLE


Mahitaji

Oats kiasi

Apple 1 au ndizi ya kuwiva...

Maziwa...

Sukari (sio lazima)...

Namna ya kutaarisha

Chemsha maji

Weka oats acha zichemke hadi kuwiva

Ponda ponda ndizi vizuri weka maziwa kidogo ipondeke vizuri....

Mimina kwenye oats alafu weka na maziwa acha ichemke kidogo kwa dakika 3

Epua mlishe mtoto.....



Lishe (3) - WALI WA YAI

Mahitaji

Yai 1....tumia kiini tu

Siagi kidogo

Mchele....

Namna ya kutaarisha...

Pika wali kama wa kawaida ila weka maji mengi uwe laini bwabwa wengine wanaita bondo

Ukikaribia kuwiva weka yai ulolivunja koroga haraka haraka uchanganyike vizuri

Weka siagi na chumvi kidogo ukipenda....

Epua mlishe mtoto....


Lishe (3) - KAROTI NA KUKU


Mahitaji

Karoti

Kuku kiasi


Namna ya kutaarisha

Chemsha kuku hadi kuwiva iwe na supu kidogo

Weka karoti na subiria kuwiva...

Toa kuku pembeni alafu mchambue mifupa tupa

Weka katika blenda kuku na katoti na supu yako saga

Tayari kwa kumlisha mtoto

Ukipendeza waweza weka na viazi



Endelea kufuatilia mjadala kwa ushauri na lishe zaidi....
 
Pretty, napenda kweli supu ya maboga na ya carrot. I bet kwa watoto inakuwa nzuri sana pia.

Formulae moja ni kuhakikisha mtoto hakinai chakula kwa kubadilisha mapishi. Samaki wa kuchemsha pia anaweza kuwa ideal. Kumbuka braising kidogo (kumshtua na mafuta kidogo sana kikaangoni kuongeza ladha na harufu nzuri ).

Bibie farkhina sijaona umeongelea mashed potatoes manake zinakuwa na maziwa pia na kumpa mtoto maziwa fresh nahisi kama ni mtihani.

Kosa kuwa tunalofanya ni kumlazimisha mtoto kula ama kumlisha huku analia na mwisho anatapika. Eating time should be fun. Wataalamu wanasema kubadili vyombo pia inasaidia. So a colourful bowl is a necessity
 
......mwanangu yupo 4 yrs now,lakini alipokuwa na umri wa miezi 6 -12 menu yake kubwa ilikuwa asubuhi nilikuwa nampa avocado nusu na ndizi nusu. Nachanganya na mtindi na rice cereal vijiko 2. Anashushia na maziwa 6 ounces.

Mchana lunch ni viazi vitamu au maboga nachanganya na spinach au karoti. Anashushia na maziwa au maji. Hivyo viazi au maboga unaviponda vinakuwa kama uji mzito.

.....usiku pia alikuwa anakula squash, namix na sweet potatoes. Then maziwa kinywaji.

.....Na bado kuna snacks btn meals, waweza mpa maziwa na cooked carrot. Mtoto wa 12 months waweza mpa cookies, akajifunza kula mwenyewe.

Vile vile nilijifunza mtoto akikataa kula usimlazimishe sana,muache baada ya muda akisikia njaa atakula.

Mtoto akiwa anakula muweke kwenye kiti special na tv nzima.
 
Habari zenu

Leo nimeona ni vyema wana jikoni na wazazi tujadili na tubadilishane mawazo kuhusu lishe za watoto wetu kuanzia umri wa miezi 6 hadi mwaka.....

Nini madhumuni hasa

1)kwa wale watoto ambao hawapendi kula au hatujatambua bado nini wanapenda lakini kuna mzazi yeyote ameona chakula flani kime work kwake basi tu share nasi kujaribu kama kitapendwa pia....


2)tujuzane trick gani unatumia wakati wa kumlisha mtoto binafsi mimi huwa namfunga kwenye kiti chake alafu nampa kijiko au kipaja cha kuku sasa wakati anafungua mdomo kutafuna alichokikamata mie namuwahi kupitisha kijiko cha chakula hii inasaidia sana na tricks nyengine tutazidi kujuzana...


Karibuni wote tujadili au tupia recipe zako....


Mniwie radhi kwa uandishi wangu usio rasmin lol

Nimeipenda hiyo trick yeye anakusudia kula nyama lakini anajikuta kachomekewa chakula asichotarajia
 
Watoto wanakinai chakula haraka, hivyo ni vyema kuwa na ratiba ya kumbadilishia chakula kila baada ya siku 2 au 3. Mtoto wetu ana miezi 9 nikimlisha mimi anakataa, akimlisha mama yake anakubali. Ushauri kwa wazazi: Acheni kuwapa watoto wachanga chakula kilicho andaliwa kwa ajili xa watu wakubwa chenye chumvi nyingi.
 
