Lishe kwa mtoto - Unampikia nini mtoto wako (miezi 6-12)

Jael

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
66,250
2,000
Mihogo ya sukari na nazi....nimepika jana so sweet
Namna ya kuandaa
. Menya mihogo, ikate katikati kutoa ule uzi
. Ichemshe na maji tu hadi iive ilainike
. Maji yakikauka katia kitunguu nusu, hoho kipande kidogo, mafuta kijiko kimoja cha chakula, kwangulia carrot, weka sukari na tui la nazi acha ichemke
. Nazi ikibaki kidogo, koroga koroga ili iwe rojo
Msosi upo tayari kwa kuliwa. Ni tamu hiyo bad luck mwanangu aligoma kula nikala mwenyewe chote nikamaliza
Hahahaaaa! Vyakula vya watoto huwa ni vitamu sijui kwanini wao huwa hawavipendi.
 

Freelancer Wakala

JF-Expert Member
Feb 6, 2016
1,207
2,000
Ngoja nikioa ntafuata,Maelekezo yote hayo Ahsante wandugu na Wanachama Wa JF-Members.Nimependa comment zenu imekaa safi sana.
 

mimi.mimi

Senior Member
Jul 11, 2013
135
225
Jaman mimi naomba msaada wanangu ana miezi 5 na nusu ila alipata toka jtano alikua anakataa kunyonya mpaka namlazimisha. Ijumaa jikaendabkumpima kwani alikaa anachemka. Nilimuanishia quinini kwaninalikua na maralia , kuanzia hapo anatapika tuu akiona nikimpa dawa, nikimpa uji au maziwa nikutapika tuu. Kinacho nisumbia sana nikutonyonya kabisaaaaa yaani hataki kuona nikilio utazani umemlambisha limao. Mpaka leo tokea jmosi . msaada jaman.
 

NANDERA

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,029
2,000
mi wangu anapenda ugali maharagwe ana miezi mi 8 sasa cjui kurithi au? hata niandae nn yeye nguna na ndondo tu,
hahahahaaa.....umenifanya nicheke. Hiyo ya kurithi aisee ipo. Mama yangu aliniambia nikiwa mdogo toka nimeanza kukaa chakula changu kikuu kilikuwa maharage. Ndo chakula pekee nilichokuwa nakula kwa hiari. Kabla hayajarojeka yanawekwa kwenye sahani naokota moja moja kama karanga. Huyu wa kwangu nae hivyo hivyo. Ana miaka 8 lakini maharage ndo mboga pendwa.
 

Nkasumuni

JF-Expert Member
Nov 18, 2015
450
250
Ulishaji watoto wa miezi 6-59.
ni muhimu kumwanzishia mtoto chakula kikamilifu akifika miezi 6 maana kabla ya hapo mtoto anatakiwa anyonyeshwe tuu. chakula kamili ni kile chenye makundi yote na chakula kwa viwango vya kufaa kulingana na mahitaji ya mtoto.
Kuna aina ya boga ambalo ni zuri sana kwa chakula cha mtoto na bei yake ni nafuu na lina virutubishi kwa wingi linaitwa butter nut.
sijui kiswahili chake ila unalichemsha kama boga la kawaida na kuliponda na cream kidogo na maziwa kidogo halafu unamlisha mtoto.
 

CharmingLady

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
18,117
2,000
Habari wanajukwaa... Nimekutana na hii nikaona ni vyema kushare nanyi. Sijui kama ipo humu tayari kama ipo naomba mniwie radhi.

KARANGA NI SUMU KWA MTOTO:KUCHANGANYA KARANGA KWENYE NAFAKA(UNGA WA LISHE) NI SUMU HATARI
Posted on AUGUST 3, 2015 9:30 PM by AFYABORAKWAMTOTO
Matumizi ya karanga kwa uji wa mtoto ni vizuri sababu inamwongezea virutubisho ,mafuta na kumsaidia kulainisha choo ila karanga haitakiwi kukaa kwa mda mrefu baada ya kusagwa.Karanga inatabia ya kutengeneza fangasi hivyo utakapo andaa nafaka(mfano -ulezi,mahindi,mchele,ngano….) za kutengeneza unga wa lishe haipaswi kuchanga’nya na karanga ,iwapo utasaga nafaka usichanganye na karanga,karanga saga pembeni na isiwe nyingi saga ya kutosha itakayo tumika wiki moja (siku 7) na unatakiwa uhifadhi sehemu kavu na safi kwenye chombo cha plastik chenye mfuniko.


Utakapo pika uji baada ya dakika 10 ongezea karanga vijiko 2-3 vikubwa ,koroga na acha karanga iive vizuri ndio uepue tayari kumpa mtoto,uji wa lishe unatakiwa kupikwa kwa mda mrefu sichini ya dakika 35-45 moto usiwe mkali ,sababu huo mchanganyiko wa nafaka na karanga uive vizuri lasivyo mtoto ataharisha.
[paste:font size="6"]JINSI YA KUANDAA KARANGAChambua karanga vizuri ondoa zile mbovu na pepeta kwenye ungo,andaa moto usiwe mkali mdogo tu, bandika sufuria na kukaanga bila mafuta zikibadili rangi kidogo epua. Anika juani zikikauka toa maganda yake na kuchambua tena kutoa zilizoungua au mbovu ,tayari kusagwa kwa blender au kutwanga na kinu au peleka mashine ila hakikisha unafanya kwa hali ya usafi. Baada ya kusagwa hifadhi kwenye chombo cha plastik na kufunika hakikisha isikae zaidi ya siku 7.[/paste:font]

[paste:font size="6"]MADHARA YA KUCHANG’ANYA KARANGA NA NAFAKA ZA(UNGA WA LISHE) WAKATI WA KUSAGA!
Karanga inatabia ya kuotesha fungus na kutengenza sumu ya toxin inakuja kuadhiri ini la mtoto na kumpelekea kupata saratani ya ini daktari bingwa wa watoto hospital ya muhimbili Dr Masawe anashauri karanga iandaliwe kidogo na itumike wakati wa kupika uji , karanga inatabia ya kuungua / kunata kwenye sufuria mapema kabla uji haujaiva, hapo unakuwa unapoteza vitutubisho vyote vilivyomo hivyo ni vizuri ukafatilia maelezo nilio toa hapo juu jinsi ya kutumia karanga kwa njia sahihi.[/paste:font]


Ushauri wa afyaborakwamtoto


Unaponunua / tengeneza unga wa lishe usinunue / kutengeneza wenye mchanganyiko wa

1:Nafaka zaidi ya mbili yani kama ni (mahindi,soya,uwele,mtama na nyinginezo) badala yake nunua wenye nafaka 1-2 tu ,kwani mchang’ayiko mkubwa sio mzuri kwa mtoto unahatarisha afya yake sababu utumbo(mfumo wa mmeng’nyo) wake hauna uwezo wa kumeng’enya vyote hivyo kwa wakati 1bado ni mdogo na utamfunga choo2:Usinunue unga wa lishe wenye soya ndani kwa watoto chini ya miaka 2


3:Usinunue uji wa lishe wenye mchanganyiko wa karanga
 

chifu77

JF-Expert Member
Aug 2, 2014
904
1,000
Habari za asubuhi wadau. Poleni kwa janga la sukari. Naombeni kujua namna ya kuandaa mchanganyiko sahihi wa uji wa lishe kwa ajili ya matumizi ya watoto nyumbani. Mfana, kilo ngapi za mahindi, soya, ulezi n.k.
 

Peace92

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
247
225
mahindi ya njano kilo mbili ngano ambayo haijakobolewa kg moja soya kg moja mchele kg moja karanga kg moja ulezi nusu nadhani nimemaliza
 

MimiT

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
602
500
mahindi ya njano kilo mbili ngano ambayo haijakobolewa kg moja soya kg moja mchele kg moja karanga kg moja ulezi nusu nadhani nimemaliza
Sijaona mahindi ya njano miaka sasa. Wapi yanapatikana? Au ni yale ya bisi?
 
Top Bottom