Lishe kwa mtoto - Unampikia nini mtoto wako (miezi 6-12)

Viazi vitamu pia ni chakua kizuri kwa watoto, unavichemsha na carrot unablend au unaviponda ponda kwa kijiko, unaweza kuweka maziwa au supu ya nyama
Pia hivo hivo unaweza kupika butternut, sijui kwa kiswahili inaitwaje unachanganya na maziwa au supu ya nyama
Screenshot_2016-01-30-12-06-27.png

Hiyo ndio butternut

Pia matunda unayablend badala ya kumix maji unamix na maziwa inakua na ladha nzuri sana mi nshajaribu papai na maziwa inakua ladha nzuri mnoo, Avocado na maziwa pia ndizi sukari
 
Viazi vitamu pia ni chakua kizuri kwa watoto, unavichemsha na carrot unablend au unaviponda ponda kwa kijiko, unaweza kuweka maziwa au supu ya nyama
Pia hivo hivo unaweza kupika butternut, sijui kwa kiswahili inaitwaje unachanganya na maziwa au supu ya nyama
View attachment 320132
Hiyo ndio butternut

Pia matunda unayablend badala ya kumix maji unamix na maziwa inakua na ladha nzuri sana mi nshajaribu papai na maziwa inakua ladha nzuri mnoo, Avocado na maziwa pia ndizi sukari
Vipi kuhusu kuchanganya dagaa na maembe?
 
Eve mbona liko kama boga? Au ni kitu gani hiki?
 
Mihogo ya sukari na nazi....nimepika jana so sweet
Namna ya kuandaa
. Menya mihogo, ikate katikati kutoa ule uzi
. Ichemshe na maji tu hadi iive ilainike
. Maji yakikauka katia kitunguu nusu, hoho kipande kidogo, mafuta kijiko kimoja cha chakula, kwangulia carrot, weka sukari na tui la nazi acha ichemke
. Nazi ikibaki kidogo, koroga koroga ili iwe rojo
Msosi upo tayari kwa kuliwa. Ni tamu hiyo bad luck mwanangu aligoma kula nikala mwenyewe chote nikamaliza :p:p
 
Habari zenu

Leo nimeona ni vyema wana jikoni na wazazi tujadili na tubadilishane mawazo kuhusu lishe za watoto wetu kuanzia umri wa miezi 6 hadi mwaka.....

Nini madhumuni hasa

1)kwa wale watoto ambao hawapendi kula au hatujatambua bado nini wanapenda lakini kuna mzazi yeyote ameona chakula flani kime work kwake basi tu share nasi kujaribu kama kitapendwa pia....

2)tujuzane trick gani unatumia wakati wa kumlisha mtoto binafsi mimi huwa namfunga kwenye kiti chake alafu nampa kijiko au kipaja cha kuku sasa wakati anafungua mdomo kutafuna alichokikamata mie namuwahi kupitisha kijiko cha chakula hii inasaidia sana na tricks nyengine tutazidi kujuzana...

Karibuni wote tujadili au tupia recipe zako.

===============================

Lishe (1) - UJI WA OATS NA NDIZI/APPLE

Mahitaji

Oats kiasi

Apple 1 au ndizi ya kuwiva...

Maziwa...

Sukari (sio lazima)...

Namna ya kutaarisha

Chemsha maji

Weka oats acha zichemke hadi kuwiva

Ponda ponda ndizi vizuri weka maziwa kidogo ipondeke vizuri....

Mimina kwenye oats alafu weka na maziwa acha ichemke kidogo kwa dakika 3

Epua mlishe mtoto.....

Lishe (3) - WALI WA YAI

Mahitaji

Yai 1....tumia kiini tu

Siagi kidogo

Mchele....

Namna ya kutaarisha...

Pika wali kama wa kawaida ila weka maji mengi uwe laini bwabwa wengine wanaita bondo

Ukikaribia kuwiva weka yai ulolivunja koroga haraka haraka uchanganyike vizuri

Weka siagi na chumvi kidogo ukipenda....

Epua mlishe mtoto....

Lishe (3) - KAROTI NA KUKU

Mahitaji

Karoti

Kuku kiasi

Namna ya kutaarisha

Chemsha kuku hadi kuwiva iwe na supu kidogo

Weka karoti na subiria kuwiva...

Toa kuku pembeni alafu mchambue mifupa tupa

Weka katika blenda kuku na katoti na supu yako saga

Tayari kwa kumlisha mtoto

Ukipendeza waweza weka na viazi

Endelea kufuatilia mjadala kwa ushauri na lishe zaidi....
Kuna website ya Mtoto Wangu ambayo nafikiri wazazi wanaweza kupata mambo mengi kuhusu mototo tangu siku ya kwanza na kuendelea.
 
Back
Top Bottom