Mwanangu alipokua na umri huo alikua foodie mashallah, asbh anapata uji wa oats mchana natengeza bondo nalikmix na supu km ya kuku , carot, mchicha etc then tunablend unakua km uji anakula vizuri na choo anapata kizuri

MaashAllah wa kwangu anapenda ukubwa anataka kula mwenyewe ati na akila anajiramba utacheka ila vyakula vyake hapendi sana yaani kwa ugomvi nimfanye namlisha yeye baba ake na mie nile apo kidogo atakula siku akiamua hataki kitu ni nyonyo tu nakomajeee
 
Watoto kuanzia mwezi 0-12 hapa katikati wanakumbana na mitihani.

Mtihani wa kwanza ni sindano za chanjo maana kwa sasa ni 2 (miguu yote)

2. Kipindi cha kujifunza kutambaa: kipindi hiki mtihani wake ni kujigonga uso, pua na mdomo kwenye sakafu. Hapa mtoto utamwonea huruma.

3. Kipindi cha kuota meno: Hiki kipindi ni kigumu sana kwa mtoto ni kipindi ambacho mtoto anakuwa na hasira kwa sababu ya maumivu ya fizi, pia anakuwa na homa, joto linapanda sana. Kipindi hiki ndicho watoto hupdnda kuuma chuchu za ziwa la mama kwa lengo la kupata nafuu ya maumivu ya fizi. Hinapotokea hali hii, mama usiomshutue mtoto kwa kumpiga mtoto kofi jepesi makalioni au kumkalipia maana kwa kufanya hivyo utamfanya alie.

4. Kipindi cha kusimama dede: Hapa ni wakati wa kusimama na kuanguka, mara agonge kidevu kwenye meza lakini zaidi ni kuangukia makalio sakafuni.

Kwa kweli Mungu atusaidie katika kuwalea watoto wetu.
 
MaashAllah wa kwangu anapenda ukubwa anataka kula mwenyewe ati na akila anajiramba utacheka ila vyakula vyake hapendi sana yaani kwa ugomvi nimfanye namlisha yeye baba ake na mie nile apo kidogo atakula siku akiamua hataki kitu ni nyonyo tu nakomajeee

Hahahahaha mpe nyonyo mkwe wangu anajua hapo ndo kwenye afya hasaa. ..lol
 
Watoto wanakinai chakula haraka, hivyo ni vyema kuwa na ratiba ya kumbadilishia chakula kila baada ya siku 2 au 3. Mtoto wetu ana miezi 9 nikimlisha mimi anakataa, akimlisha mama yake anakubali. Ushauri kwa wazazi: Acheni kuwapa watoto wachanga chakula kilicho andaliwa kwa ajili xa watu wakubwa chenye chumvi nyingi.

copy mkuu..
 
Farkhina aksante mno kwa uzi mzuri. Utatusaidia wengi.

Wangu ana miezi 5 soon tunaanza mchakato wa chakula. Maziwa ya mama ananyonya usiku tu. Mchana formula sababu kwanza alikuwa hashibi na pia ratiba za ajira.

Naomba kuuliza, tunashauriwa chakula cha mtoto kiwe fresh yaani kipikwe ale. Siyo unapika asubuhi ale jioni. Sasa wenzangu mnafanyaje? H/gs ndo wanapika mchana wakati mpo makazini au?

At least cha jioni mama unaweza andaa as ukiwahi kurudi...including weekends.

Maana hawa H/gs nao umakini unahitajika.
 
Mimi mwanangu hapendi kula lkn anapenda maji sana kwa hiyo nikimlisha nampa kijiko kimoja chakula na vijiko viwili vya maji basi anakula vizuri na anakuwa anameza ata km hataki

Hii pia mie naona inasaidia sana ahsante sana
 
Watoto kukataa kula jamani kuna mtoto wa cousin yangu ana miezi 8 yeye hapendi kula nikagundua mama ake anampa chakula cha nyanya na maungo chakula hicho kina mkinai

Nimemwanzishia chakula chake tatizo ulitaka ale mpigie mluzi akicheka unamwekea kijiko

Uji wa karanga

Chambua karanga zako safisha
Zisage ziwe laini kabisa

Jinsi ya kutayarisha uji

Korogo unga wa karanga kwenye maji tia jikoni koroga mpaka ushike(uwe mzito) acha uchemke uive mpaka uone kama unaganda.

Utakuwa tayari kwa kunywa tia sukari kidogo ni uji mzuri kwa mtoto
 
Thread muhimu kama hizi kibongobongo utaona zinaenda zinafika page moja, mbili.

Tena hapo kwa kujipigia self promo wenyewe sana.

Leta stories za shoga kaenda kwa mganga kalirudisha buzi lake uone, thread itafika mpaka page mia kama ripoti ya Kamati ya Mahesabu ya bunge.
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom